Lowassa awakaribisha CHADEMA/UKAWA waliotimuliwa CCM

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.

Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema
 
Siasa za Tanzania zina vituko!

Lowassa ameishapata ''madaraka'' ya kuwakaribisha watu wake baada ya yeye kukaribishwa kwa kutumia nguvu ya pesa mwaka mmoja uliopita!

Sikuwahi kuamini kama maisha ya kisiasa nchini yanaenda kwa kasi ya aina hii ambapo leo Lowassa anadai maisha yake ya kisiasa ni mazuri sana kwa sababu anaweza kufanya lolote analopenda/kutaka na hakuna mtu wa kumzuia ndani ya CHADEMA!

Kununua chama ni raha sana! You can do whatever you want/like!

Money talks hasa kwenye chama chenye viongozi ambao ni wajasiriamali wa kisiasa!
 
Waje tu wala wasichelewa na waandaliwe mapokezi makubwa tena yawe live na siku hiyo wawaeleze wananchi sababu ya wao kufukuzwa mmoja baada ya mwingine au baadhi wawakilishe wenzao.

Tukio liwe live ikiwezekana zaidi ya channel 3 na wafanye siku ya week-end.
 
Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.
YEYE HAKUONA alivyo mfanyia Dr SLAA dhuluma ya kuzuia Dr SLAA kuwa mgombea urais kupitia CHADEMA?????.....Yaani mtu UNAKUJA KUPOKONYA WENZIO TONGE MDOMONI hata haujui uo ugali walisonga vipi .....Ni upuuzi kuamini LOWASSA nae ni muumini anaeamini uwepo wa DEMOKRASIA angekuwa ana amini hivyo ANGERUHUSU MCHAKATO WA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA KUCHAGUA MGOMBEA na si kujipendekeza yeye bila ushindani.....
 
Lowassa siyo mropokaji na wala hasukumwi na mihemko ya matukio, omba radhi mleta mada kwa kumlisha maneno kamanda Lowass
 
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.

Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema
Kama muhalifu ni mtaji wachukue.
 
YEYE HAKUONA alivyo mfanyia Dr SLAA dhuluma ya SLAA kuwa mgombea urai kupitia CHADEMA?????.....Yaani mtu UNAKUJA KUPOKONYA WENZIO TONGE MDOMONI hata haujui uo ugali walisonga vipi.....Ni upuuzi kuamini LOWASSA nae ni mtu wa kuamini katika DEMOKRASIA angekuwa ana amini hivyo ANGERUHUSU MCHAKATO WA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA KUCHAGUA MGOMBEA na si kujipendekeza yeye bila ushindani
Slaa anaongozwa na Josephine asingeweza kuongoza nchi

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom