Lowassa: Harusi yageuka matanga

Lowassa: Harusi yageuka matanga

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,665
Tumeshuhudia mbuyu ukichinjwa kwa wembe na kuanguka chali. Hii ni tamthiliya ya 4U Movement iliyoratibu project ya kumuingiza Lowassa Ikulu ya Magogoni.

Wadadisi wa mambo wamekuwa na maswali yasiyojibiwa hasa kuhusu ULAZIMA wa kuhakikisha Lowassa anapitishwa na chama chake kwa gharama zozote. Swali lingine ni tija ya projekti nzima kwa Watanzania...

Je waliohusika na mradi huu wanarandana na haiba ya mtu wao? Hapa nazungumzia watu kama Apson, Kingunge, Rostam, Chenge, Nchimbi n.k.

Je chaguo la Watanzania ni chaguo lao? Au chaguo lao ndilo chaguo la Watanzania?

Udadisi hauishii hapo bali plan B ya Wezesha Lowassa na utiifu wa kundi lake kwake nk.

Tambo za Lowassa kuwa hakuna wa KUMKATA jina lake kwenye hatua zote za mchujo, ni wazi kuna egemeo thabiti la ndani ya chama alilokuwa amejiaminisha kwake. Inawezekana mtaji wa wajumbe wa NEC na hamasisho la wajumbe wa mkutano mkuu, inawezekana vilimpa imani kuwa ana kundi kubwa linalomuunga mkono.

Tangu mteule wa CCM kupatikana, Lowassa amekuwa kimya kumuunga mkono au kukosoa mfumo uliofikisha utimilifu wa mchakato mzima. Hivyo haiyumkiniki plan B inaweza kuleta kishindo ama maumivu zaidi.

Shamrashamra, majivuno na tambo za mashabiki wa Lowassa ambapo walithubutu kutumia CCM kama kichaka chao hata kukiuka taratibu, kanuni na maadili ya Chama kwa kigezo cha kupendwa vimegeuka simanzi na fadhaa nzito kwao.

Hakuna tofauti na msiba kugeuka matanga na historia haibadilishwi...
 
This is just the beginning my friend..... This is like the sleeping volcano my friend....!!!
This is the state of something dreadful my friend...!!!
mshana jr upo salama kweli?
Mbona unajiamini hivyo? Hatuna raha huku mtaani, please Tupe hilo aminisho lako mkuu ili tusizidi kunjong'onyea
 
Last edited by a moderator:
mshana jr upo salama kweli?
Mbona unajiamini hivyo? Hatuna raha huku mtaani, please Tupe hilo aminisho lako mkuu ili tusizidi kunjong'onyea

Omba Mungu akupe maisha marefu....! Tutakumbushana hii post bdo
 
Last edited by a moderator:
mshana jr upo salama kweli?
Mbona unajiamini hivyo? Hatuna raha huku mtaani, please Tupe hilo aminisho lako mkuu ili tusizidi kunjong'onyea

Omba Mungu akupe maisha marefu....! Tutakumbushana hii post bdo
 
Last edited by a moderator:
mshana jr upo salama kweli?
Mbona unajiamini hivyo? Hatuna raha huku mtaani, please Tupe hilo aminisho lako mkuu ili tusizidi kunjong'onyea

nyie nyongeeni tu si safari ya ikulu ilishaanza...kilichomkalisha kimya dodoma ni nini kama ile kitu ilikuwa 'rough'? alafu lowassa ni nani yeye kila atakalo liwe kama alivyolipanga? hya ni maisha yanayohusisha binadamu ambao hawatabiriki..na kumbuka lolote linalomhusisha binadamu halitabiriki. Lowassa alijisahau kwamba mipango anapanga na "binadamu"ambao kubadilika ni sekunde.
 
Last edited by a moderator:
Usalama wa taifa hawapo? Kama wapo mbona wanashindwa kuwapata? USA Yule jamaa aliyeua blacks kanisani alipatikana ndani ya 24hrs kama hatuna technology kwanini tusiinvest? znz,Nairobi wameweza why Dsm washindwe? tukisema hayo matukio wanafanya wao wenyewe tutakuwa tumekosea?
 
Tasisi ya urais ndiyo tasisi kuu kuliko zote kitaifa. Ndiyo tasisi inayosimamia mihili mingine yote ya Taifa kwa niaba ya Wananchi. Ndiyo maana rais anapatikana kwa ridhaa ya wananchi wote, wa vyama mbali mbali na wasio na vyama vya kisiasa. Sheria zinazotungwa na Bunge (la vyama vingi siku hizi) haviwezi kuwa sheria bila kupata ridhaa ya Rais kwa niaba ya wananchi walio wengi waliomchagua. Rais kwa niaba ya wananchi amepewa mamlaka ya kuteuwa na kuwawajibisha wakuu wa mhili wa mahakama na wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Taifa, yote haya ni kwa niaba ya wananchi wote bila kujali vyama vyao kisiasa nk

Sasa mchakato wa kupata mkuu wa tasisi hii ya urais haiwezekani kufanyika kihuni huni namna hii kama baadhi ya makundi ya watu walivyokuwa wanafanya, iwe kwenye chama tawala au upinzani.

Hii iwe fundisho kwa wote kwa siku zijazo. Mambo ya makundi hayakubaliki, na katiba za vyama na nchi ziliweke hili wazi.
 
Maamuzi atakayoyafanya mhusika anayezungumziwa kwenye uzi..yatawashangaza watanzania kuanzia viongozi wa ccm..😀😀
 
Kuna watu lowasa ni km maji yao ya uzima. Akiacha siasa wanakufa njaa ndo maana wanajitahidi hata kumshauri uongo ili tu aendelee kutumia mabilioni mengine.
Ukimwangalia sn lowasa amekuwa km teja
 
Mipango yake mingine ni anguko lake, hawa waliomwangusha Dodoma hawako kimya kumwacha afurukute tena kihuni kwingine kama alivyofanya ccm,kwa kujiongeza tu ni kwa nini anataka Urais kwa nguvu hivyo
 
Kuna watu lowasa ni km maji yao ya uzima. Akiacha siasa wanakufa njaa ndo maana wanajitahidi hata kumshauri uongo ili tu aendelee kutumia mabilioni mengine.
Ukimwangalia sn lowasa amekuwa km teja

Ovyo sana hawa mkuu. Walitaka kutupandikizia mtu wa ovyo ikulu.

Wakatafute kazi ingine ya kufanya. Waendekeza njaa wakubwa hao
 
Back
Top Bottom