Lowassa kakosea? Hapana, tujikumbushe ushauri huu

Lowassa kakosea? Hapana, tujikumbushe ushauri huu

Ifikie mahali penye ukweli tupaseme, acheni kupaka vitu mafuta kwa mgongo wa chupa inamaana mtu akitaka kujisafisha na maovu yake aamie ukawa ety
 
Hazina tija kwa sasa

Natamani kuamini haya maneno mazuri kabisa uliyoyasema, ila nashindwa kwa sababu siamini kama nikiamka kesho nitakuta haya yamebaki au tayati utakua umebadilisha kauli kuwa haya ya leo si mali kitu,kama ulivyobadilisha yaleee ya mwakaa ule kuhusu huyu LOWASA. mkuu Yericko Nyerere hivi kwanini nikuamini tena???
 
Makala hii ni marudio, niliiandika mwaka 2015 baada ya Mh Edward Lowassa kujiunga na Chadema. Lengo la kuirudia makala hii ni kujibu mjadala unaoendelea hivi sasa kuwa Mh Lowassa alikosea aliposhauri kuwa Chadema sasa ijikiti kwenye lengo la kisiasa la kushika dola badala ya kuendelea na harakati zaidi..

....................
Huwezi kuwa Mwanasiasa bila kwanza kuwa mwanaharaka, lakini unaweza kuwa mwanaharakati bila kuwa mwanasiasa, Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni NJIA azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya
njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa
lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni
mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani.

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa ya chama chake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo
huo huhanikizwa katika siasa. Uzalendo makazi yake ni kwa mwanaharakati na sio kwa mwanasiasa, lakini uzalendo huo hulindwa vema chini ya mwanasiasa madhubuti.

Mwanaharakati hunyooka kama kamba katika misimamo yake, na mwanasiasa hutembea katka fursa za kisiasa. Chama cha siasa lengo ni kushika dola kwanza, kisha kuwatumikia watu wake kwamisingi ya itikadi na ilani yake, na harakati na mwanaharakati lengo lake ni usawa wa maisha kati jamii na haki za kiraia zaidi tu.

Ni Mtanzania mjinga tu na asiyelitakia mema taifa hili ndie atakayepinga Lowasa asiende Upinzani. Tunataka kulikomboa taifa toka mikononi mwa ccm, kila nyenzo iliyombele yetu tutaitumia na kila mwenye uthubutu tutakuwa nae,

Ccm itoke kwanza na mengine yatafuata, Kama Lowasa amekubali itikadi ya Chadema nani mwenye kuzuia ujio wake? Vyama vya siasa ni sawa na masinagogi, mtu akitubu na kujutia madhambi yake huyu pepo ni yake!

Karibu Lowasa, Karibu mawaziri wote, karibu makada wote, karibu nawe Jk kwakuwa kazi tuliyokutuma kuiua ccm umeikamilisha.

Nchi hii ni ya watz wote, na Upinzani ni wawote sio mali ya mtu ama kikundi. Siasa ni sanaa ya ajabu sana, haina rafiki wa kudumu, wala haina adui wakudumu. Kwa miaka zaidi ya tisa nyimbo hiyo hiyo mara Lowasa fisadi, mara oooh mwizi, wanaohubiri hayo ni viongozi wa ccm,
Wamesahau mifumo ya utendaji kati ya serikali na dola ilivyo badala yake wanafanya siasa.

Ukiuangalia na kuuchambua mfumo wa utendaji wa vyombo vyq ulinzi na usalama vinavyotumia muundo wa westan Secur utaona kuwa Lowasa ni mtu safi KABISA, ila siasa ndizo zimemdhihaki na kumdhariri kabisa.

Nataka kuzungumza dhana ngumu kidogo machoni pawengi, lakini hima nitaeleweka bila mawaa wala chembe ya makunyanzi. Nazungumza kama mtaalamu wa mifumo ya kiulinzi duniani hasa kile ninachokifahamu, nikiangaza mifumo ya kiusalama ya Franks Secur, Westm secur, Latino secur, Kremlin secur.

Siasa tuiache kando utaalam uchukue nafasi yake, na hapa nataka tujikite kuuangalia mfumo na muundo wa utendaji wa Westan secur na vyombo saidizi vyake katika kulitumikia taifa chini ya Westan secur

Nchi zote ama karibu zote Usalama wa Taifa ni idara au shirika lililochini ya Ofisi ya Rais kwa zile zinazoendeshwa kwa mfumo wa Madola, na zile za kifalme huwa chini ya Waziri Mkuu, hii inamaana kuwa mkuu wa idara hiyo anaripoti kwa rais au kwa Waziri mkuu mojakwamoja, pia mkuu wa idara hii huteuliwa na rais, Waziri mkuu au Bunge kwakuzingatia vetting maalumu iliyochini ya command ya ndani.

Miuundo ya utendaji wa idara au shirika hilo umegawanyika katika sehemu kuu sita, tano, au tatu kulingana na mahitaji ya wakati huo, ambazo kimsingi ni idara ndogondogo ndani ya idara hiyo au shirika hilo kubwa. Mfano ni idara ya mambo ya ndani, idara ya siasa, idara ya mambo ya nje, idara ya uchumi, idara ya ukusanyaji taarifa, idara ya uchakataji taarifa na idara ya vita na teknolojia.

Hapa nataka kuzungumzia idara ya siasa ambayo ndio tunayokumbana nayo mtaani kila kukicha na tunashirikiana katika maandamano nk,

Kwamfano nchini Urusi ambako nchi nyingi zinaiga ikiwemo Tanzania, Idara hii nayo ina vitengo mhimu vya kiutendaji ikiwemo ulinzi wa chama na serokali, sera za kisiasa na muundo wa siasa kutegemeana na chama kilichopo madarakani wakati huo.

Pia idara hii inajukumu la kufuatilia na kutambua mienendo ya wanasiasa viongozi na wale wote watu maarufu katika taifa, bila kusahsu kufuatilia mawasiliano yao, baruapepe zao, mizunguko yao ya kila siku, vyakula vyao vya kila siku, vipato vyao nk.

Idara hii pia imepewa jukumu la kuwalinda viongozi wa kisiasa (mawaziri na wabunge) kwa saa 24 bila kukoma. Mfano, Rais hulindwa na watu 40 wanaoonekana na 48 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka.

Makamu wa Rais hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 10 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka

Waziri mkuu hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 8 wasionekana hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2) zingatia kukiwa na hali ya hatari kiwango cha ulinzi huongezeka.

Mawaziri hulindwa na watu 3 wanaoonekana, na 5 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def s2).

Majukumu ya walinzi wanaooneka na wasioonekana yanatofautiana na kila mtu kati yao huripoti kwa boss wake,
Wale walinzi wanaoonekana huripoti kwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, na wale wasioonekana huripoti kwa rais kila mmoja kwa wakati wake bila wao kujuana.

Hii inamaana kuwa kila anachotaka kufanya ama anachofanya waziri yoyote kabla hajakitenda basi taarifa huwa mikononi mwa rais na mkurugenzi wa Usalama nchini.

Wale wanaoonekana wanaomlinda Rais huripoti kwa mkurugenzi na mnadhimu, wale wasioonekana 10 huripoti kwa rais moja kwa moja, na 30 huripoti pande zote tatu lakini kwa umakini mkubwa bila kujuana.

Sio nia yangu kusafisha wanasiasa, bali nia yangu nikukuelezeni kitaalamu mfumu wa ulinzi nchini unavyoendeshwa na madhari ya kisiasa kuwa waziri fulani ni mwizi ama fisadi kwa dhana ileile ya kisiasa.

Kwenye medani ya siasa huko kuna filosofia tofauti kidogo ambayo hutafsiri uwajibikaji kisiasa katika dhana inayokinzana na uhalisia wa kiutaalam katika mifumo ya kiulinzi.

Hapo sijazungumzia intelligence ya jeshi la Polisi ambayo nayo ni mdau, na kwa nchi kama Israel hiyo ina nguvu sana, pia sijaigusa Tanzanian Military Intelligence ambayo kwa nchi kama Urusi ndio mwamuzi wa mwisho katika muktadha wa taifa hilo.

Hii ndio ya tofauti ya siasa, harakati,na taaluma. Chadema na UKAWA wamevuka ngazi ya uanaharakati na kuwa vyama rasmi vya KISIASA,
Harakati zipo kwa akina Kibamba, Kijo Bisimba, Maria Sarungi, Mr Sungusia nk...

Sisi wengine ni wanasiasa, na lengo kuu la siasa ni kushika dola ndipo tutatekeleza yale tuyanenayo juu ya umma. Silaha yoyote iliyo mbele yetu tutaitumia ilimradi inaiondoa ccm na mfumo wake unaolitafuna taifa hili.

Nakubaliana na wewe.
Kwa sasa CCM ya sasa imekua ya wanaharakati. Ndio maana imekua na hofu na inashindwa kujikita kwenye sheria na katiba badala yake inaendesha mchi kwa matamko ya kila siku.

Chadema ikijipanga kisiasa itaiondoa CCM madarakani kisayansi kwenye chaguzi zijazo.

Tatizo chadema ina vijana wanaofikiri kuwa kila tajiri wa nchi hii ni mwizi na fisadi. Jambo ambalo linaleta fikra za kimaskini. Fikra hizi zimehamia ndani ya vijana wa CCM ambao sasa wanatafuta kila namna ya kupata madaraka kwa kufanya harakati dhidi ya matajiri na wafanyakazi. Kila sekta sasa inashikiliwa na wanaharakati ndani ya CCM .Wametoka kwenye jukumu la kuongoza nchi na kusimamia uchumi wa taifa na kuleta unafuu wa maisha wamebaki na harakati za kupambana na maoni ya wapinzani na kutafuta wale wanaotoa wazo au fikra mbadala.

Chama cha siasa makini hakina ulazima wa kufikisha kila taarifa kwa kutumia maandamano au mikutano ya badhara wakati kuna viongozi wa ngazi zote wenye uwezo wa kuitisha vikao ngazi mbalimbali.
Ni suala la kutunga waraka unaohusu jambo fulani na kuusambaza mpaka ngazi za chini.
Mfano sudhani kuwa kuna Waraka unaohusu msimamo wa chadema juu ya kupigwa marufuku vyombo vya habari huru na vya umma kutangaza live bunge n.k , n.k.

Hali hii inapelekea Chama kuwa ni cha kiharakati na kimatukio. Tukio liputa basi agenda inaishia hapo bila kumbukumbu yoyote ya kimaandishi.Na wanaopata fursa ya ya kupata taarifa mara nyingine sio wanachama kwani hakuna vikao vya ndani vya kupeana taarifa.
Kwenye maandano hua hakuna mijadala ya kina zaidi ya mihemko inayoishia kutukana na kukashfu viongozi wa serikali amba kwa awamu hii ni marfuku hata kuwataja kama sio kwa maana ya kuwasifia.

Lowasa kwa uzoefu wake wa siasa akaligundua hilo. Aligundua kuwa awamu hii hakuna chama kitakachoruhusiwa kumtaja mwizi au fisadi kama kiki ya kujipatia umaarufu kikapona.
Awamu hii ukihoji tu kuwa nyumba na mashirika ya umma kwa nini yaliuzwa kinyemela na kwa bei chee basi ujue utaitwa mchochezi na utaishia kukamatwa .
Ukihoji suala la wizi unaitwa mchochezi.

Kwa hiyo kwa sasa haiwezekani kutegemea kufanya harakati za kimaandamano ili kupata umaarufu wa chama au mtu.
Ndio maana mpaka sasa kuna watu na wabunge ndani ya chadema wameanza kupoteza umaarufu kwa sababu tu walitegemea agenda moja tu ya kusimama na kumtuhumu mtu kwenye majukwaa. Ni rahisi kusimama na kusema kuwa mtu anauza madawa ya kulevia China au Itali bila kueleza ni vipi watu wengi watanufaika au kutonufaika na wachina walioamua kununua madawa na kumfanya mtanzania huyo kuwa bilionea.

Ni lazima chama kiwe na agenda za kudumu za kushika dola. Mfano kama agenda ni mafisadi itakuaje sasa wakati Magufuli anaonekana na wananchi wameshaamini kuwa anayatumbua. Je, sasa upinzani utatoweka kwa sababu ya kutumbuliwa kwa majipu tu wakati mipango ya kukuza uchumi bado haijawa na uelekeo huku maisha yakiwa magumu.

Chadema kiweke sasa mikakati kama serikali iliyokuwa madarakani ikawekwa pembeni na inajiandaa tena kurudi. Hii ni kutokana na kuwa na wanachama ambao walikua madarakani na wenye uzoefu mkubwa wa kusimamia dola bila kuyumbisha umoja wa taifa. Jambo ambalo kwa sasa CCM wanapwaya sana kutokana na kuendesha siasa za hasira na chuki dhidi ya wananchi wasiowaunga mkono.
Wengi hawakumwelewa lowassa.
Chadema imetumia fedha nyingi kujitangaza, naona wamefanikiwa kujulikana.

Sasa ni wakati wa kuweka mikakati ya kuchukua dola. Chadema ina watu wakubwa ndani ya chama ambao wanajua mifumobya nchi kiusalama.

Ni wakati wao wa kufanya mikakati ya kiakili kushika dola.
Kwa nch za kiafrika kushika dola kwa maandamano ni kujisumbua bure, cha zaidi mtaishiwa kuuwawa.

Niwakati wa ukawa kuwa na timu ya strategy isiyozidi kumi, timu yenye kuaminiana kuhakikisha na wao wanafanya siasa ya kiutu uzima.

Nadhan wakubwa waliopevuka wamenielewaa
 
Lowasa anatoa misaada au?
Lowassa HAFAI hata kama sasa unageuka kumsafisha

Aliitumikia serikali dhalimu ya CCM na ndiye yy aliongoza kupiga kura kuikataa rasimu ya Warioba!Anahurumia umaskini wa watz leo akiwa hayupo madarakani,mbona alipokuwa hadi PM hakuonyesha kuwahurumia watz?

Mbowe na Lowassa ondekeni CHADEMA mtuachie chama chetu!Lengo la Mbowe ni kuwa tu Kiongozi wa Wapinzani Bungeni apewe heshima na ving'ora,hawa watu wawili HAWANA hata chembe ya mikakati kushika dola

We want Dr Slaa and Mnyika back
 
duh mabandiko ya mihemko ndio shida yake....they always come back and bite you in the a....se!
Mediocre ni nani sasa kwa hapo?
 
Mtume (S.A.W) amesema "umaskini ni nusu ya ukafiri". Tumekuwa wanafiki na waongo sababu ya shida zetu. Kila tukiamka tumekuwa tukijisaliti sisi wenyewe.
Nakubaliana na wewe.
Kwa sasa CCM ya sasa imekua ya wanaharakati. Ndio maana imekua na hofu na inashindwa kujikita kwenye sheria na katiba badala yake inaendesha mchi kwa matamko ya kila siku.

Chadema ikijipanga kisiasa itaiondoa CCM madarakani kisayansi kwenye chaguzi zijazo.

Tatizo chadema ina vijana wanaofikiri kuwa kila tajiri wa nchi hii ni mwizi na fisadi. Jambo ambalo linaleta fikra za kimaskini. Fikra hizi zimehamia ndani ya vijana wa CCM ambao sasa wanatafuta kila namna ya kupata madaraka kwa kufanya harakati dhidi ya matajiri na wafanyakazi. Kila sekta sasa inashikiliwa na wanaharakati ndani ya CCM .Wametoka kwenye jukumu la kuongoza nchi na kusimamia uchumi wa taifa na kuleta unafuu wa maisha wamebaki na harakati za kupambana na maoni ya wapinzani na kutafuta wale wanaotoa wazo au fikra mbadala.

Chama cha siasa makini hakina ulazima wa kufikisha kila taarifa kwa kutumia maandamano au mikutano ya badhara wakati kuna viongozi wa ngazi zote wenye uwezo wa kuitisha vikao ngazi mbalimbali.
Ni suala la kutunga waraka unaohusu jambo fulani na kuusambaza mpaka ngazi za chini.
Mfano sudhani kuwa kuna Waraka unaohusu msimamo wa chadema juu ya kupigwa marufuku vyombo vya habari huru na vya umma kutangaza live bunge n.k , n.k.

Hali hii inapelekea Chama kuwa ni cha kiharakati na kimatukio. Tukio liputa basi agenda inaishia hapo bila kumbukumbu yoyote ya kimaandishi.Na wanaopata fursa ya ya kupata taarifa mara nyingine sio wanachama kwani hakuna vikao vya ndani vya kupeana taarifa.
Kwenye maandano hua hakuna mijadala ya kina zaidi ya mihemko inayoishia kutukana na kukashfu viongozi wa serikali amba kwa awamu hii ni marfuku hata kuwataja kama sio kwa maana ya kuwasifia.

Lowasa kwa uzoefu wake wa siasa akaligundua hilo. Aligundua kuwa awamu hii hakuna chama kitakachoruhusiwa kumtaja mwizi au fisadi kama kiki ya kujipatia umaarufu kikapona.
Awamu hii ukihoji tu kuwa nyumba na mashirika ya umma kwa nini yaliuzwa kinyemela na kwa bei chee basi ujue utaitwa mchochezi na utaishia kukamatwa .
Ukihoji suala la wizi unaitwa mchochezi.

Kwa hiyo kwa sasa haiwezekani kutegemea kufanya harakati za kimaandamano ili kupata umaarufu wa chama au mtu.
Ndio maana mpaka sasa kuna watu na wabunge ndani ya chadema wameanza kupoteza umaarufu kwa sababu tu walitegemea agenda moja tu ya kusimama na kumtuhumu mtu kwenye majukwaa. Ni rahisi kusimama na kusema kuwa mtu anauza madawa ya kulevia China au Itali bila kueleza ni vipi watu wengi watanufaika au kutonufaika na wachina walioamua kununua madawa na kumfanya mtanzania huyo kuwa bilionea.

Ni lazima chama kiwe na agenda za kudumu za kushika dola. Mfano kama agenda ni mafisadi itakuaje sasa wakati Magufuli anaonekana na wananchi wameshaamini kuwa anayatumbua. Je, sasa upinzani utatoweka kwa sababu ya kutumbuliwa kwa majipu tu wakati mipango ya kukuza uchumi bado haijawa na uelekeo huku maisha yakiwa magumu.

Chadema kiweke sasa mikakati kama serikali iliyokuwa madarakani ikawekwa pembeni na inajiandaa tena kurudi. Hii ni kutokana na kuwa na wanachama ambao walikua madarakani na wenye uzoefu mkubwa wa kusimamia dola bila kuyumbisha umoja wa taifa. Jambo ambalo kwa sasa CCM wanapwaya sana kutokana na kuendesha siasa za hasira na chuki dhidi ya wananchi wasiowaunga mkono.
 
Walioanzisha, kuhamasisha, kutoa matamko kuwa Lowasa ni fisadi ni Chadema. Wewe Yericko ukiwa moja ya wapiga propaganda za mitandaoni kauli zako zimewekwa hata ktk uzi huu. Njoo hapa uombe radhi umma kwa matamshi yasiyo na ushahidi. Hizi twist za kijinga fanyieni watanzania wa zama zile lakini sasa watabaki na kumbukumbu. Weka akiba ya maneno maana ndio kwanza kumekucha ....
Hawa jamaa ni wapuuzi sana.
Ndo waliosababishwa watu wakaitwa "malofa".
Haiingii akilini ukamchukua mtu unayemwita fisadi namba moja afu ndo akawe "rais" wako.
Na sasa matamko ya Lowassa yana nguvu kuliko kiongozi yeyote wa Chadema.
 
CHADEMA watu wenye akili zao waliisha jitoa na wapo kimywa!
Wamebaki hawa wahuni tu
 
Hahahaa mkuu, unapiga kichwani kabisa?
Mkuu hiyo ndiyo njia pekee iliyo bakia maana hawa jamaa hawataki kubebeka,ktk kipindi kigumu kama hiki badala ya kushiikiana wapinzani wote wao kila kukicha ni kuiandama cdm tu
 
Jiwe walilolikataa waashi...leo lowasa waliyemchafua ndio mwenye ushawishi wa kutoa dira ya chama,mtu sio mwenyekiti wala mjumbe wa kamati kuu lakini anawaambia waache harakati. Swali moja tu kwa wanafiki "lowasa alikuwa mwizi au sio mwizi!?" yericko atujibu hili bila siasa na kumung'unya maneno.
 
Swali la kwamba Lowasa ni Mwizi au sio mwizi wakuulizwa ni wenye vyombo vya uchunguzi,mahakama na intelijensia.

Wapinzani walipokea toka kwa CCM wenyewe waliokua wanaendesha siasa za kikabila,kikanda na kidini.
Hayo ndiyo waliyotumia kumpiga vita Lowasa. Walianza tangu enzi za chama kimoja ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika.. Hata ndani ya CCM hiyo vita ya kupakana matope ipo na ndiyo inayotumika kuwagawa kimakundi.
Leo hii kuna CCM wanaotaka kupata fursa ya kula mema ya nchi kupitia madaraka wameshaanza kudai wenzao wafukuzwe kwenye chama kisa wanaona kuwa Mkulu hatoshi kwenye uenyekiti mana hajawahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kwenye chama.

Ukumbuke kuwa hata ndani ya CCM kilichosababisha Lowasa akatwe sio ufisadi mana huko hakuna msafi hata wa kuangalia kwa darubini. Kilichomtoa Lowasa ni Afya yake kwani wakati ule ilidorora sana.
Na kwa mziki wa wapinzani wake waliikua wanatumia kila mbinu kumdhibiti ili asije akaingia ikulu akawaadhibu bila huruma na woga wao wa kulipizwa visasi. Hapakuwa na jinsi zaidi ya kumkata.

Hata hivyo Wananchi ndio wanaoona usafi wa Lowasa na sio adui zake kisiasa.
Nisingetegemea mtu maarufu kama Lowasa kusifiwa na wapinzani wake kisiasa.
Na pia nisingetegemea wapinzani kuendelea kumpinga mtu ambaye ameamua kukipinga chama wanachotaka kukitoa madarakani.
Ni sawa kama leo hii kwa Magufuli , sisi wananchi ndio tunamuona anajitahidi lakini wanasiasa hawajamkubali.
Ni kawaida kwenye siasa. Na ndio maana wanamwambia Magufuli ahame Chama.

Tofauti ya Lowasa na wanasiasa wengine ni kuwa hatumii siasa za kutukana watu.
Kura alizopata ni ushahidi tosha kuwa wananchi ndio waliokua wanamuhitaji na sio wanasiasa. Mbowe aliliona hilo. Kwa katiba yetu na tume inayosimamiwa na makada wa CCM kuanzia kwenye vijiji,wilaya ,mikoa na vyombo vya dola Lowasa kubakiziwa kura mil. 6 ni ushindi kwa UKAWA.
 
Back
Top Bottom