Lowassa: Hatutakubali Matokeo ikiwa...

Lowassa: Hatutakubali Matokeo ikiwa...

Kitu wasichojua ni kuwa ukiiba kura humuibii Lowasa bali unawaibia wale waliochagua Lowasa ambao kwa vyovyote ni mamilioni ya watu. Na mbaya zaidi na la kuogopa ni kuwa wengi wa hao mamilioni ni wale walio kata tamaa na maisha na wanaona hawana la kupoteza zaidi ya kupata iwapo fujo zitatokea. Ndivyo ilivyotokea kwa nchi nyingi.
Wanaonufaika na CCM ikiiba kura ni wale ambao wengi wako ndani ya mfumo na maisha ya purukushani hawayawezi hata kidogo, tusidanganyane kuwa watawala na familia zao wataishi kwa raha tena nchi ikichafuka. Haya maneno ya kejeli na dhihaka mnayasema tuu kwa vile hamjatembea na kujionea nchi ambazo utaratibu huo wa kuiba kura umezifikisha. Please ni wajibu wetu sote kuhakikisha kuwa uchaguzi unakwenda kwa uhuru na haki na mshindi anatangazwa aliyeshinda, hawa watawala wasitusababishie hali ya sintofahamu hata kidogo maana wao walishajiwekea mapesa nje na wanaweza kuishi huko maana hata watoto wao wako huko wanasoma na kuishi tayari.
Kwanza ya nini ugomvi? Mbona ndani ya familia zetu waweza kukuta Baba ni Ukawa na mama ni CCM? Na uchaguzi ukiisha ndoa zinaendelea? Hawa wakina Bulembo na Mwigulu wasituletee zao za kuleta maana kama uchaguzi wa haki haupo kulikuwa na sababu gani ya kuuitisha si bora hayo mabilioni yangeenda kulipa deni la MSD ili tupate dawa hospitalini, madawati kwa watoto wetu na vitanda hospitalini kwa wajawazito kuliko kujifungua kama makundi ya nguruwe zizini?

Tatizo kubwa hamlijui lakini naamini mnalijua, haiwezekani kama akili yako inafanya kazi vizuri alafu unaongea mambo ya kipuuzi namna hii, huu co muda wa kulalamika tena, ni muda wa kujikosoa, tatizo linafahamika vema kuwa tume si huru, ss unachotaka ni nn kama si ujinga huo, mm nilitegemea sana kwamba UKAWA tuna viongozi makini, kumbe ni tabu tuu, tatizo la nchi hii si Urais, lakini kwa ujinga wetu tumewekeza sana kwenye Urais, na huu Urais hauna msaada kwetu cc watu wa chini, unaposema unataabika sana na hali ngumu ya maisha, dawa yake ni serikali za mitaa/kijiji, udiwani na ubunge, cc hatuna shida na urais, kama wabunge hawatoshi kufanya maamuzi bungeni wakati huo Rais ni Lowasa hayo mabadiliko utayapata vipi? sheria zote mbovu zinaondoka tu endapo una wabunge wa kutosha bungeni, ni ujinga sana kuongelea Urais kuliko ubunge, unapowalaumu akina Mwigulu, kimsingi ww ndo unaonekana kichwa chako kina matatizo, na huo ndo umekuwa ugonjwa mkubwa wawapinzani kulalamika, tunayo nafasi kubwa ya kufanya haya mageuzi kwa kupitia wabunge tutakao wachagua, na kwa bahati nzuri ubunge unahojiwa mahakamani, ww unataka kitu ambacho hakihojiwi mahakamani, huo ndo tunauita umburula, haya Mwl.Nyerere aliwahi kuyasemea kwa kuwashauri wapinzani kwamba, watafute nafasi za kuwawakilisha wananchi wao bungeni hakuwa mjinga kusema hivyo- sasa UKAWA akili zao zimeishia kwenye Urais, viongozi wanaongea mpaka mishipa ya kichwa inataka kuchomoka eti Urais, hiyo nguvu ingetumika kwenye nafasi za uwakilishi tungekuwa tumepiga hatua kufikia kuomba Urais na wananchi wangekuwa wamepata hamasa ya kutosha.

Kwa upande wangu ninaye penda mabadiliko, nasikitika sana kuona viongozi tulionao ni wa namna gani, UKAWA hawawezi kushinda, na kwa bahati mbaya tumeweka kiongozi ambaye na yy anaipenda hiyo tume kama akifanikiwa kuingia ikulu, angekuwa anaichukia asinge poteza muda wake kugombea Urais.
 
This is silly!.. alisema ni lini Uchaguzi haujawahi kuwa Huru na wa haki? Mbona hatujawahi kumsikia akiungana na wapinzani walipopiga kelele ya kukosekana uhuru na haki kwenye chaguzi mbalimbali; au anafikiri tumesahau yaliyotaka kutokea Arumeru Mashariki?

msalimie josefin na dr.mihogo
 
Vurugu hazina macho.
Uzuri vi asset vyake vyote tunavijua labda aanze kuhamishia ughaibuni familia yake

Awambie wanae ndo wakapigane lakini co sisi walala hoi, mtu mwenyewe amejichokea ss anataka watoto wa wenzie ndo wauwawe? ujanja wa ccm alikuwa anaujua na bahati nzuri yy ndo alikuwa kinara wa ujinga huo, wakati wanafanyiwa wapinzani alikuwa anasikia raha sana wakati huo, na ninaamini hakutegemea kuwa suku moja na yy angejikuta anasema "people" wembe ni uleule na yy utamnyoa, baada ya kinyolewa sasa atatwambia ukweli, make hadi muda huu hajesema kitu, ni sawa na mtu anaye jidai mjanja sana kuwa anaficha siri, ukimpa pombe zikamkolea utamsikia anafungua domo lake na kuelezea siri zake zote, kwa hali hiyo mzee bado hajasema. tunamwitaji aseme na tunataka safari hii tuongeze wabunge angalau hata tufikishe 100 kwa kupitia yy, alafu akapumzike Mondili, make Dr. Slaa na yy alituongezea wabunge kwa wakati huo, ss ni zamu ya Mzee Lowasa, ninaimani uchaguzi ujao kuongezea wabunge33 ili tuunde serikali, itawezekana tena kwa kishindo!
 
This is silly!.. alisema ni lini Uchaguzi haujawahi kuwa Huru na wa haki? Mbona hatujawahi kumsikia akiungana na wapinzani walipopiga kelele ya kukosekana uhuru na haki kwenye chaguzi mbalimbali; au anafikiri tumesahau yaliyotaka kutokea Arumeru Mashariki?

Lowassa kutokusema uchaguzi hauko huru haimaanishi ulikua huru. Kama suala ni kusema tu, kwanini mnamsema kwamba ni fisadi wakati alikua hukohuko? Watu huamua kunyamaza tu kwa sababu hawataki shari na kuvumilia mambo yaende.
 
Kwani lini wapinzani walishawahi kukubali matokeo? Mjiandae mapema kisaikolojia.. Na mkikaidi mtapigwa tu na mm nasema mmpigwe tu maana hamna namna sasa.

Endelea kuishi kwa kukariri.endelea kuishi kwa mazoea
 
Baada ya October 25 tutajua mbivu na mbichi kama MUNGU akitufikisha hiyo siku.so hakuna haja ya kuandikia mate,kwa upande wangu mshindi ni mshindi,sina muda wa kuandamana kupinga sababu hainisaidii zaidi inaweza nipa shida.
 
Lowassa Mwenyewe ni Jeneza Linalotembea, sasa atamtwanga nani au anataka kuwashakizia vijana wa kimachinga?
Invisible Maxence Melo
Kuruhusu ujinga kama huu umeua JF. No wonder watu wenye hekima siku hizi tumebaki wasomaji tu!
Kuna haja ya kurudisha heshima ya JF kabla mbadala hajapatikana.
Ni maoni yangu tu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom