Lowassa atakiwa kuripoti tena Polisi mwezi August

Lowassa atakiwa kuripoti tena Polisi mwezi August

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Jeshi la Polisi limemtaka waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuendelea kuwa chini ya dhamana ya polisi na anatakiwa kuripoti tena bila kukosa tarehe 14/8 kwa madai uchunguzi unaendelea

Mhe. Lowassa alikuwa ameenda kuripoti leo kama alivyotakiwa wiki iliyopita

kabla ya Lowassa kuwasili katika viwanja hivyo vya makao makuu ulinzi uliimarishwa kila kona huku kila gari iliyokuwa inafika hapo kukaguliwa na watu kufukuzwa ovyo wakiwemo waandishi wa habari.

ulinzi uliondolewana kurejea katika hali ya kawaida na watu kuruhusiwa kuondoka mara waziri mkuu huyo mstaafu alipoondoka.
 
Wiziri Mkuu wa zamani na Mgombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Edward Lowassa leo aliwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwaajili ya kuendelea na mahojiano na Ofisi ya DCI kama alivyotakiwa kufanya hivyo.

Lakini Mzee Lowassa akiwa ameambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa mara baada ya kufika katika viunga vya ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ofisi ya DCI amemtaka arudi nyumbani kwakuwa Upelelezi wa tuhuma zake za Uchochezi bado haujakamilika.

=======

SAKATA LA LOWASSA KUITWA POLISI- UPDATES.

Baada ya kutakiwa ku-report Police kuhusiana na kinachosemekana ni matamshi ya kichochezi anayadaiwa kuyatamka Mh. Edward Lowassa katika Iftar iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara; na baada ya kuandikisha maelezo kuhusiana na tuhuma hizo, Mh. Lowassa awali alitakiwa ku-report ofice ya DCI mnamo 13th July 2017 na baadaye leo 20th July 2017.
Leo baada ya ku-report kama ilivyoamriwa na ofisi ya DCI, maelekezo yaliyotolewa ni kwamba bado Jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi/Upelelezi wa suala husika na baada ya wiki 3 hivi tutapata maelekezo zaidi kuhusiana na nini kinafuata baada ya ukamilishaji wa taratibu husika.
Tutawapa taarifa zaidi kadri zitakavyoendelea kujitokeza .

Imetolewa na CHADEMA Media.
 
Tatizo si yanayoendelea tu, ila tuelekeako pia. Kama ni mapenzi yako eeh Mungu, kikombe icho kituepuke.
 
bado miezi mitano mwaka kukatika, ngoja tuone labda izi mambo ndo catalysts za viwanda
Viwanda vya Jpm hivyo.huwa nacheka sana mbinu zetu za kuweka viwanda ukilinganisha na njia walizopitia wenzetu walioendelea hadi nabakia kucheka tu
 
!
!
Sheria unasemaje kuhusu hizi Nenda rudi? Maana naona kama ni kumkomoa vile
Hapo wanamtafutia timing, siku akikataa kwenda tu wanamkamata kwa kosa la kutotii wito halali. Polisi wanafunua udhaifu wao na kutuonyesha Watanzania jinsi jeshi la polisi lilivyo dhaifu ktk utendaji wake. Wanaposema upelelezi haujakamilika huwa najiuliza huo upelelezi unafuatwa sayari gani.

Vv
 
Aisee sasa si bora kama wanamshtaki wamshtaki ijulikane kuliko kumtesa baba wa watu
 
Wiziri Mkuu wa zamani na Mgombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Edward Lowassa leo aliwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwaajili ya kuendelea na mahojiano na Ofisi ya DCI kama alivyotakiwa kufanya hivyo.

Lakini Mzee Lowassa akiwa ameambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa mara baada ya kufika katika viunga vya ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ofisi ya DCI amemtaka arudi nyumbani kwakuwa Upelelezi wa tuhuma zake za Uchochezi bado haujakamilika.

The Great Adv. Hon. Tundu A. M. Lissu alilitibua deal lao siku ya press hivyo hawawezi kumpeleka popote Mh. Eddo! Wamekwishajua kuwa issue imefika kwa jemedali Lissu hata wakimpeleka Eddo Mahakamani wanangukia pua na matako....
 
Back
Top Bottom