Lowassa kakosea? Hapana, tujikumbushe ushauri huu

Swali la kwamba Lowasa ni Mwizi au sio mwizi wakuulizwa ni wenye vyombo vya uchunguzi,mahakama na intelijensia.

Wapinzani walipokea toka kwa CCM wenyewe waliokua wanaendesha siasa za kikabila,kikanda na kidini.
Hayo ndiyo waliyotumia kumpiga vita Lowasa. Walianza tangu enzi za chama kimoja ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika.. Hata ndani ya CCM hiyo vita ya kupakana matope ipo na ndiyo inayotumika kuwagawa kimakundi.
Leo hii kuna CCM wanaotaka kupata fursa ya kula mema ya nchi kupitia madaraka wameshaanza kudai wenzao wafukuzwe kwenye chama kisa wanaona kuwa Mkulu hatoshi kwenye uenyekiti mana hajawahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kwenye chama.

Ukumbuke kuwa hata ndani ya CCM kilichosababisha Lowasa akatwe sio ufisadi mana huko hakuna msafi hata wa kuangalia kwa darubini. Kilichomtoa Lowasa ni Afya yake kwani wakati ule ilidorora sana.
Na kwa mziki wa wapinzani wake waliikua wanatumia kila mbinu kumdhibiti ili asije akaingia ikulu akawaadhibu bila huruma na woga wao wa kulipizwa visasi. Hapakuwa na jinsi zaidi ya kumkata.

Hata hivyo Wananchi ndio wanaoona usafi wa Lowasa na sio adui zake kisiasa.
Nisingetegemea mtu maarufu kama Lowasa kusifiwa na wapinzani wake kisiasa.
Na pia nisingetegemea wapinzani kuendelea kumpinga mtu ambaye ameamua kukipinga chama wanachotaka kukitoa madarakani.
Ni sawa kama leo hii kwa Magufuli , sisi wananchi ndio tunamuona anajitahidi lakini wanasiasa hawajamkubali.
Ni kawaida kwenye siasa. Na ndio maana wanamwambia Magufuli ahame Chama.

Tofauti ya Lowasa na wanasiasa wengine ni kuwa hatumii siasa za kutukana watu.
Kura alizopata ni ushahidi tosha kuwa wananchi ndio waliokua wanamuhitaji na sio wanasiasa. Mbowe aliliona hilo. Kwa katiba yetu na tume inayosimamiwa na makada wa CCM kuanzia kwenye vijiji,wilaya ,mikoa na vyombo vya dola Lowasa kubakiziwa kura mil. 6 ni ushindi kwa UKAWA.
Asante sana mkuu kwakuwapa somo hawa ndugu zetu
 
Unaweza ukawa mkubwa lkn kubwa jinga,sio kila mtu ana akili zakushikiwa kama uzaniavyo,watu vigeu geu kama huyu ingepita sheria ya kutandika risasi tu,sababu wapo radhi kumzalilisha mtu kwa vijisent vya kujikomba komba,,ila nw nimeamini umri unapozidi kusonga,ndio akili yako inarud kama mtoto,ikizid zaid unafikia hatua ya kujisaidia kama mtoto,
 
Yericko kama uliyajua haya kwa nini ulikuwa unamsingizia Lowasa kuwa ni fisadi??

Hivi unajua kuwa shombo zako ndio zilipelekea lowasa kukatwa na ccm??

Unajua kuwa bila shombo zako Lowasa Leo angekuwa rais wa Tanzania.??

Ni lini sasa utaenda kutubu na kumuomba Mzee Lowasa msamaha kwa matusi uliyomtukana na kumzomea kuwa ni fisadi ,huku ukijua si fisadi??

Hizi siasa za kusingizia watu ufisadi kwa manufaa ya tumbo lako ,ni bora ukaachana nazo kabisa.
Hamna dola inayokamatwa kwa kujiegesha kwenye misingi ya siasa za kinafiki.
Akatwe tu!
 
Unaweza ukawa mkubwa lkn kubwa jinga,sio kila mtu ana akili zakushikiwa kama uzaniavyo,watu vigeu geu kama huyu ingepita sheria ya kutandika risasi tu,sababu wapo radhi kumzalilisha mtu kwa vijisent vya kujikomba komba,,ila nw nimeamini umri unapozidi kusonga,ndio akili yako inarud kama mtoto,ikizid zaid unafikia hatua ya kujisaidia kama mtoto,
Mada umeielewa?
 
Makala hii ni marudio, niliiandika mwaka 2015 baada ya Mh Edward Lowassa kujiunga na Chadema. Lengo la kuirudia makala hii ni kujibu mjadala unaoendelea hivi sasa kuwa Mh Lowassa alikosea aliposhauri kuwa Chadema sasa ijikiti kwenye lengo la kisiasa la kushika dola badala ya kuendelea na harakati zaidi..

....................
Huwezi kuwa Mwanasiasa bila kwanza kuwa mwanaharaka, lakini unaweza kuwa mwanaharakati bila kuwa mwanasiasa, Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni NJIA azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya
njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa
lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni
mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani.

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa ya chama chake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo
huo huhanikizwa katika siasa. Uzalendo makazi yake ni kwa mwanaharakati na sio kwa mwanasiasa, lakini uzalendo huo hulindwa vema chini ya mwanasiasa madhubuti.

Mwanaharakati hunyooka kama kamba katika misimamo yake, na mwanasiasa hutembea katka fursa za kisiasa. Chama cha siasa lengo ni kushika dola kwanza, kisha kuwatumikia watu wake kwamisingi ya itikadi na ilani yake, na harakati na mwanaharakati lengo lake ni usawa wa maisha kati jamii na haki za kiraia zaidi tu.

Ni Mtanzania mjinga tu na asiyelitakia mema taifa hili ndie atakayepinga Lowasa asiende Upinzani. Tunataka kulikomboa taifa toka mikononi mwa ccm, kila nyenzo iliyombele yetu tutaitumia na kila mwenye uthubutu tutakuwa nae,

Ccm itoke kwanza na mengine yatafuata, Kama Lowasa amekubali itikadi ya Chadema nani mwenye kuzuia ujio wake? Vyama vya siasa ni sawa na masinagogi, mtu akitubu na kujutia madhambi yake huyu pepo ni yake!

Karibu Lowasa, Karibu mawaziri wote, karibu makada wote, karibu nawe Jk kwakuwa kazi tuliyokutuma kuiua ccm umeikamilisha.

Nchi hii ni ya watz wote, na Upinzani ni wawote sio mali ya mtu ama kikundi. Siasa ni sanaa ya ajabu sana, haina rafiki wa kudumu, wala haina adui wakudumu. Kwa miaka zaidi ya tisa nyimbo hiyo hiyo mara Lowasa fisadi, mara oooh mwizi, wanaohubiri hayo ni viongozi wa ccm,
Wamesahau mifumo ya utendaji kati ya serikali na dola ilivyo badala yake wanafanya siasa.

Ukiuangalia na kuuchambua mfumo wa utendaji wa vyombo vyq ulinzi na usalama vinavyotumia muundo wa westan Secur utaona kuwa Lowasa ni mtu safi KABISA, ila siasa ndizo zimemdhihaki na kumdhariri kabisa.

Nataka kuzungumza dhana ngumu kidogo machoni pawengi, lakini hima nitaeleweka bila mawaa wala chembe ya makunyanzi. Nazungumza kama mtaalamu wa mifumo ya kiulinzi duniani hasa kile ninachokifahamu, nikiangaza mifumo ya kiusalama ya Franks Secur, Westm secur, Latino secur, Kremlin secur.

Siasa tuiache kando utaalam uchukue nafasi yake, na hapa nataka tujikite kuuangalia mfumo na muundo wa utendaji wa Westan secur na vyombo saidizi vyake katika kulitumikia taifa chini ya Westan secur

Nchi zote ama karibu zote Usalama wa Taifa ni idara au shirika lililochini ya Ofisi ya Rais kwa zile zinazoendeshwa kwa mfumo wa Madola, na zile za kifalme huwa chini ya Waziri Mkuu, hii inamaana kuwa mkuu wa idara hiyo anaripoti kwa rais au kwa Waziri mkuu mojakwamoja, pia mkuu wa idara hii huteuliwa na rais, Waziri mkuu au Bunge kwakuzingatia vetting maalumu iliyochini ya command ya ndani.

Miuundo ya utendaji wa idara au shirika hilo umegawanyika katika sehemu kuu sita, tano, au tatu kulingana na mahitaji ya wakati huo, ambazo kimsingi ni idara ndogondogo ndani ya idara hiyo au shirika hilo kubwa. Mfano ni idara ya mambo ya ndani, idara ya siasa, idara ya mambo ya nje, idara ya uchumi, idara ya ukusanyaji taarifa, idara ya uchakataji taarifa na idara ya vita na teknolojia.

Hapa nataka kuzungumzia idara ya siasa ambayo ndio tunayokumbana nayo mtaani kila kukicha na tunashirikiana katika maandamano nk,

Kwamfano nchini Urusi ambako nchi nyingi zinaiga ikiwemo Tanzania, Idara hii nayo ina vitengo mhimu vya kiutendaji ikiwemo ulinzi wa chama na serokali, sera za kisiasa na muundo wa siasa kutegemeana na chama kilichopo madarakani wakati huo.

Pia idara hii inajukumu la kufuatilia na kutambua mienendo ya wanasiasa viongozi na wale wote watu maarufu katika taifa, bila kusahsu kufuatilia mawasiliano yao, baruapepe zao, mizunguko yao ya kila siku, vyakula vyao vya kila siku, vipato vyao nk.

Idara hii pia imepewa jukumu la kuwalinda viongozi wa kisiasa (mawaziri na wabunge) kwa saa 24 bila kukoma. Mfano, Rais hulindwa na watu 40 wanaoonekana na 48 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka.

Makamu wa Rais hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 10 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka

Waziri mkuu hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 8 wasionekana hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2) zingatia kukiwa na hali ya hatari kiwango cha ulinzi huongezeka.

Mawaziri hulindwa na watu 3 wanaoonekana, na 5 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def s2).

Majukumu ya walinzi wanaooneka na wasioonekana yanatofautiana na kila mtu kati yao huripoti kwa boss wake,
Wale walinzi wanaoonekana huripoti kwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, na wale wasioonekana huripoti kwa rais kila mmoja kwa wakati wake bila wao kujuana.

Hii inamaana kuwa kila anachotaka kufanya ama anachofanya waziri yoyote kabla hajakitenda basi taarifa huwa mikononi mwa rais na mkurugenzi wa Usalama nchini.

Wale wanaoonekana wanaomlinda Rais huripoti kwa mkurugenzi na mnadhimu, wale wasioonekana 10 huripoti kwa rais moja kwa moja, na 30 huripoti pande zote tatu lakini kwa umakini mkubwa bila kujuana.

Sio nia yangu kusafisha wanasiasa, bali nia yangu nikukuelezeni kitaalamu mfumu wa ulinzi nchini unavyoendeshwa na madhari ya kisiasa kuwa waziri fulani ni mwizi ama fisadi kwa dhana ileile ya kisiasa.

Kwenye medani ya siasa huko kuna filosofia tofauti kidogo ambayo hutafsiri uwajibikaji kisiasa katika dhana inayokinzana na uhalisia wa kiutaalam katika mifumo ya kiulinzi.

Hapo sijazungumzia intelligence ya jeshi la Polisi ambayo nayo ni mdau, na kwa nchi kama Israel hiyo ina nguvu sana, pia sijaigusa Tanzanian Military Intelligence ambayo kwa nchi kama Urusi ndio mwamuzi wa mwisho katika muktadha wa taifa hilo.

Hii ndio ya tofauti ya siasa, harakati,na taaluma. Chadema na UKAWA wamevuka ngazi ya uanaharakati na kuwa vyama rasmi vya KISIASA,
Harakati zipo kwa akina Kibamba, Kijo Bisimba, Maria Sarungi, Mr Sungusia nk...

Sisi wengine ni wanasiasa, na lengo kuu la siasa ni kushika dola ndipo tutatekeleza yale tuyanenayo juu ya umma. Silaha yoyote iliyo mbele yetu tutaitumia ilimradi inaiondoa ccm na mfumo wake unaolitafuna taifa hili.
Hivi Yericko huwaga una hallucinate ama ni ukogo serious na hizi mambo unaandikaga andikaga...???

Two Things!!!

Either unaangalia sana muvi na series za propaganda zakimarekani ama you hav a serious mental issue ambayo inakufanya una teleport invariably.. (Mind you the mental issue is not necessarily a problem of which endapo itakua is a problem ni afadhali sana kwako maana itakusaidia ukapate tiba)..

Nikiwa bored huwa najiburudisha kwa kupitia pitia machapisho yako mtandaoni na kuyasoma kama riwaya za Willy Gamba.. nothing more nothing less..
 
Asante sana mkuu kwakuwapa somo hawa ndugu zetu

Me hili Somo lako nililielewa saana!!

Yericko Nyerere
May 30, 2015 ·
Hivi mnawezaje kukaa na kufuatilia maigizo na kuamini asemacho? Lowasa alisoma BA Fine and Performing Arts, ni mwanamazingaombwe msomi.

Viongozi wa dini aina ya Gwajima ni mabakuli ya wanasiasa, pesa yako tu utaamua aseme nini. Wiki iliyopita alikuwa alisema ameotesha na Mungu wake kuwa Slaa ndie Rais mpya ajae, Leo tena amesema ameonyeshwa na Mungu wake kuwa Lowasa ndie Joshua wa kwenye biblia aliyewavusha Israel. Hivyo atawavusha wa Tanzania ikiwa atakuwa Rais.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom