Lowassa aunguruma Bungeni: "Bora kufanya maamuzi na kulaumiwa, kuliko kutofanya!"

Lowassa has 9 lives! Wabunge wameshangilia mbaya! ......watanzania wanajua na dunia inajua.

I have to admit, he has scored some points with respect to 2015. Huyu jamaa hawawezi kumvua gamba.
 
Duh! Si nilisikia kuwa yeye ndiye anayeongoza kwa utoro mjengoni?
 
Anasema ofisi ya PM ni kubwa na muundo wake uangaliwe upya! Unasababisha urasimu. Miaka 50 ccm imefanya mema yasibezwe! Watanzania wanajua na dunia inajua. Reli ya kati ijengwe upya, bandari za tanga na mtwara nazo zijengwe. Tukinuia tunaweza na fedha zipo. Tatizo analosema ni ugonjwa wa kutotoa maamuzi! Anasema ni heri ulaumiwe kwa kutoa maamuzi kuliko kulaumiwa kwa kutotoa maamuzi. Anashangiliwa kwelikweliii
 
tutoe maamuzi anasema bora uhukumiwe kwa kwa kutoa maamuzi si kwa kuogopa kutoa maamuzi, mawaziri wamekuwa waoga wa kutoa maamuzi toeni maamuzi jamani, kamaliza hotuba yake kwa kuunga mkono na alipomaliza ameshangiliwa na bunge zima mpaka wakamuonesha na sita akipiga meza!! this is funny politics!


Kulia na kucheka zote ni kelele
 
Huyu jamaa kumbe ni muhimu sanaa kwa siasa za CCM na Tanzaniaa inonekanaa!!!
 
Watanzania wanajua, Dunia nzima inajua!!

Serikali iliyopo madarakani thubutu kuliko kaa mkiogopa mtalaumiwa, hata mkikopa kopeni kwani hata serikali ya Marekani inaongoza kwa kukopa iweje Tanzania??

Lowassa kasema kilichopo moyoni kwani kaona Serikali ya CCM ni wababaishaji kamsema waziri mkuu live kwakushindwa kutekeleza majukumu yake na kamkumbusha aliyoyafanya akiwa waziri mkuu.

Ukweli leo Lowassa kanifurahisha tugange yajayo Lowassa unafaa, mapungufu ni ya kibinadamu.
 
May be ameshatubu dhambi zake zote na Mungu amemsamehe... maana Mungu hana upendeleo so may be Mungu kampa kibali kwa watz.
lets wait and see the end to his ambitions.
 
nimemsikiliza jamaa ukweli ni kwamba kaongea pumba tupu.. labda alipoongea kuhusu watu kuogopa kufanya maamuzi ndio nimempa nukta kidogo mengine yote ni pumba na wabunge wa ccm wamepiga meza utafikiri mtanzania kapata ukombozi... stupid politics:music:
 
Jamani umeme ni shida maeneo mengi ya Tanzania, kama waziri mkuu kivuli Mh.Mbowe alishapewa nafasi ya kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu tunaomba angalau kwa mktasari kile alichoongea kuhusiana hiyo Hotuba ya Waziri Mkuu.
 
Mkuu hii habari iko nusunusu haijakamilika, kutokana na tatizo la umeme watu wengi hawana habari kinachoendelea nchini, kwahiyo unapopost taarifa jaribu kuikamilisha taarifa pasi na kuhitaji ufafanuzi.
 
Lowassa amemaliza kuchangia hotuba ya Waziri mkuu kwa mbwembwe za kusifia mafanikio ya CC-Magamba kwa miaka 50. Amejidai kusema kwamba tuna maendeleo makubwa sana na hayo ni mafanikio ya Magamba na mtu asiwabeze. Amemshauri Jk kutoogopa kufanya maamuzi mazito kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosea kuliko kutofanya kabisa.Ameendeleza porojo za uchumi kuwa unakuwa kuliko nchi nyingi duniani lakini hajaeleza kwa nini mtu wa kawaida kijijini anazidi kuwa maskini. ameshindwa kujua kwamba uchumi unapokua hau-trickle down bali unakingwa juju kwa juu na mafisadi akiwemo yeye kiasi kwamba haufiki kwa bibi na babu zetu kule vijijini.Anazungumzia kuwa barabara zimejengwa nyingi na madarasa bila kueleza hayo madarasa yamezaa vitu gani. Anaangalia quantity bila kuelezea quality kuonyesha kuwa bado ile tabia ya uVIVU WA KUFIKIRI NA KUTOKUWA REALIST KWA VIONGOZI WETU KUNA ENDELEA.Ameni fanya hata kufuta lile wazo kuwa anaweza kufikiriwa kuwa the next presidee 2015 kwani bado ana magamba mengi kuliko wanamagamba wenyewe. Anaonyesha hata kero za wananchi hazijui tena halafu anataka urais sijui kwa ajili ya kitu gani. Nilifikiri pia atakuja na kitu tofauti na Magamba kumbe yake yeye ni makubwa zaidi.
 
ameniudhi kusema mafanikio ya miaka 50 ya uhuru wetu kama mtu akikuuliza sema "amani na utulivu"

amani wakati matatizo lukuki, ukiwa na njaa utakuwa na amani kichwani?
 
Back
Top Bottom