Ndugu wana Jamvi Asalaam Aleykum or Bwana Asifiwe !! , Hatimae Mr JK azuia mafuriko ya Mr EL kwa Mkono. Hongera sana JK na Pole sana EL. Hii ndiyo SIASA na JK ni mwana Siasa Bora. Mr. EL please achana na SIASA kwani UMESHINDWA !!! Elewa Siasa ni Zaidi ya Mshiko ulio nao, na nasema tena POLE SANA. Kwa Ushauri wangu Elekeza Mshiko wako katika kusaidia Jamii hasa Vijana kiuchumi na Kielimu kwani Unamshiko Mwingi kiasi wa kukutia wazimu !! Ndugu wana Jamvi wakati wenye nguvu CCM wanaungana baada ya kumdondosha bepari wao ili kuendelea Kumnyonya Mnyonge wa Nchi hii, ni Vizuri sisi wanyonge Kuungana pamoja ili Kumkabili Mwenye nguvu huyu CCM ili asiendelee Kutunyonya !! Kwanza tujipange kupunguza wingi wa wabunge wa CCM ili kumpunguzia nguvu Bwanyenye Huyu , Hivyo basi kila mmoja wetu atumie nafasi yake kuelimisha wa TZ wenzetu hasa Vijijini waweze Kuelewa SOMO hili , na Pale tunapoona kuna wa Bunge Mahiri wa Upande wa pili ni Wajibu wetu kuwaunga mkono kwa hali na Mali. Wanyonge lazima Tuungane pamoja Kupunguza nguvu za Bwanyenye CCM !! Wasalaam.