Lowassa awakaribisha CHADEMA/UKAWA waliotimuliwa CCM

Lowassa awakaribisha CHADEMA/UKAWA waliotimuliwa CCM

Lowassa huwezi kkumlinganisha nao mtu yeyote huko misri QUOTE="Kigodoro, post: 20112937, member: 223497"]Lowassa siyo mropokaji na wala hasukumwi na mihemko ya matukio, omba radhi mleta mada kwa kumlisha maneno kamanda Lowass[/QUOTE]
 
Hii inaweza kuandikwa na mtu ambaye ana upeo mdogo au hana kabisa.

Mara kadhaa waropokaji wamekuwa wanasema Lowasa alinunua chama. Ni waropokaji kwa sababu hawajawahi kueleza Lowasa alinunua CHADEMA kwa namna gani na kwa pesa kiasi gani.
Sijawahi kusikia maneno hayo toka kwa kiongozi yeyote ndani ya CCM wala kutoka kwa mwanachama yeyote wa CCM mwenye akili na hekima ila maneno hayo utayasikia kutoka kwa watu ambao hawana mbele wala nyuma katika kuelewa chochote katika Taifa hili.

Wapiga kelele kama hawa wanashusha hata hadhi ya CCM na kuonekana ni chama kilichojaa watu wenye uwezo mdogo wa fikra na wasioweza kujenga hoja.
Chadema iliuzwa kwa billion kumi kwa Lowasa.

Dj akakimbia fasta fasta kwenda kuficha pesa ulaya
 
Waje tu wala wasichelewa na waandaliwe mapokezi makubwa tena yawe live na siku hiyo wawaeleze wananchi sababu ya wao kufukuzwa mmoja baada ya mwingine au baadhi wawakilishe wenzao.

Tukio liwe live ikiwezekana zaidi ya channel 3 na wafanye siku ya week-end.
Hakuna haja ya wao kuwaeleza wananchi kwakuwa wananchi tunajua kuwa hao ni wasakatonge na mtandao uliokuwa ukijiandaa kuifirisi nchi yetu...wananchi tunajua wala wasijisumbue
 
Siasa za Tanzania zina vituko!

Lowassa ameishapata ''madaraka'' ya kuwakaribisha watu wake baada ya yeye kukaribishwa kwa kutumia nguvu ya pesa mwaka mmoja uliopita!

Sikuwahi kuamini kama maisha ya kisiasa nchini yanaenda kwa kasi ya aina hii ambapo leo Lowassa anadai maisha yake ya kisiasa ni mazuri sana kwa sababu anaweza kufanya lolote analopenda/kutaka na hakuna mtu wa kumzuia ndani ya CHADEMA!

Kununua chama ni raha sana! You can do whatever you want/like!

Money talks hasa kwenye chama chenye viongozi ambao ni wajasiriamali wa kisiasa!
Hapo ndio mwanzo na mwisho wa uwezo wako wa kufikiri? Poor you!
 
Tuwapokee wote katika ujumla wao; mabadiliko ya kweli yatakuja kutokana na kuparaganyika kwa ccm
 
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.

Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema
Awali kabisa ulisema ccm imekukuza hivyo huna mpango wa kuihama ccm.
Tena ukasisitizia kwamba wewe utakuwa ni wa mwisho kuihama ccm.
Sasa ilikuwaje ukayakana hayo maneno yako.
 
Kwa Lowasa yule niliyemuona Arusha siku ya Kesi ya Lema,nachelea kusema kwamba Haya maneno Lowasa ameandikiwa tu..

Lowasa amechoka,hata kuandika sms hana ufahamu huo,nilitamani nizirushe picha nilizompiga lakini naheshimu umri wake na cheo chake cha PM mstaafu!!

Lowasa hata kupanda gari anashindwa,anapandishwa tu kwenye gari,tangia mahakama inaanza mpaka inaisha babu wa watu alikuwa anasinzia tu,alishituliwa na sauti ya askari aliyepiga koooortiiii ndipo mzee akaamka na kumuangalia Mbowe usoni..

Musimsingizie Lowassa wa watu...Lowassa ameshajichokea kabisa,muacheni apumzike!!

Hakika Parkinson's disease ni ugonjwa mbaya sana
 
Hawa si alisema wangehama naye tangu mwanzo? Walikuwa wanasubiri nini mpaka leo wanatimuliwa.
 
Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.

Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema
SAWA LOWASA MWENYEKITI WA SASA WA CHADEMA, MAANA NAAMINI HUYO MWINGINE WA KUCHAGULIWA UMESHAMTIA KWENYE MFUKO WA SHATI KANYAMAZA KIMYAA ANAKULA HELA YAKE YA UDALALI NA YA KUBADILISHA GIA ANGANI YA MWAKA 2015! PIGENI RUZUKU TU CHADEMA KWA KUTUMIA KESI ZISIZO NA MSINGI
 
Ccm ya zamani wanataka izaliwe upya ndani ya Chadema ili wachukue nchi tena 2020.
 
kama wamefukuzwa sio bora kukaa huku wakisononeka. watafute chama kingine wajiunge nacho maisha ya kisiasa yaendelee. hawajanyang'anywa utanzania wao bali uwanachama. nashauri wafuate ushauri wa mzee lowasa.
 
Lumumba wote akili zao wanalingana. Huwa hawajiongezi hata kwa nukta moja. Wanawafukuza watu uanachana, kisha wanakimbilia kwenye mitandao kuvishauri vyama vingine navyo visikubali kuwachukua! 14thC ignorance....
 
Waje tu wala wasichelewa na waandaliwe mapokezi makubwa tena yawe live na siku hiyo wawaeleze wananchi sababu ya wao kufukuzwa mmoja baada ya mwingine au baadhi wawakilishe wenzao.

Tukio liwe live ikiwezekana zaidi ya channel 3 na wafanye siku ya week-end.
Mkuu waeleze sababu za kufukuzwa zaidi ya ambazo zimetajwa kwamba ni wasaliti kama mlivyosema kwa akina Zitto, Mwampamba, Prof. Kitilya, nk. Au unataka wajiundie sababu nyingine?
Wakaribisheni ili CHADEMA igeuke kuwa CCM B. Ila kwa hakika nakuambia kwamba wakija huko kutakuwa na fukuto kubwa ndani ya CHADEMA. Kuna vijana wanalalama kwamba Chama chao kinatekwa na watu wa kuja ambao siyo kwamba wanaipenda CHADEMA bali wanayapenda matumbo yao zaidi.
Tusubiri tu kama unavyosema Muda ni Mwalimu Mzuri sana, tuupe Muda muda ili utufundishe.
 
Back
Top Bottom