Nimependa hapo penye nyekundu. Tunataka rais anayeweza kufanya maamuzi. Mpaka leo mashirika mengi ya serikali/umma hayana watendaji kwa sababu ya kutofanya maamuzi.
Mtoa mada, subject ni tofauti na ulivyoandika. Ungetoa mada kuwa kasemaje bila kuweka feeling zako halafu ukaacha tuchangie nawe pia uchangie. Ingekuwa vizuri ungenukuu vyote alivyosema na siyo kuchukua tu zile sehemu ambazo wewe unataka kukataa. Weka maelezo yake yote ili ituwezeshe kufanya maamuzi katika kuchangia na siyo utulazimishe wachangia mada au wasomaji kuamini mawazo au kuchangia mawazo yako. Otherwise thread uitume kama mawazo yako au maoni yako kuhusu Lowassa.
Nafikiri wakuu haya ni maoni ya mweka mada na wala sidhani yeye amechukua mawazo ya watu wote humu. Ana uhuru wa kumsifia Lowassa the way anavyotaka ila kwa maoni yangu sidhani kama kuna mtu anayefaa kuwa rais kwa upande wake. Kama anafaa kuwa kiongozi atuambie ni kwa nini nchi ni maskini hadi muda huu na utajiri wa rasilimali tulio nao na atuambie kama viongiozi wamefanya nini kuhakikisha kuwa rasilimali zinatumika kuwaletea maendeleo wananchi na asitupe porojo za makaratasi kuwa uchumi unakua kwa kasi wakati kwa hali halisi umaskini ndo unazidi kuongezeka miongoni mwa watanzania. Wasituletee porojo za kwenye makaratasi ya kukua kwa uchumi wa mifukoni mwao na kufananisha na maisha ya babu na bibi zetu huko vijijini ambako mlo mmoja ni shida na huduma za muhimu kama maji, huduma za afya ni kama anasa kwao