Lowassa: Hatutakubali Matokeo ikiwa...



Naona kama anajiandaa kisaikolojia kuyakataa matokeo - inaonekana ameshajua atashindwa. Basi atuambie kwanza ni vitu gani vitakavyoonyesha kuwa uchaguzi ni huru na wa haki?? Aviseme sasa hivi - sio baada ya tarehe 25 - Octoba.
 

Ni kweli Chadema hatutakuwa tiyari kupokonywa ushindi wetu.

Ni lazima Tufike mahali tuamue juu ya vizazi vyetu vijavyo sio kila siku tukubali matokeo kirahisi.

Mwaka huu hakuna hio.
 

Daaaah!nimecheka sana mkuu!
 
mh, hawa fisiemu ni kwamba wanajipanga kuhakikisha goli la mkono linatumika pasipo watu kugundua, na ukijifanya umegundua wanakupoteza
 
UKAWA ni chama cha upinzani...wasipoyakubali matokeo ya CCM kushinda kwa goli la mkono lazima zipigwe...zinapigwa na nani hayo ni majaliwa. Magufuli kwa sasa anajitahidi kukusanya kura vijijini ili goli liwe la mguu na UKAWA wasipotafuta kura za vijijini basi watapigwa goli la haki wala hawataweza kukataa matokeo. Kuzunguka makao makuu ya mikoa wasidhani hali iko kama vile vijijini waende wakaone hali ikoje na kama umma unawakubali lakini pia warudi wachukue wagombea wanaokubalika na wananchi wala wasijidanganye kupata kura kama watalazimisha wagombea dhaifu wa udiwani na ubunge eti kwa vile wako Chadema au CUF kwa makubaliano yaliyowekwa kabla; angalieni sasa na siyo wakati TWAWEZA ikikusanya kura mlizozikataa.
 
Kashanusa harufu ya kushindwa kama kipindi kile cha hakatwi mtu hapa. alinusa harufu kua anakatwa akaanza kuleta maigizo mbali mbali mara wenyeviti wa mikoa 13 wakapiga mkwara pale Dodoma wakiitaka kamati kuu isilikate jina la Lowasa na kipindi kile habari iliyoanza kuvuma kwenye vyombo vya habari ilikua ni kuhusu kukatwa au kutokatwa kwa jina lake. Na sasa muanze kujiandaa kisaikolojia Magufuli anakwenda kushinda kw kishindo na mtabaki midomo wazi
 

Vurugu hazina macho.
Uzuri vi asset vyake vyote tunavijua labda aanze kuhamishia ughaibuni familia yake
 
Mazingia ya uchaguzi ni huru na haki kwa sababu anaruhusiwa hata kujinyea kwenye suruali.
 
Hahaha haaaahaa ameona dalili mbaya ya kushindwa vibaya uchaguzi huu
 
Lowassa Mwenyewe ni Jeneza Linalotembea, sasa atamtwanga nani au anataka kuwashakizia vijana wa kimachinga?

Kati ya hawa wawili ni nani jeneza linalotembea!!?
 

Attachments

  • 1443164262646.jpg
    25.2 KB · Views: 116

Mzee shamba lako la mihogo limejaa nyasi lini utakuja kulima? bora urudi tu huko uhamishoni kumekushinda naona unatafuta fadhila za CCM.
 

Ndo ameungana nao sasa...
Kwani wewe mpinzani..??
Na je, utapiga kura...??
 
mh, hawa fisiemu ni kwamba wanajipanga kuhakikisha goli la mkono linatumika pasipo watu kugundua, na ukijifanya umegundua wanakupoteza

Kitu wasichojua ni kuwa ukiiba kura humuibii Lowasa bali unawaibia wale waliochagua Lowasa ambao kwa vyovyote ni mamilioni ya watu. Na mbaya zaidi na la kuogopa ni kuwa wengi wa hao mamilioni ni wale walio kata tamaa na maisha na wanaona hawana la kupoteza zaidi ya kupata iwapo fujo zitatokea. Ndivyo ilivyotokea kwa nchi nyingi.
Wanaonufaika na CCM ikiiba kura ni wale ambao wengi wako ndani ya mfumo na maisha ya purukushani hawayawezi hata kidogo, tusidanganyane kuwa watawala na familia zao wataishi kwa raha tena nchi ikichafuka. Haya maneno ya kejeli na dhihaka mnayasema tuu kwa vile hamjatembea na kujionea nchi ambazo utaratibu huo wa kuiba kura umezifikisha. Please ni wajibu wetu sote kuhakikisha kuwa uchaguzi unakwenda kwa uhuru na haki na mshindi anatangazwa aliyeshinda, hawa watawala wasitusababishie hali ya sintofahamu hata kidogo maana wao walishajiwekea mapesa nje na wanaweza kuishi huko maana hata watoto wao wako huko wanasoma na kuishi tayari.
Kwanza ya nini ugomvi? Mbona ndani ya familia zetu waweza kukuta Baba ni Ukawa na mama ni CCM? Na uchaguzi ukiisha ndoa zinaendelea? Hawa wakina Bulembo na Mwigulu wasituletee zao za kuleta maana kama uchaguzi wa haki haupo kulikuwa na sababu gani ya kuuitisha si bora hayo mabilioni yangeenda kulipa deni la MSD ili tupate dawa hospitalini, madawati kwa watoto wetu na vitanda hospitalini kwa wajawazito kuliko kujifungua kama makundi ya nguruwe zizini?
 
Asituletee ujinga wake akapigane na mafisadi wenzake siyo kutuletea huu ujinga kwenye taifa letu.

Kama Dr. Magufuli ana ajenda ya Rasimu ya pili ya Katiba ya wananchi ategemee kura yangu, vinginevyo kama ndio ahadi hizi kama za kikwete ambazo hazima mfumo madhubuti wa kuzitekeleza na kuzisimamia siwezi kumuentrust kura yangu, najua ni uongo na ubabaishaji kama wa mtangulizi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…