Lowassa awakaribisha CHADEMA/UKAWA waliotimuliwa CCM

hata yule mnaefanana mwenye sura ya sokwe nae alisemaga hivihivi mwaka juzi kuwa cdm inakufa 2014...
sasa wewe endeleza uzombie wenyu
cdm inakanyaga twende
Hizi lugha zisizo na staha za nini??
Mbona nyie vijana wa chadema mkikosolewa mnakimbilia matusi?
 
chukueni makapi hayo, mbn tumeshawazoea
Mtu akihama CCM ndio makapi ila akihamia shujaa. Hivi kati ya Madabida au Sophia Simba na Machali aliyepitia vyama takriban sita na bado akaupoteza ubunge nani aitwe makapi hapo? Wengine hadi mwenyekiti wenu anawashtukia anawaita ng'ombe wasio na mkia maana hawaeleweki wanataka nini kwenye siasa, kutwa kuzurura vyamani.
 
Hii inaweza kuandikwa na mtu ambaye ana upeo mdogo au hana kabisa.

Mara kadhaa waropokaji wamekuwa wanasema Lowasa alinunua chama. Ni waropokaji kwa sababu hawajawahi kueleza Lowasa alinunua CHADEMA kwa namna gani na kwa pesa kiasi gani.
Sijawahi kusikia maneno hayo toka kwa kiongozi yeyote ndani ya CCM wala kutoka kwa mwanachama yeyote wa CCM mwenye akili na hekima ila maneno hayo utayasikia kutoka kwa watu ambao hawana mbele wala nyuma katika kuelewa chochote katika Taifa hili.

Wapiga kelele kama hawa wanashusha hata hadhi ya CCM na kuonekana ni chama kilichojaa watu wenye uwezo mdogo wa fikra na wasioweza kujenga hoja.
Aisee.... Kuamini hicho unachokiamini inahitaji ujasiri sana. Kwani Lowasa aliingiaje CHADEMA? Na utaratibu upi uliomweka akawa mgombea pekee tena bila ushindani?
 
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.

Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema
Waliofukuzwa ni wasaliti...!
CCM, inajifunza!
Bashe, Nchimbi, na Msukuma, hawakukisaliti chama!
...unadhani uteuzi wa ubunge wa yule mama wa iringa, aliekuwa na nafasi ktk ccm, haukuwa somo?...alikuwa ni msaliti....teuzi ya ubunge, ndo ilimbadilishia nafasi ya kuhujumu ccm...
Hao waliofurushwa walikuwa wakifanya alichokuwa akikifanya yule mama...ulichelewa kuwazawadia, sasa ccm imewapa, zawadi astahiki yao...
 
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.

Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema
Hizi habari za kuzidi kuwadanganya wananchi inabidi zifike mwisho. Wewe hauna hati miliki ya nchi hii ya Tanzania kwamba bila wewe basi hakuna mwingine! Wakati ukiwa ndani ya CCM, ni jambo gani la maana uliloifanyia nchii? Kilichokukimbiza kwenda UKAWA ni UROHO wa madaraka tu. Ungekuwa kweli ni mwanademokrasi, ungebaki ndani ya chama chako na kukubaliana na maamuzi ya chama. Kama kweli wewe ni mwanademokrasia, je, uko CHADEMA na UKAWA ulishindanishwa na nani hadi ukapita kuwania urais? Kama kweli wewe ni mwanademokrasia, mbona tayari umeshaanza kujitangaza kuwania urais mwaka 2020 wakati hata vikao vya chama havijakaa na kuamua nani atagombea? Ndiyo maana sisi baada kuona umekuja chadema, tuliamua kuondoka. Inasemeka kuwa hata ile RASIMU ya Jaji WARIOBA wewe ni miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba walioikanyaga ile maoni yake yasipitiswe. CCM ipo na itaendelea kuwepo na tutaipigia kura 2020, hizo siasa za kudanganyana kwa sasa hazifai.
 
Siasa za Tanzania zina vituko!

Lowassa ameishapata ''madaraka'' ya kuwakaribisha watu wake baada ya yeye kukaribishwa kwa kutumia nguvu ya pesa mwaka mmoja uliopita!

Sikuwahi kuamini kama maisha ya kisiasa nchini yanaenda kwa kasi ya aina hii ambapo leo Lowassa anadai maisha yake ya kisiasa ni mazuri sana kwa sababu anaweza kufanya lolote analopenda/kutaka na hakuna mtu wa kumzuia ndani ya CHADEMA!

Kununua chama ni raha sana! You can do whatever you want/like!

Money talks hasa kwenye chama chenye viongozi ambao ni wajasiriamali wa kisiasa!
Wewe badala ya kuwa msema ukweli umegeuka kuwa msema uongo.Ni muda muafaka sasa muweke ushahidi wa kiasi cha pesa alicholipa lowasa na njia alizotumia kufanya malipo hayo,au mkae kimya maana naona hoja yako haina maana.
 
Kwa Lowasa yule niliyemuona Arusha siku ya Kesi ya Lema,nachelea kusema kwamba Haya maneno Lowasa ameandikiwa tu..

Lowasa amechoka,hata kuandika sms hana ufahamu huo,nilitamani nizirushe picha nilizompiga lakini naheshimu umri wake na cheo chake cha PM mstaafu!!

Lowasa hata kupanda gari anashindwa,anapandishwa tu kwenye gari,tangia mahakama inaanza mpaka inaisha babu wa watu alikuwa anasinzia tu,alishituliwa na sauti ya askari aliyepiga koooortiiii ndipo mzee akaamka na kumuangalia Mbowe usoni..

Musimsingizie Lowassa wa watu...Lowassa ameshajichokea kabisa,muacheni apumzike!!

Hakika Parkinson's disease ni ugonjwa mbaya sana
Acha ujinga wewe ugonjwa wake unahusiana vipi na kilicholetwa hapa na mtoa mada usiandike kwa kukurupuka..swala la kuchoka ama kutokuchoka anajua mama Regina peke yake au ndo wewe nini
 
Siasa za Tanzania zina vituko!

Lowassa ameishapata ''madaraka'' ya kuwakaribisha watu wake baada ya yeye kukaribishwa kwa kutumia nguvu ya pesa mwaka mmoja uliopita!

Sikuwahi kuamini kama maisha ya kisiasa nchini yanaenda kwa kasi ya aina hii ambapo leo Lowassa anadai maisha yake ya kisiasa ni mazuri sana kwa sababu anaweza kufanya lolote analopenda/kutaka na hakuna mtu wa kumzuia ndani ya CHADEMA!

Kununua chama ni raha sana! You can do whatever you want/like!

Money talks hasa kwenye chama chenye viongozi ambao ni wajasiriamali wa kisiasa!
Wapumbafu wenzako na ufinyo wenu wa akili watakuona umeandika ya maaanaaa.,kumbe ushuzi mtupu kama akili yako....
 
Mtu wa kwanza duniani kupoteza uaminifu ni mwanasiasa,yupo tayari kuuza utu wake maslahi mbele,wachumia tumbo!
 
b72fe70b83017c03d49d6bf059e870f9.jpg
msibani kwa sir George Kahama
 
Waje tu wala wasichelewa na waandaliwe mapokezi makubwa tena yawe live na siku hiyo wawaeleze wananchi sababu ya wao kufukuzwa mmoja baada ya mwingine au baadhi wawakilishe wenzao.

Tukio liwe live ikiwezekana zaidi ya channel 3 na wafanye siku ya week-end.
Madabida Huyu Huyu mliyemtukana kwa ARVs fake? Apokelewe kwa maandamano? Chadema ni zaidi ya genge la matapeli
 
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.

Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema

Kila chama au kundi la watu lina kanuni zake, Lowassa anapowaaminisha watu waliofukuzwa wameonea hayupo sahihi. Mwanachama anapokuwa masaliti kwa chama adhabu yake ni kuvuliwa uanachama. Zitto Kabwe alivuliwa uanachama Chadema , Kitila Mkumba alivuliwa uanachama Chadema...juzi juzi Prof. Lipumba CUF walitaka kumvua uanachama.............tusiwe kama Nyumbu.
 
Back
Top Bottom