Lowassa hakudhuria Msiba wa Mwalimu Nyerere

Lowassa hakudhuria Msiba wa Mwalimu Nyerere

Kuna jamaa kaniambia kuwa tangu Mwaka 1990 Lowasa hajawahi kwenda Butiama hata wakati Mwalimu yupo.

Mwalimu alipatwa Msiba wa kaka yake Kiboko Nyerere Lowasa hakuhudhuria.

Mwalimu alifiwa na Mama yake Mzazi Bibi Mogaya Nyerere watu wote walifika kuhani msiba isipokuwa Lowasa.

Nyerere ameugua mpaka anakufa Lowasa hapata kumwona wala kufika kutoa pole.

Msiba umefanyika Butiama, Nchi nzima ilizizima, Watu wengi walifika Lakini Lowasa hakufika.

Huyu mtu wenu ana walakini. Kazi ipo.
Kama na haya ni kweli ni bora asiende huko msibani. Itakuwa ni aibu sanaaa
 
Lowasa anavisasi sana baada ya kuambiwa wazi juu ya ufisadi wake anahaha tu.
 
LOWASA ANA MAHUSIANO MAZURI NA WATU WOTE TANZANIA , ILA SINA HAKIKA NA WATU WAWILI , HISIA ZANGU, MAANA SIJAWAHI KUONA WALA KUKUTA WAMESIMAMA KWA KARIBU, KAMA UNAKANUSHA ,NITAFUTIE ANGALAU PICHA LOWASA WAPO KARIBU AMA WAMESHIKANA MIKONO NA 1.MH. PAULO MAKONDA (Mkuu wa wilaya Kinondoni) 2.Mh, Bernad Membe (waziri wa mambo ya nje ya nchi)
View attachment 251420
lowasa ushindi copy.jpg
 
Mkuu DSN ngoja niweke clear hapa, mimi simshabikii mtu, wala sina habari za team Lowasa sijui team Membe etc, ninachosema hapa ni kwamba issue ya bifu la Nyerere na Lowasa bado sioni kama ni point kubw ya kum disqualify Lowasa, zipo points kubwa zenye mashiko bana, sio issue ya kutohudhuria msiba wa Nyerere.

Alafu niite hizi hoja kama siasa za maji taka yaani msiba wa Nyerere ulitokea tarehe 14 October 1999, leo ndo muanze kusema Lowasa hakuhudhuria msiba wa Mwalimu?

Kisa nini kwa sababu anataka kugombea urais? Mbona hamkusema hizi hoja wakati anaapishwa kua waziri mkuu??

Kwa siasa hizi tutabaki kua maskini kila karne.

Mtazamo wangu

Lowasa angekua dis qualified kwa mambo mengine kama rushwa, haya ndo yenye kugusa maslahi ya taifa moja kwa moja sio msiba wa mtu mara bifu lao wenyewe unataka liwe bifu la taifa.

Well said natoka hapa dont forget hoja hiyo ilisemwa sana akiwa madarakani...alisumbuliwa sana vijimaneno mpaka humu JF...ajakaa sawa ubao ukapinduka mzigo ukamwagwa..ndio watanzania wakasahau la Mwalimu na kupaa kwa ndege ya maisha na team lowasa ,,,wakaanza na Richmond...sasa alipoanza kuonyesha kuwa anaitaji kuingia OFISI KUU ndio wakakumbuka na yale ya nyuma yanaanza kuludi....what goes around comes around.

Ndio kusema unapokuwa Kiongozi kuna mambo yako binafsi inabidi uyaweka kando ili uweze kufanana na jumla ya walio wengi ambao unategemea kuwaongoza.Ndio maana kwa mindset ya Watanzania ukisema umtambui Nyerere na ukataka URAIS basi ni disqualification kwao kuwa uwafai.Hoja yako kusema asimtambue Mwalimu na kuappreciate maamuzi yake katika kuliasisi na kulijenga Taifa hili kisha aombe kupewa ukuu wa Taifa mmmh naona itakuwa ngumu sana ..kitakachotokea ni wenzie kumchezea chezea masile muda ukifika panga pindua ahaaa imekuwaje...ishatokaa...kama walivyopindua pindua kwenye Uwaziri Mkuu...leo hii ukuu wenyewee...ngumu sana kuliko unavyodhani.
 
Lowasa hafai kukaa na binadamu ile roho yake siyo ya kukaa na watu kabisa.
 
Lowasa anavisasi sana baada ya kuambiwa wazi juu ya ufisadi wake anahaha tu.

Kama hii comment imeandikwa na Simiyu Yetu basi inaashiria CCM ni vipande vipande maana hata Simiyu Yetu inaonekana hayuko na EL.

Economic importance of the kingdom
1. Wafu wanazikana wenyewe sasa.

2. Hata mwenye hatia naye sasa anatusaidia kuwatambua wenye hatia wenzie
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Ccm mnapenda kutumia misiba hadi mmefikia hatua ya kugombea huu msiba kama wachawi.
 
GAZETI acha kurahisisha mambo,lowasa kutohudhuria msiba wa aliyekuwa mwasisi wa taifa hili ni dhahiri hafai kuwa kiongozi wa taifa hili....maana kutohudhura msiba huo ni kutokuwa na uvumilivu wa kiasa maana mwalimu alikuwa hamkubali lowasa hata kidogo ndio maana akalipiza kisasi kwa mwalimu na sisi pia tutalipiza kisasi kwenye sanduku la wapiga kura.

Tusichaguwe viongozi kwa kulipiza visasi. Hiyo italipeleka Taifa kubaya.
Pamoja na hivyo lowassa hafai.
 
Lowassa anahukumiwa na Historia ya kutokuwa na Mahusiano mazuri na Familia ya Mwalimu Nyerere. Lowassa hajawahi kufika Butiama Tangu Mwalimu afariki.

Lowassa hakuhudhuria Msiba wa Baba wa Taifa. Ni Mgombea pekee wa Urais ambaye hajui kaburi la Baba wa Taifa liko wapi.

Inasemekana alishangilia na kufanya tafrija fupi Monduli wakati Watanzania wanaomboleza Mwezi Mzima Butiama.

Huyu hakuwa na Mahusiano mazuri na Mwalimu aliyependa viongozi waadilifu. Lowassa kakwepa mara nyingi kwenda Butiama kwasababu ya kuogopa Mzimu wa Nyerere. Nafsi inamsuta kwasababu hakudhuria Mazishi ya Mwalimu, Doa na kumbukumbu hii haiwezi kufutika hata awe nani leo mpaka kesho.

Leo anagombea Urais, umepatikana msiba wa kijana wa Mwalimu, Marehemu John Nyerere inasemwa Lowassa atakwenda Butiama, Lahaula! Kwasababu gani?

Au kwakuwa Msiba umevuta hisia za wengi? Au kwasababu Msiba umetokea kipindi muhimu kuelekea uchaguzi? Kwasababu msiba utakusanya walio wengi wa Muhimu? Au kwakuwa kwasasa itakuwa rahisi kujulikana kuwa hukuhudhuria?

Mbona sijakuona Msasani Dar es Salaam?? Maana unavyopenda picha zingekuwa Magazetini.

Acha unafiki kama hufika Msiba wa Baba wa Mtoto wake unakusibu nini? Sikatalii msiba la hasha! Ni mshangao kama Lowassa amesahau kuwa Mzimu wa Nyerere bado upo na unaishi, utamzukia Butiama na kumuangusha?
Maana haujapata kumuona tangu Mwalimu amefukiwa Mwitongo.

Leo Familia itashangaa, Wazee wa Zanaki watashangaa, Wanaojua siri hii watakushangaa.

Nenda lakini Mzimu wa Mwalimu unakusuta! Ulikuwa wapi siku zote?

Tuko wa TZ zaidi ya 44M, katika hao ...
1. Wangapi wahudhuria msiba wa Nyerere..??
2. Kati hao, wangapi washafika kwenye kaburi la Nyerere..??
3. Katika hao wangapi wameshawahi fika nyumbani kwake..??

HIVI YEYE NI BABA WA TAIFA AU NI BABA WA WANAOPAJUWA KABURINI KWAKE..??? WALIOHUDHURIA MSIBA WAKE..??
 
nakumbuka kuna watu walikwenda katika huo msiba
kwa ndege za kukodi,jioni wanapanda ndege kwenda kulala nairobi
asubuhi wanarudi msibani.
Labda alikosa sehemu ya kulala.
You know ''lower sir''?
Yote hiyo ni kwa sababu kama hii hapa chini.....wenzie wadiliki kulala Nairobi na kuludi msibani, manake ni kuwa walikuwa na political vision ya kesho kwao itakuwa ni msingi wa kupata support ya umma ambao kwao Mwalimu ni Baba wa kaya.

Mwalimu Gado-CartoonCCM.jpg
 
Na nyie mliotupa mchanga kwenye kaburi la Nyerere mna lipi la kutuambia? Kwamba Nyerere alikuwa fisadi?
 
Wewe ulienda kwenye msiba wa baba wa taifa.?????? Acha propaganda za kizamani wewe
 
Mbona Dr.Slaa hakudhuria msiba wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, au yeye hamna tatizo.

kwa hiyo mtu akibaka na wewe utabaka kutokana na flani alibaka ?
 
Lowasa ni MTU wa kisasi !! Na fisadi mkubwa utajiri wake una maswali mengi????
 
Naombeni mniambie utaratibu wa kukataa uraia wa taifa lako,maana yake ni kwamba nina mpango iwapo lowassa atatangazwa na ccm kua mgombea urais tu nabadili uraia wangua au nakataa uraia wa Tanganyika na kua msomalia au mrwanda.

Naomba kujua utaratibu huo wakuu.
 
Back
Top Bottom