Swali la kwamba Lowasa ni Mwizi au sio mwizi wakuulizwa ni wenye vyombo vya uchunguzi,mahakama na intelijensia.
Wapinzani walipokea toka kwa CCM wenyewe waliokua wanaendesha siasa za kikabila,kikanda na kidini.
Hayo ndiyo waliyotumia kumpiga vita Lowasa. Walianza tangu enzi za chama kimoja ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika.. Hata ndani ya CCM hiyo vita ya kupakana matope ipo na ndiyo inayotumika kuwagawa kimakundi.
Leo hii kuna CCM wanaotaka kupata fursa ya kula mema ya nchi kupitia madaraka wameshaanza kudai wenzao wafukuzwe kwenye chama kisa wanaona kuwa Mkulu hatoshi kwenye uenyekiti mana hajawahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kwenye chama.
Ukumbuke kuwa hata ndani ya CCM kilichosababisha Lowasa akatwe sio ufisadi mana huko hakuna msafi hata wa kuangalia kwa darubini. Kilichomtoa Lowasa ni Afya yake kwani wakati ule ilidorora sana.
Na kwa mziki wa wapinzani wake waliikua wanatumia kila mbinu kumdhibiti ili asije akaingia ikulu akawaadhibu bila huruma na woga wao wa kulipizwa visasi. Hapakuwa na jinsi zaidi ya kumkata.
Hata hivyo Wananchi ndio wanaoona usafi wa Lowasa na sio adui zake kisiasa.
Nisingetegemea mtu maarufu kama Lowasa kusifiwa na wapinzani wake kisiasa.
Na pia nisingetegemea wapinzani kuendelea kumpinga mtu ambaye ameamua kukipinga chama wanachotaka kukitoa madarakani.
Ni sawa kama leo hii kwa Magufuli , sisi wananchi ndio tunamuona anajitahidi lakini wanasiasa hawajamkubali.
Ni kawaida kwenye siasa. Na ndio maana wanamwambia Magufuli ahame Chama.
Tofauti ya Lowasa na wanasiasa wengine ni kuwa hatumii siasa za kutukana watu.
Kura alizopata ni ushahidi tosha kuwa wananchi ndio waliokua wanamuhitaji na sio wanasiasa. Mbowe aliliona hilo. Kwa katiba yetu na tume inayosimamiwa na makada wa CCM kuanzia kwenye vijiji,wilaya ,mikoa na vyombo vya dola Lowasa kubakiziwa kura mil. 6 ni ushindi kwa UKAWA.