Baada ya kupata maoni kuwa RICHMOND ina matatizo Edward Ngoyai Lowasa aliitisha kikao cha makatibu kwa ajili ya kujadili suala hilo na alishauri kama wanaafiki kuwa magumashi wavunje mkataba, Lakini amri ilitoka kutoka mamlaka ya juu kuagiza mchakato uendelee. Na ukaendelea.
Taarifa ya Dr. Harrison Mwakyembe pamoja na mambo mengine ilipendekeza kufutwa mikataba yote inayonyonya TANESCO na mlipa kodi lakini azimio hilo halikutekelezwa na matokeo yake ndio ESCROW ACCOUNT TEGETA.
Akiwasilisha ripoti kwa mbwembwe Dr. Harrison Mwakyembe alieleza kwamba wangeendelea kuchimbua zaidi kutokana na taarifa walizopata serikali ya JK ingeanguka kwa sababu muhusika mkuu ni IKULU.
Kudhiirisha anguko la mtu dhalimu halionekani machoni pake, kwa kuwa mboni za macho zake zimevikwa vazi la kiburi, sasa tunakuja kukutana na ESCROW ACCOUNT TEGETA. Mungu alitaka kuwaumbua kweupe madhalimu, kuwaumbua kweupe wadhulumaji.
Maazimio yote ya bunge kuhusu ESCROW ACCOUNT TEGETA mkulu JK aliyaongea kwa tabasamu na kuchekacheka tu akikwepa maazimio mahsusi kwa mara ya pili kufuta mikataba, kutaifisha mitambo kwa madai yasiyo na mashiko kama ya Prof.Lipumba alivyojizulu uongozi CUF.
Dr.Magufuli amewaahidi wana CCM wenzake hato waangusha, ina maana mikataba ya kinyonyaji sekta ya umeme itaendelea na watanzania tutaendelea kununua umeme kwa gharama kubwa. Mwaka 2008 kiasi cha tsh.10,000 nilipata UNIT 72 leo hii natumia tsh.30,000 kupata unit 64
Kuna unafuu tangu LOWASA aondolewe Uwaziri Mkuu? Huyo Mwakyembe aliyeandika kitabu akieleza serikali ya shirikisho ndio muafaka na kupitia hicho alifanikiwa kupata udaktari alibinua mdomo kuwaeleza wenzake katika bunge la katiba?
Samwel Sitta aliyesimamia vizuri bunge akiwa spika awamu ya kwanza JK, akijipambanua kusimamia haki, usawa na kutokomeza ufisadi. Si ndio huyo huyo kashiriki kufuta vifungu kadhaa Rasimu ya Warioba kuzuia kukimbiza pesa za umma akaunti za uswisi, kufuta tunu za taifa na kuruhusu zawadi za kitaifa kuwa za watawala?