ALIYETUUZIA NYUMBA ZA VIONGOZI NA KUTUNUNULISHA MV DARESALLAM MBOVU NDIYE ANASAFISHIKA???
ii au
Lowassa hasafishiki
Na Mwandishi wetu - Imechapwa 06 April 2011
JUHUDI za waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kujisafisha mbele ya jamii, zimegonga mwamba baada ya kubainika kuwa ni serikali iliyoingiza kampuni ya Richmond katika mkataba wa kufua umeme.
Wakati huo, maelekezo yote kuhusiana na utoaji mkataba kwa Richmond yalikuwa yakifanyika chini ya Lowassa, kwa mujibu wa waziri wa nishati wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha.
Ilibainika katika kikao baina ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali na makatibu wakuu wa Fedha na Nishati, kwamba TANESCO ililazimishwa na serikali kuingia mkataba na kampuni ya kitapeli ya Richmond.
Taarifa zimeeleza kuwa serikali ilitupilia mbali sheria zote za manunuzi na mikataba ili âkulazimisha na kulinda Richmond kupewa zabuni.â
Kamati teule ya bunge, katika uchunguzi wake wa kashfa hii, pamoja na kutaja wahusika wote na kutaka wawajibishwe, ilimwacha waziri mkuu âkuchukua uamuziâ anaoona unafaa. Lowassa alijiuluzu.
Taarifa zinaonyesha serikali iliingia mchakato wa kupata mzabuni, hata baada ya TANESCO kuona kuwa hakukuwepo mshindi kwa mujibu wa zabuni.
Kinyume na maoni ya TANESCO, wizara ya nishati, baada ya kupitia maombi ya zabuni, iliamuru bodi kukubali kuwa Richmond ndiye mshindi na Juni 19, 2009 wizara ikaagiza TANESCO kusaini mkataba na Richmond.
Katika uchunguzi wa bunge, ilibainika kuwa Richmond haikuwa na fedha, uwezo wa kiufundi, vitendea kazi wala uzoefu katika miradi kama hii.
Mkataba wa Richmond ulirithiwa na kampuni ya Dowans Holdings SA ya Costa Rica na Dowans Tanzania Limited (DTL).
Kwa mujibu wa Ibara ya 68 ya sheria ya manunuzi ya mwaka 2004, jukumu la kuamua mshindi wa zabuni ni la bodi ya zabuni ya shirika (TANESCO).
Kwa msingi huo, kamati iliyoteuliwa na serikali kushughulikia mkataba na zabuni, haikuwa na mamlaka ya kisheria ya kufanya uamuzi kuhusu zabuni.
Hiki ndicho chanzo cha kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma kufikia hitimisho wiki iliyopita kwamba ni serikali inayopaswa kubeba mzigo kwa vile TANESCO ilikuwa ikiamriwa tu.
Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara (ICC) iliamua katika kesi ya madai, Novemba mwaka jama, kuwa TANESCO ilipe Dowans na Richmond dola 62.4 milioni (sawa na Sh. 94 bilioni) kwa kuvunja mkataba wake.
Tayari Dowans wamesajili uamuzi wa ICC mahakama kuu kama utaraibu wa kulipwa unayotakiwa.
Hata hivyo, TANESCO inapinga tozo hiyo. Katika utetezi wake, shirika hilo la umeme, pamoja na hoja nyingine, inawasilisha pia kuwa ililazimishwa na serikali kuingia katika mkataba.
Wachunguzi wa mambo ya utawala bora wanasema Lowassa, ambaye aliwahi kukiri kuwa alikuwa karibu sana na mchakato wa kupata mfua umeme, hawezi kujinasua katika kashfa hii.
âHilo siyo swali, hata wewe unaona na Lowassa mwenye aliliona ndiyo maana aliamua kujiuzulu kabla hajafukuzwa au kabla bunge halijataka achukuliwe hatua,â ameeleza kiongozi mmoja wa asasi ya kijamii inayofundisha masual ya utawala bora.
chanzo Mwanahalisi
Lowassa hasafishiki
Na Mwandishi wetu - Imechapwa 06 April 2011
JUHUDI za waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kujisafisha mbele ya jamii, zimegonga mwamba baada ya kubainika kuwa ni serikali iliyoingiza kampuni ya Richmond katika mkataba wa kufua umeme.
Wakati huo, maelekezo yote kuhusiana na utoaji mkataba kwa Richmond yalikuwa yakifanyika chini ya Lowassa, kwa mujibu wa waziri wa nishati wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha.
Ilibainika katika kikao baina ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali na makatibu wakuu wa Fedha na Nishati, kwamba TANESCO ililazimishwa na serikali kuingia mkataba na kampuni ya kitapeli ya Richmond.
Taarifa zimeeleza kuwa serikali ilitupilia mbali sheria zote za manunuzi na mikataba ili kulazimisha na kulinda Richmond kupewa zabuni.
Kamati teule ya bunge, katika uchunguzi wake wa kashfa hii, pamoja na kutaja wahusika wote na kutaka wawajibishwe, ilimwacha waziri mkuu kuchukua uamuzi anaoona unafaa. Lowassa alijiuluzu.
Taarifa zinaonyesha serikali iliingia mchakato wa kupata mzabuni, hata baada ya TANESCO kuona kuwa hakukuwepo mshindi kwa mujibu wa zabuni.
Kinyume na maoni ya TANESCO, wizara ya nishati, baada ya kupitia maombi ya zabuni, iliamuru bodi kukubali kuwa Richmond ndiye mshindi na Juni 19, 2009 wizara ikaagiza TANESCO kusaini mkataba na Richmond.
Katika uchunguzi wa bunge, ilibainika kuwa Richmond haikuwa na fedha, uwezo wa kiufundi, vitendea kazi wala uzoefu katika miradi kama hii.
Mkataba wa Richmond ulirithiwa na kampuni ya Dowans Holdings SA ya Costa Rica na Dowans Tanzania Limited (DTL).
Kwa mujibu wa Ibara ya 68 ya sheria ya manunuzi ya mwaka 2004, jukumu la kuamua mshindi wa zabuni ni la bodi ya zabuni ya shirika (TANESCO).
Kwa msingi huo, kamati iliyoteuliwa na serikali kushughulikia mkataba na zabuni, haikuwa na mamlaka ya kisheria ya kufanya uamuzi kuhusu zabuni.
Hiki ndicho chanzo cha kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma kufikia hitimisho wiki iliyopita kwamba ni serikali inayopaswa kubeba mzigo kwa vile TANESCO ilikuwa ikiamriwa tu.
Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara (ICC) iliamua katika kesi ya madai, Novemba mwaka jama, kuwa TANESCO ilipe Dowans na Richmond dola 62.4 milioni (sawa na Sh. 94 bilioni) kwa kuvunja mkataba wake.
Tayari Dowans wamesajili uamuzi wa ICC mahakama kuu kama utaraibu wa kulipwa unayotakiwa.
Hata hivyo, TANESCO inapinga tozo hiyo. Katika utetezi wake, shirika hilo la umeme, pamoja na hoja nyingine, inawasilisha pia kuwa ililazimishwa na serikali kuingia katika mkataba.
Wachunguzi wa mambo ya utawala bora wanasema Lowassa, ambaye aliwahi kukiri kuwa alikuwa karibu sana na mchakato wa kupata mfua umeme, hawezi kujinasua katika kashfa hii.
Hilo siyo swali, hata wewe unaona na Lowassa mwenye aliliona ndiyo maana aliamua kujiuzulu kabla hajafukuzwa au kabla bunge halijataka achukuliwe hatua, ameeleza kiongozi mmoja wa asasi ya kijamii inayofundisha masual ya utawala bora.
chanzo Mwanahalisi
Hivi tundu lissu kaingia bungeni mwaka gani
Hebu katafute kazi hapo lumumba hapakufai huna kumbukumbu
Lowasa kachoka hawezi kushinda popote pale kuanzia mwili mpaka akili anatawaliwa na ufisadi wa wazi kabisa mzee mwizi sana.
shida ya haya chadema yanafanyabiashara kwenye siasa wanawaona watanzania kama hatuna akili vile.
Maskini magamba mnahaha,magamba Lowasa amewakosea nini?mbona mna gubu nae kiasi hiki?
ukweli unauma subirin matusi na sio hoja
Siku zote nyumbu hawana hoja. Kwao matusi ndo mtaji wao
Hao unaowataka wameanza kununuana hata kabla hawajafika Ikulu, wakifika Ikulu si ndo watakuwa fundi mchundo? Lakini pia ni bora tukawa na wale wenye kujua kulinda amani kuliko wakutuletea vita asubuhi
Mleta mada na wachangia mada mliomsapoti vema mkaacha ushabiki,kana kwamba mnaishi sayari ingine.Hivi kipi kikubwa na cha ajabu kumshambulia mtu ikiwa nukuu iliyowekwa hapa iko wazi,NANUKUU
Kamati teule ya bunge, katika uchunguzi wake wa kashfa hii, pamoja na kutaja wahusika wote na kutaka wawajibishwe, ilimwacha waziri mkuu kuchukua uamuzi anaoona unafaa. Lowassa alijiuluzu.Jiulize kwa nini kamati teule ilimwacha waziri mkuu?Jibu ni rahisi sana,haikuonekana kosa linalomuhusu moja kwa moja.Na ndio maana kamati ilishindwa hata kumuita na kumuhoji.Pamoja na hayo,Mh.Lowassa akaamua kujiuzuru,ni ujasiri wa hali ya juu sana.Je,mlitaka agome kama walivyofanya wengine wengi tu?Swali,ikiwa Lowassa ndio mwizi na fisadi kuliko wote katka nchi hii,mbona ile mitambo mpaka leo ipo na pesa zinaendelea kulipwa?Ni nani anaelipwa au ni Lowassa?Ni takribani miaka nane sasa,sheria ziko wapi?Acheni ushabiki usio na maana,ni vema tukajadili mambo ya msingi Kitaifa.Inashangaza sana kuona hata viongozi wasomi na wakubwa ktk nchi hii,wamekazana kuupotosha umma,wanaacha kutumia taaluma,elimu na uwezo mkubwa waliojaaliwa na MUNGU,kuleta majawabu ya nini kifanyike ili kuondokana na kero za nchi hii,wanatuletea propaganda za funika kombe mwanaharamu apite,pasipo kujali Watanzania kesho wataamkaje.Kuna mangapi tena makubwa kuliko Richmond tena mengi tu,mbona hatuyazungumzi?Nini msimamo wangu:-Ningalikuwa ninayo maamuzi ya mwisho,mwaka huu ningeshauri kuwe na mfumo wa serikali kama MAREKANI,kisiwe chama kimoja kinaongoza kuanzia Rais,ubunge,udiwani mpaka serikali za mitaa,Badala yake kuwe na balance itakayoondosha kujisahau na kujinufaisha watu wachache na kuwaacha wengi wakitaabika.Jamani nchi hii ni yetu sote tuache ubinafsi,mwisho wa siku litakuwa bomu,na kilio hata asipatikane mtu wa kufuta machozi.Mwl Nyerere alisema!
Mbona mgumu kuelewa wewe kiumbe!!? hizo shule za kata ni wazo lake au kwa mantiki nyingine ni maono yake (ndio maana viongozi bila maono taifa huangamia) sema tu ccm ikageuza wazo hilo au maono hayo kama sera na kwa upande mwingine ni sehemu ya kula kodi zetu!Mbona shule za kata anadai alijenga yeye na amumuulizi hayo maswali badala yake mnabaki tu mnasema ndio mzee?