Lowassa aunguruma Bungeni: "Bora kufanya maamuzi na kulaumiwa, kuliko kutofanya!"

Mwamikili

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
417
137
Anaongea Lowassa bungeni.

Anashangiliwa ile mbaya, anasema tujenge reli ya kati, tupanue bandari Tanga, DSM, pesa tunazo, tumejenga UDOM kwa pesa zetu wenyewe

ufisadi.

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, hatimaye amezungumza bungeni miaka mitatu na miezi karibu mitatu tangu kujiuzulu kwake kufuatia kashfa iliyolitikisa taifa ya Richmond. Bw. Lowassa ambaye baada ya kashfa ile alijaribu pole pole kurudi katika mijadala ya taifa kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari alikuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake na wakosoaji wake kuzungumza tena Bungeni na hasa swali kubwa ni jambo gani ambalo angeamua kurudi nalo katika hadhara ya mijadala ya kisiasa nchini.

Bw. Lowassa mmoja wa wanasiasa wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na ambaye anaushawishi mkubwani ndani ya Chama cha Mapinduzi aliamua kuvunja ukimya wake Bungeni akitoa mchango wake kufuatia hotuba ya makadirio ya ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda. WM Pinda aliridhi mikoba na cheo chake baada ya anguko la Lowassa.

Pamoja na kutoa sifa mbalimbali za mafanikio ya serikali ya chama chake Bw. Lowassa aliamua kurusha mashambulizi ya wazi ambayo baadhi ya watu wamechukulia kama mashambulizi yasiyo na utata ya viongozi walioko madarakani. Bw. Lowassa alitumia muda kushambulia utendaji serikali akisema kuwa watendaji serikalini wamekuwa wazito kufanya maamuzi magumu kwa kuhofia kulaumiwa. Hata hivyo hakutoa mfano wa maamuzi magumu ambayo yameshindwa kuchukuliwa kwa hofu ya kulaumiwa.

Kabla kuelekeza mashambulizi hayo, Lowassa alieleza kwa majigambo ya mwanasiasa kuwa yeye alikuwa ni kati ya wabunge walioshinda kwa asilimia kubwa ya kura, akishika nafasi ya nne mbele ya wabunge watatu wa CCM. Katika mchango wake kwenye hotuba hiyo ya bajeti ya Waziri Mkuu, alieleza kuibuka ugonjwa wa kuogopa kufanya maamuzi serikalini na kusisitiza kuwa ni bora kuamua kwa makosa kuliko kutoamua kabisa.

Hata hivyo, wakati akieleza kuwa serikali imekuwa ikikabiliwa na ugonjwa wa kushindwa kufanya maamuzi hakuwa tayari kueleza ugonjwa huo umeanza baada ya yeye kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond au hata wakati huo akiwa katika wadhifa huo. Pamoja na kuzungumzia suala hilo la uthubutu wa kufanya maamuzi Bw. Lowassa alizungumzia pia haja ya kufanya mabadiliko katika ofisi ya Waziri Mkuu akitoa wito kuwa ofisi hiyo ina majukumu mengi sana na kutokana na wingi wake imekuwa haifanyi vizuri. Alitoa pendekezo la kuondoa ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

"Ofisi hii ni kubwa sana, kuna Maafa, Uratibu, Bunge, Uwezeshaji, Uwekezaji na Tamisemi. Tamisemi yenyewe pia imegawanyika katika mambo mengi sana. Nashauri Serikali itafakari kuigawa Ofisi ya Waziri Mkuu ili Tamisemi iwe yenye kujitegemea. Kwa kuwa sehemu katika Ofisi ya Waziri Mkuu inashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, haina budi kupunguziwa mzigo" alisema Bw. Lowassa. Kutokana na kauli hiyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na hasa siasa za ndani ya CCM wanaeleza kuwa ndani ya mchango wa Lowassa bungeni, kwa sehemu kubwa amejielekeza kujibu mapigo ya uamuzi wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kumtaka yeye na wenzake, Rostam Aziz na Andrew Chenge kuachia nyadhifa zao kwenye chama hicho kutokana mwenendo wao unaokipunguzia umaarufu chama hicho mbele ya jamii.

Wachambuzi hao wanahusisha mchango huo wa Lowassa na mwelekeo wa maamuzi ya CCM kwa kugusa baadhi ya hoja zake hasa pale alipobainisha kuwa kwenye Jimbo la Monduli, CCM imepata kura nyingi za urais na yeye kati kura za ubunge amezoa nyingi kiasi kushika nafasi ya nne kitaifa kati ya wabunge wa CCM.

Kwa mujibu wa wachambuzi hao, bado inaaminika kuwa mtazamo wake huo kwamba amekuwa akikibeba CCM kwenye Jimbo lake unatajwa kukinzana na ule wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama ambaye hivi karibuni mbele ya wabunge wa CCM alisisitiza kuwa hakuna mtu maarufu kuliko chama hicho na kwamba chama kitazidi kujijenga kama taasisi wakati wote.

"Tumesikia ujumbe wake ambao tunaamini unalenga kukosoa uamuzi wa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao kama ilivyoamuliwa na NEC, lakini kigezo pekee cha kwamba mwenendo wao umekuwa ukigharimu chama unatazamwa kitaifa na si katika eneo moja dogo, kwa sababu mwenendo wa viongozi wa kitaifa unagusa taswira ya chama kitaifa.

"Kule kwake (Monduli) au Igunga na hata Bariadi inawezekana mbinu fulani kufanikisha ushindi ili baadaye kuunda hoja Fulani mahsusi ya kujijenga zaidi kisiasa, lakini ukweli halisi kutoka kwenye jamii kitaifa, inaibua mtazamo tofauti kabisa na huo. Utakumbuka hata wakati anajiuzulu uwaziri mkuu, nchi nzima ilishangilia lakini kule Monduli waliandaliwa magari na watu maalumu kwa ajili ya kumpokea kishujaa. Ujanja huu ndiyo CCM hauupi nafasi tena, tunataka kuwa realistic na si kubuni mbinu za ujanja ujanja," alisema mmoja wa viongozi wa sasa wa CCM.

Baadhi ya wananchi waliotoa michango yao mbalimbali katika mitandao ya kijamii wameonekana kuvutiwa na kauli ya Lowassa juu ya ukosefu wa ujasiri wa maamuzi wakipongeza uamuzi wake kusema kile ambacho baadhi ya watu katika jamii wanaamini kuwa ni tatizo. "kanifurahisha sana pale aliposema watu wanaogopa kutoa maamuz, hope message sent" amesema Sam Kabugo kwenye mtandao wa Facebook.

Wananchi wengine hata hivyo wamechukulia uamuzi wa Lowassa kuzungumza kwa kuimwagia sifa CCM akiyapa shavu mafanikio ya miaka 50 ambayo "kila mtu anajua, na dunia inajua" kuwa ni mbinu ya kujaribu kutafuta huruma ndani ya CCM lakini wakati huo huo kuzungumzia kwake suala la uamuzi kuwa ni kujiandaa kwa maamuzi yanayokuja hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.

Hata hivyo tetesi ambazo FikraPevu haijaweza kuzithibitisha zimedai kuwa masaa machache kabla ya hotuba yake kulikuwa na kampeni ya chini kwa chini ya kupata support (washangiliaji) kutoka kwa baadhi ya wabunge hasa kutoka viti maalum na wale wa Zanzibar. Hata hivyo haijajulikana hasahasa matokeo ya kurudi kwake katika mijadala ya siasa kuna maana gani kwani hakugusia moja kwa moja tatizo kubwa zaidi ambalo linakabili taifa, yaani ufisadi.

Waandishi Wetu, Dodoma
 
Thread za JF kama hizi zinajaza seva tu..!
Sijui muanzishaji anakua amedhamiria nini?
Kazi bado tunayo humu
 
yap, ila pongezi nyingi mno, na kujigamba na asilimia kubwa ya kura alizopata. tusubiri kama ataongelea ufisadi
 
Jamani.

Hata wao bado ni wabunge, na wanawawakilishi wananchi wao kama wabunge zetu walivyo.

Wahurumie tu kama c.c.m inavyowahurumia.

Asante
 
Aache unafiki ndio waliotufikisha kwenye uchovu huu.
Wakapumzike sasa muda wao ulishaisha.
 
Hana jipya avue Gamba bana alikuwa ofisi hiyo mbona haku yafanya hayo anayo ya sema bana ufisadi Uraisi hapatiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Anadai Fedha tunazo Kwani wamerudisha walizo chota nini!!!
 
anashangiliwa ile mbaya, huyu jamaa anafaa kuwa president, tujenge reli ya kati, tupanue bandari tanga, dsm pesa tunazo, tumejenga udom kwa pesa zetu wenyewe
 
Washangaliaji wanafanya hivyo kwa KEBEHI au kwa dhat??????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mbona udom inawashinda????wanashindwa hata kuwapa hela za field.....hela wanazo wao ndo maana anasema hela tunazooooo......she*z#
anashangiliwa ile mbaya, huyu jamaa anafaa kuwa president, tujenge reli ya kati, tupanue bandari tanga, dsm pesa tunazo, tumejenga udom kwa pesa zetu wenyewe
 
anashangiliwa ile mbaya, huyu jamaa anafaa kuwa president, tujenge reli ya kati, tupanue bandari tanga, dsm pesa tunazo, tumejenga udom kwa pesa zetu wenyewe
hahahaha hivi kuna nani asiejua haya? siasa bana
 
tutoe maamuzi anasema bora uhukumiwe kwa kwa kutoa maamuzi si kwa kuogopa kutoa maamuzi, mawaziri wamekuwa waoga wa kutoa maamuzi toeni maamuzi jamani, kamaliza hotuba yake kwa kuunga mkono na alipomaliza ameshangiliwa na bunge zima mpaka wakamuonesha na sita akipiga meza!! this is funny politics!
 
aaah ni ccm tena hawa wanajiita magamba kwanini mnaokota magamba tena
 
Back
Top Bottom