Lowassa aunguruma Bungeni: "Bora kufanya maamuzi na kulaumiwa, kuliko kutofanya!"

Kweli fisadi ni fisadi yaani kawanunueni mnampigia kampaign kwa nguvu zote...
Hakuna jipy jf sasa hivi ni lowasa kakohoa ,lowasa kacheka, lowasa kanisani ,lowasa kijiweni !
 
Lowassa amemaliza kuchangia hotuba ya Waziri mkuu kwa mbwembwe za kusifia mafanikio ya CC-Magamba kwa miaka 50. Amejidai kusema kwamba tuna maendeleo makubwa sana na hayo ni mafanikio ya Magamba na mtu asiwabeze. Amemshauri Jk kutoogopa kufanya maamuzi mazito kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosea kuliko kutofanya kabisa.Ameendeleza porojo za uchumi kuwa unakuwa kuliko nchi nyingi duniani lakini hajaeleza kwa nini mtu wa kawaida kijijini anazidi kuwa maskini. ameshindwa kujua kwamba uchumi unapokua hau-trickle down bali unakingwa juju kwa juu na mafisadi akiwemo yeye kiasi kwamba haufiki kwa bibi na babu zetu kule vijijini.Anazungumzia kuwa barabara zimejengwa nyingi na madarasa bila kueleza hayo madarasa yamezaa vitu gani. Anaangalia quantity bila kuelezea quality kuonyesha kuwa bado ile tabia ya uVIVU WA KUFIKIRI NA KUTOKUWA REALIST KWA VIONGOZI WETU KUNA ENDELEA.Ameni fanya hata kufuta lile wazo kuwa anaweza kufikiriwa kuwa the next presidee 2015 kwani bado ana magamba mengi kuliko wanamagamba wenyewe. Anaonyesha hata kero za wananchi hazijui tena halafu anataka urais sijui kwa ajili ya kitu gani. Nilifikiri pia atakuja na kitu tofauti na Magamba kumbe yake yeye ni makubwa zaidi.
Nimependa hapo penye nyekundu. Tunataka rais anayeweza kufanya maamuzi. Mpaka leo mashirika mengi ya serikali/umma hayana watendaji kwa sababu ya kutofanya maamuzi.
Mtoa mada, subject ni tofauti na ulivyoandika. Ungetoa mada kuwa kasemaje bila kuweka feeling zako halafu ukaacha tuchangie nawe pia uchangie. Ingekuwa vizuri ungenukuu vyote alivyosema na siyo kuchukua tu zile sehemu ambazo wewe unataka kukataa. Weka maelezo yake yote ili ituwezeshe kufanya maamuzi katika kuchangia na siyo utulazimishe wachangia mada au wasomaji kuamini mawazo au kuchangia mawazo yako. Otherwise thread uitume kama mawazo yako au maoni yako kuhusu Lowassa.
 
Whos is Lowassa katika hii nchi? si mwizi tu kama kikwete sasa mnamsifia nini? Jamani watanzania tusikubalikuyumbishwa na haya majambazi yanayotutawala kikunguvu lazima tuwapigeni chini
 
tanzania inajua na dunia nzima inajua mimi lowassa nina helaa
 
My opinion EL amepoteza uhalali wa kuzungumzia maendeleo ya nchi kwa sababu tunaamini kwamba anatengeneza mchongo ili avute cha juu Kama alivyofanya kwenye mchakato wa mikataba ya Buzwagi na Richmund. Halafu wakati anaongea bungeni leo karibu nchi nzima haina umeme wakati tatizo la umeme liaanzia na maamuzi yake.... Du watu wengine hawana Aibu.
 
Jamani hajaongea cha maana ni yale yale mambo ya Jumla jumla kama vile kwenye kampeni. Hotuba yake hata mtoto wa form 4 angeweza kuitoa ni kama alikuwa anataka kuwahadaa wabunge kwa maneno ya kuisifia CCM. Hotuba ya Mh. Mbowe na, wabunge wengi wa CDM imeipita ya Lowassa kwa mbali may be a 10000 times.
 
Hilo neno la Amani na Utulivu ni la kishenzi sn. Huo ndio mtaji wao wanaowadanganyia wazungu na kupewa hela wanazozipiga ufisadi. Mi nawashangaa sn Wazungu, pamoja na akili na ugunduzi mwingi walio nao wanashindwaje kugundua non-perfomance ya hii serikali, matokeo wanaishia kuisifu kuwa inapiga hatua nzuri sana ya uchumi!! Mi nadhan madawa wana yoenda kunywa Bagamoyo yanawalevya hadi wazungu...kweeee!
 
Kajipa shavu kiaina kwa kufagilia shule za kata na mradi wa maji wa ziwa victoria vitu ambavyo kimsingi alivisimamia, kapeleka dongo kiaina nadhani kwa mkulu na kwa chama chake kwa kuogopa kufanya maamuzi na nilichokiona kikubwa jamaa ana nguvu kubwa kisiasa ndani ya CCM si saizi ya kupewa mtu kama Nape ammalize.
 
Anaongea Lowassa bungeni.Anashangiliwa ile mbaya, anasema tujenge reli ya kati, tupanue bandari Tanga, DSM, pesa tunazo, tumejenga UDOM kwa pesa zetu wenyewe
Nasema na ntaendelea kusema na sitakoma kusema Lowasa hafai kuwa kiongozi wa taifa hili.Lowasa alipokuwa waziri mkuu alikuwa hafahamu ya kuwa wanapaswa kufanya maamuzi magumu? Nasema Lowasa hafai. Lowasa ulikuwa hufahamu kuna ulazima wa kujenga reli kipindi ulichokuwa madarakani? Lowasa acha unafiki usitafute kura za huruma kwa watanzania wakati uliwasaliti vilivyo na hizo hela unazosema zipo mbona mlizichukua na kuzikalia? Aibu aibu aibu tupu kwa Lowasa hufai wala hutofaa kuwa Rais wataifa hili.
 
kwa kifupi ni kwamba lowasa hatoki ccm na ana nguvu.......huyu jamaa ni mchapa kazi tatizo lake ni wizi .....tofauti sana na mzee wa kulia lia
 
Huyu jamaa kweli ni lobbiest anasema pesa ipo mbona bajeti tunachangiwa na hao wazungu????.Mpaka imefikia kipindi kwa ajiri ya ufisadi wake wazungu wamekataa kuchangia bajeti na serikali inakopa ili kulipa mishahara hizo pesa anazosema zipo ziko wapi????.Serikali imeshindwa hata kutoa pesa ili TTCL ipige hatua zaidi hata kuidhamini ili ikope na kuendesha biashara kisasa imeshindwa hizo pesa anazosema zipo ziko wapi?????.
 
bila shaka safari ya lowasa kule naigeri imeanza kuzaa matunda. Kwa kweli wabunge wa ccm wameanza kumkubari tunako elekea huenda asiwe ghamba tena na gamba labda awe mkuu mwenyewe, na losatam atakuwa ameenda huko huko naigeria make haonekani mjengoni.
Naigeria si mchezo ndo mwisho wa kila kitu.
 
Wabunge wamemshangilia sana baada ya kumaliza kuchangia sasa sijui ni kwa kumkebehi au ndio wale waliopo kwenye Posho zake. Maana Jamaa anakampeni kali sana ya 2015.
 
Back
Top Bottom