- Lowassa ni beneficiary wa kelele za wananchi zinazoendelea sasa hivi juu ya mapungufu ya Rais wa sasa, huyu ndiye hasa beneficiary wa lile Kongamano la Foundation majuzi na sitashangaa kama hakukuwa na mkono wake kule!
- Sasa politically, huu ndio wakati wake wa kuanza kujitokeza as the alternative, lakini kwa ujanja sana kama huu wa huko Ummasaini, ninatabiri one thing kwamba in the end Muungwana atakata deal, ambalo litamrudisha Lowassa kwenye cabinet level with condition ya kuachiwa urais 2015!
- I mean lets face it ni huyu Lowassa peke yake sasa hivi ndiye mwenye uwezo wa kuivunja CCM vipande viwili na hilo linamuogopesha sana Rais wa sasa kwa sababu anajua kuwa linawezekana na Lowassa analiweza, tena sana kwa sababu 2/3 ya uongozi wa CCM sasa hivi unam-support Lowassa, na wala sio siri ukifanyika uchaguzi wa haraka leo kati ya Muungwana na Lowassa nani awe Rais, Lowassa anamshinda tena hands down! Ninasema tena kwamba ukifanyika uchaguzi wa dharura leo Muungwana hawezi simama na Lowassa! and yes I said it!
- Ili kuendelea na Urais 2010, Muungwana anahitaji sana support ya Lowassa, tena bila hata ya wapiganaji, ndio maana kwenye uchaguzi wa UWT Muungwana ali-side na Lowassa kumfagilia Sophia Simba, pamoja na kwamba huko nyuma na mapema alishasema kwamba wagombea wote hawafai kwa sababu hawana afya nzuri! Kwenye ile NEC sio siri kwa wale wote waliokuwepo kwenye kile kikao kwamba Muungwana, alikuwa side ya Lowassa, against Sitta ni baada ya mabalozi wa nje hasa wafadhili kuingilia kati ndio akajifanya hayuko huko upande wa pili, lakini hakujua kwamba pamoja na kujaribu kujisafisha na ule mkutano wake wa kujibu simu, it was too late!
- Muungwana na Membe, peke yao hawawezi kuzima sauti za kina Butiku na Quaresi ni lazima nguvu ya Lowassa isaidie, ndio maana sasa unaona maajabu mengi yanatokea katika kuwajibu na kujaribu kunyamazisha sauti mbadala! No wonder Lowassa is so confident wala hayumbi au kubabaika, anapanga operation moja baada ya nyingine na zinafanikiwa, I mean look what happened to Nape, where was Muungwana to rescue him kama kweli anakijali chama kuliko kujikomba kwa Lowassa and the gang?
- Wa-Tanzania tufike mahali sasa tutafakari hali ya siasa ya taifa letu kwa kina na umakini, na it is simply a fact kwamba anayeweza kutukomboa sasa hivi ni Lowassa peke yake, sasa either tusuke au tunyoe maana hapa tuna-face mikuki miwili tena ya moto, upi ni afadhali? Ninasema hivi kWa sababu sio siri kwamba Lowassa is not going anywhere soon na hakuna wa kumuondoa! Na mimi ninashangazwa sana na confident aliyonayo yeye na wapambe wake, huwa ninajiuliza wanajua nini hasa kuhusu taifa letu I mean wana ujeuri flani ambao sio wa kawaida kwa sisi tunaowajua na kuongea nao kwa karibu,
- Wanajiamini nini hasa? I mean ni mawazo yangu tu madogo thinking aloud! Na I could be wrong pia!
Respect.
FMEs!