kitendo alichokifanya lowasa kuonyesha bashasha na watu wanaokamata wabunge wa chama chako Lema yupo ndani,mwalimu kakamatwa,lisu anakesi kibao,sugu alikamatwa unaipataje furaha ya kuhag na kinana,kujichekesha mbele ya raisi. even president alishangaa yote ninayowafanyia lakini hajastuka is a miracle.
Lowasa aangaliwe asije akawa usalama akatuchora tu kumbe anadisplay upande wa pili,tahadhari muhmu kwa kuzingatia aliyoyafanya bwana Augustine mrema
watu tunajiandaa na Ukuta wewe unajichekesha na wstu ambao tarehe moja huenda wakatuvunja viuno km si kutufunga bila kesi
lowasa katika mazingira haya smile kwa kinana na magufuli inatoka wapi, it raises more doubt. tusije kusacrife for nothing "km unatraitor#
Tuache uchochezi.
Taifa hili linahitaji watu wenye hekima kama Kinana , Pengo na Lowasa.
Kinana hajawahi kuwa na uadui na mtu.
Tuache fitina na majungu.
Kinana ni mwanasiasa tangu enzi za JK , Kinana alisimama kidete kupambana kutetea chama chake kwenye majukwaa ya kisiasa.
Alifikia mahali akawa anapingana na wenzake kama akina Np kwa kueneza siasa za chuki binafsi na kumshauri ajikite kwenye kujenga chama badala ya majungu na fitina.
Kinana anajua umuhimu wa siasa za majukwaani na nadhani hata yeye angependa kuona siasa na mikutano ya jadhara inafanyika . Kinana sio muoga wa kuingia kwenye ulingo wa majukwaa ya kisiasa.
Kusema eti Lowasa asisalimiane na Kinana ni kufilisika kisiasa. Kinani ni mwanasiasa bora dana ndani ya CCM ndio maana wakati wa JK alipambana kwa hoja kujenga chama chake bila kuingiza vyombo vya dola.
Hata Magufuli anapenda kuona wapinzani wake wanakaa kwa raha kwa kuheshimiana alimradi kukosoana kwa staha bila maneno ya kuudhi.
Kila chama ni lazima liwe na wazee wenye hekima na busara wanaoweza kukaa mezani na kuzungumza juu ya amani ya nchi.
Ndio maana Warioba na Salmu A. Salim walidhalilishwa sana na vijana wa CCM kwenye mchakato wa katiba mpya lakini hawakuonyesha chuki na kupaniki. Walijua ni utoto tu. Wakaendelea kushirikiana nao. Kinana ni Mzee wa siku nyingi na ametoka mbali na Lowasa. Wametofautiana kisiasa tu lakini sio maadui.
Siasa mukiijenga kwa misingi ya uadui basi hamtufai kabisa. Siasa tunataka iwe ni tofauti za namna mtakavyotuletea maendeleo na sio namna mnavyoweza kutukanana na kujenga uhasama dhidi ya watu.