Muacheni afanye mazoezi. Hamjui mtu ukikaa sehemu mmoja muda mrefu ni sawa na kuvuta pakiti ishirini za sigara kali kwa siku? Kumzuia kufanya mazoezi unakuwa humtakii mema.!
!
Sheria unasemaje kuhusu hizi Nenda rudi? Maana naona kama ni kumkomoa vile
daah... inatia uchungu kuona watu wanasumbuliwa bila sababu ya msingi, basi wamfunge tu ili nyongo zao zitulie!
Jeshi la Polisi limemtaka waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuendelea kuwa chini ya dhamana ya polisi na anatakiwa kuripoti tena bila kukosa tarehe 14/8 kwa madai uchunguzi unaendelea. Mhe. Lowassa alikuwa ameenda kuripoti leo kama alivyotakiwa wiki iliyopita
ccm wanafanya mambo kizamani sana
Unajua nini wewe kinachoendelea maskini mpendwa wa Mungu tu!Viwanda vya Jpm hivyo.huwa nacheka sana mbinu zetu za kuweka viwanda ukilinganisha na njia walizopitia wenzetu walioendelea hadi nabakia kucheka tu
Ni kweli, tunakoelekea si shwari. Viogozi wanakurupuka na kufanya mambo kwa nidhamu ya woga. Mahakama na vyombo vya habari havipo huru tena.Tatizo si yanayoendelea tu, ila tuelekeako pia. Kama ni mapenzi yako eeh Mungu, kikombe icho kituepuke.
Someni article iliyopo The Economist, How powerful people use criminal defamation laws to silence their critics. Mtaelewa nini kinachoendeleaHivi hili suala bado ni kauli ya Lowassa ya Masheikh? Kama ndivyo hii ni harassment ya makusudi na by design, wala sio utaratibu wa kipolisi. Tangu lini mtu unaenda kuripoti polisi wakiwa katika uchunguzi? Polisi wanatakiwa wachunguze, wakimaliza waamue kama utakuwa arrested na kufikishwa mahakamani au la. Kwanza unachunguza nini kama suala ni ile kauli, si iko wazi inajulikana?
Yaani serikali hii ya CCM, ikiongozwa na Magufuli, imefilisika kabisa kimawazo juu ya kukabiliana na ushindani wa kisiasa. Inatia aibu na kichefuchefu.
Na mimi nasema hapa wazi, wafikisheni Masheikh mahakamani au waachieni. Mnatoa mifano ya Guantanamo Bay ya Marekani, kwani nani kawaambia Marekani ndio kigezo cha jinsi tutakavyoendesha mambo yetu Tanzania? Kama mnawapenda Marekani kiasi hicho mbona ushoga hamuukubali hadharani mnaendelea kujificha ficha?