Lowassa ataka mfumo wa elimu ufumuliwe

Lowassa ataka mfumo wa elimu ufumuliwe

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,745
LEO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI:WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema kuna haja ya kutathmini upya mfumo wa elimu nchini, ili kuona kama bado unafaa au la.Alisema hatua hiyo inapaswa kufanywa sasa kabla mambo hayajaharibika zaidi na kwamba anaamini kuwa tangu mfumo uliopowekwe enzi za Mwalimu Nyerere, kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.

Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ofisini kwake jijini Dar es slaam.''Mimi nasema kuwa sasa wakati umefika kama taifa. kuunda tume ya elimu, ili kuangalia na kupitia mfumo wote wa elimu, kuangalia mitalaa yetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, kuangalia ubora wa elimu hiyo, vitabu gani vitumike, maslahi ya walimu, yaani kwa ujumla tuangalie upya kuhusu mfumo wa elimu yetu.''alisisitiza Lowassa.Lowassa alipendekeza kuundwa kwa tume ya elimu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ili kwenda na wakati. "Tume hiyo iundwe kuchunguza, kutathmini na kuona, endapo mfumo wa elimu wa sasa unaendana na wakati,"Lowassa alisema nchi zote zilizoendelea duniani, zimekuwa zikifanya hivyo."Marekani hivi sasa kuna mchakato wa kuangalia elimu inayotolewa kama inaendana na changamoto za karne ya 21," alisema.Kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kwamba mitalaa ya elimu nchini, haimwandai mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha ya karne hii ikiwa ni pamoja na kujiajiri.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa sana katika sekta ya elimu, hususan awamu hii ya nne ambayo kwa mafanikio makubwa, imeweza kujenga shule za sekondari katika kata zote nchini.Katika mkutano wake mkuu wa nane hivi karibuni mjini Dodoma, CCM ilitoa mapendekezo kadhaa miongoni mwao likiwa la kuboresha elimu nchini.''Mimi nilipata bahati ya kuongoza juhudi hizo za Serikali kwa mafanikio makubwa kujenga shule hizo, lakini mafanikio hayo yamekuja na changamoto zake''alisema.Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafanikio hayo ni ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo, uhaba wa walimu na vitendea kazi vikiwemo vitabu na masilahi kwa walimu.

Alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na wasomi waliobobea ambao wanaweza kazi hii ya kuangalia mitalaa inayotumika ili kuona kama inakidhi haja na matakwa ya karne ya sasa.My Take- Hivi Lowassa anapochukua muda mwingi kuongea haya na vyombo vya Habari ni sehemu sahihi?.

Lowassa ni Mbunge kama wabunge wengine kwa nini haya anayoyasema asingeyaongea Bungeni ambayo ni sehemu muafaka na Bajeti ya serikali ndiko inakopitia?
 
Na kwa kuongezea anachosema Lowasa ni kwamba anakubaliana na sera/Ilani ya elimu ya vyama pinzani kama CHADEMA wakati wa uchaguzi wa 2010.

Ni vema sasa ccm wakubali kwamba hoja za wapinzani wao zilikuwa na mashiko wakati ule wa uchaguzi 2010.
Vyama vyote vinapigania kuijenga Tanzania , ni vya watanzania na viko Tanzanaia, Tanzania ni yetu sote... na kama CCM wanaanza mchezo wa ku-copy na ku-pasty sera za vyama vingine inabidi pia wa-acknowledge source vinginevyo itakuwa ni plagiarism ambayo hairuhusi popote pale duniani bila ktoa chanzo.

Haiwaondolei CCM U-CCM wao kama wakikili kwamba hoja zao kwa sasa ni copy aand pasty kutoka upinzani haijalishi kama ni CHADEMA CUF au za akina Dovutwa...
 
Viongozi wa TZ ni wa ajabu sana!

(1)LOWASA-Alikuwa PM lkn HAKUTHUBUTU kuyasema mapungufu ya mfumo wetu wa elimu na KUYAPATIA UFUMBUZI alipokuwa madarakani!

(2)SUMAYE-Alikuwa PM na ndiye aliitumbukiza nchi kwenye rushwa ya uchaguzi alipoongoza Bunge litunge sheria ya TAKRIMA lkn sasa analia kuwa Mama Nagu alimuangusha kwa rushwa amesahau kuwa ni YY aliyeiasisi!

(3)Mzee Mangula nae juzi kasema atapambana na rushwa lkn KASAHAU kuwa ndiye yeye aliipamba kwa kutamka kuwa"mgombea kuwahudumia wapiga kura KABLA ya kupiga kupiga kura sio dhambi"lkn baadae akalalamika sana alipoangushwa kwa rushwa na Jah People kule Iringa!

INA MAANA VIONGOZI WETU WANAONA MATATIZO HADI WAKITOKA MADARAKANI?Lowassa na wenzake ni wa kupuuzwa na HAWANA JIPYA!
 
Tunakoelekea waTZ siyo kuzuri. Hivi kweli mtu aogope kutoa dukuduku lake moyoni au mawazo yake ya namna ya kuboresha jambo fulani eti kwa sababu tu jambo analoongelea alishindwa kulitekeleza wakati alipokuwa na fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi!!!??? Sidhani kama hiyo inaketa mantiki. In fact, kuna mambo ambayo ukiwa nje unayaona vizuri kuliko ukiwa ndani. Kwa hiyo, kwa kuwa nchi inahitaji mawazo ya watu katika kuijenga, lazima turuhusu kila mtu awe na uhuru wa kuchangia mawazo yake whether alikuwa au hajawahi kuwa kiongozi.
 
sawa ukiwa nje unaona mambo vizuri... sasa kwa nini basi usikiri kwamba hukuyaona hayo unayoyazungumzia sasa wakati ule au unaogopa kwamba utaambiwa hauna vision? Pia kukubali au kuwapa credit wale walio kuwa na vision wakati ule walipo liona tatizo sio kosa la jinai... Jamii ya kitanzania imestaarabuka na itakuelewa kwa kukili mapungu yako .

si jambo jema kuwa mnafki kujifanya sasa ndo unaamka usingizini kwa kusema yale yaliyo semwa na mpinzani wako wakati ule na wewe au chama chako kuyapinga na sasa ndo unakuja endeleza ngonjela zile zile ulizozipinga ambazo wenzako walikwambia toka awali na wewe ukawa hutaki kuambilika ni kupinga tu na kuwa mgumu kuliko jiwe ambalo likibonyezwa laweza hubonyezeka......

Tuwe na tujenge utamaduni wa kukili mapungufu ile tujifunze toka kwa wale wenye mawazo tofauti yenye manufaa kwa nchi yetu Tanzania...kuliko kuwa ngangali hata pale tusipokuwa na vision...
 
Tunakoelekea waTZ siyo kuzuri. Hivi kweli mtu aogope kutoa dukuduku lake moyoni au mawazo yake ya namna ya kuboresha jambo fulani eti kwa sababu tu jambo analoongelea alishindwa kulitekeleza wakati alipokuwa na fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi!!!??? Sidhani kama hiyo inaketa mantiki. In fact, kuna mambo ambayo ukiwa nje unayaona vizuri kuliko ukiwa ndani. Kwa hiyo, kwa kuwa nchi inahitaji mawazo ya watu katika kuijenga, lazima turuhusu kila mtu awe na uhuru wa kuchangia mawazo yake whether alikuwa au hajawahi kuwa kiongozi.

Ninachopinga kwa LOWASSA ni kuwa kila mtz alimuambia kuwa hizo shule zake za kata anazozianzisha bila maandalizi ni janga la kitaifa lkn yy akadharau ushauri huu!Leo hii yupo nje ya system analalamika mno kasahau ni yy (Lowassa )aliyetuletea matatizo haya!

Hapa nilipo kuna shule ya sekondari ya kata ni aibu,ina walimu 2!Lowassa ndiye alituanzishia shule hizi za hovyohovyo!

APUUZWE tu!
 
Lowasa anajinadi kwa ajili ya2015.
sasa anadai Tume ya Elimu iundwe kutathmini ubora wa elimu.
kuna haja gani ya kuundwa tume ya elimu wakati tuna Wizara nzima ya Elimu.
systems za serikali ya CCM hazijui wajibu wake, yaani kila kitu kiundiwe tume?
 
Tunakoelekea waTZ siyo kuzuri. Hivi kweli mtu aogope kutoa dukuduku lake moyoni au mawazo yake ya namna ya kuboresha jambo fulani eti kwa sababu tu jambo analoongelea alishindwa kulitekeleza wakati alipokuwa na fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi!!!??? Sidhani kama hiyo inaketa mantiki. In fact, kuna mambo ambayo ukiwa nje unayaona vizuri kuliko ukiwa ndani. Kwa hiyo, kwa kuwa nchi inahitaji mawazo ya watu katika kuijenga, lazima turuhusu kila mtu awe na uhuru wa kuchangia mawazo yake whether alikuwa au hajawahi kuwa kiongozi.
Huyu huyu Lowassa angekuwa bado serikalini angetetea kwa nguvu zake zote utendaji wa serikali. Ndiye aliyeanzisha shule za kata, ni lini amegundua kuwa kuna haja ya kuwa na waalimu bora kabla ya kuanzisha hizo shule? He is part of the problem, he cannot be part of the solution.
 
Malafyale nakuunga mkono kwa 101% Lowassa na wanafiki wenzake wa CCM wanalazimisha huruma toka kwa WaTz. Lowasa Bungeni anafunika mdomo wake mpaka unatoa uvundo kwa kutochangia hoja na mamvi yake kichwani. Akitoka nje ndipo huita wana habari na kutamka utumbo wake. CCM most of them if not all of them ni manyang'au hawafai kuongoza Tz TENA!
 
Unaaafiki unaaafiki mtupu. Alipokuwa madarakani mbona hakuufumua? Ina maana anaona mwanga baada ya kuwa nje ya serikali au ni kutafuta sifa uchwara ili atakapogombea urais ambao hata hivyo hatapata akubalike? Kama Lowassa ana maanisha asemacho basi arejeshe pesa yetu ya Richmond ndipo aseme hayo anayosema. Hivi Lowassa hajui kuwa amehujumu elimu kwa kusababisha mgao wa umeme ambapo wazazi hulanguliwa umeme huku watoto na wanafunzi wenginei wakikosa mwanga kujisomea na kujiandaa kwa ajili ya shule. Lowassa go tell it the birds and shame on you!
LEO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI:WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema kuna haja ya kutathmini upya mfumo wa elimu nchini, ili kuona kama bado unafaa au la.Alisema hatua hiyo inapaswa kufanywa sasa kabla mambo hayajaharibika zaidi na kwamba anaamini kuwa tangu mfumo uliopowekwe enzi za Mwalimu Nyerere, kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ofisini kwake jijini Dar es slaam.''Mimi nasema kuwa sasa wakati umefika kama taifa. kuunda tume ya elimu, ili kuangalia na kupitia mfumo wote wa elimu, kuangalia mitalaa yetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, kuangalia ubora wa elimu hiyo, vitabu gani vitumike, maslahi ya walimu, yaani kwa ujumla tuangalie upya kuhusu mfumo wa elimu yetu.''alisisitiza Lowassa.Lowassa alipendekeza kuundwa kwa tume ya elimu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ili kwenda na wakati. "Tume hiyo iundwe kuchunguza, kutathmini na kuona, endapo mfumo wa elimu wa sasa unaendana na wakati,"Lowassa alisema nchi zote zilizoendelea duniani, zimekuwa zikifanya hivyo."Marekani hivi sasa kuna mchakato wa kuangalia elimu inayotolewa kama inaendana na changamoto za karne ya 21," alisema.Kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kwamba mitalaa ya elimu nchini, haimwandai mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha ya karne hii ikiwa ni pamoja na kujiajiri.Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa sana katika sekta ya elimu, hususan awamu hii ya nne ambayo kwa mafanikio makubwa, imeweza kujenga shule za sekondari katika kata zote nchini.Katika mkutano wake mkuu wa nane hivi karibuni mjini Dodoma, CCM ilitoa mapendekezo kadhaa miongoni mwao likiwa la kuboresha elimu nchini.''Mimi nilipata bahati ya kuongoza juhudi hizo za Serikali kwa mafanikio makubwa kujenga shule hizo, lakini mafanikio hayo yamekuja na changamoto zake''alisema.Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafanikio hayo ni ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo, uhaba wa walimu na vitendea kazi vikiwemo vitabu na masilahi kwa walimu. Alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na wasomi waliobobea ambao wanaweza kazi hii ya kuangalia mitalaa inayotumika ili kuona kama inakidhi haja na matakwa ya karne ya sasa.My Take- Hivi Lowassa anapochukua muda mwingi kuongea haya na vyombo vya Habari ni sehemu sahihi?. Lowassa ni Mbunge kama wabunge wengine kwa nini haya anayoyasema asingeyaongea Bungeni ambayo ni sehemu muafaka na Bajeti ya serikali ndiko inakopitia?
 
LEO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI:WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema kuna haja ya kutathmini upya mfumo wa elimu nchini, ili kuona kama bado unafaa au la.

Alisema hatua hiyo inapaswa kufanywa sasa kabla mambo hayajaharibika zaidi na kwamba anaamini kuwa tangu mfumo uliopowekwe enzi za Mwalimu Nyerere, kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ofisini kwake jijini Dar es slaam.

''Mimi nasema kuwa sasa wakati umefika kama taifa. kuunda tume ya elimu, ili kuangalia na kupitia mfumo wote wa elimu, kuangalia mitalaa yetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, kuangalia ubora wa elimu hiyo, vitabu gani vitumike, maslahi ya walimu, yaani kwa ujumla tuangalie upya kuhusu mfumo wa elimu yetu.''alisisitiza Lowassa.

Lowassa alipendekeza kuundwa kwa tume ya elimu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ili kwenda na wakati. "Tume hiyo iundwe kuchunguza, kutathmini na kuona, endapo mfumo wa elimu wa sasa unaendana na wakati,"Lowassa alisema nchi zote zilizoendelea duniani, zimekuwa zikifanya hivyo."Marekani hivi sasa kuna mchakato wa kuangalia elimu inayotolewa kama inaendana na changamoto za karne ya 21," alisema.

Kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kwamba mitalaa ya elimu nchini, haimwandai mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha ya karne hii ikiwa ni pamoja na kujiajiri.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa sana katika sekta ya elimu, hususan awamu hii ya nne ambayo kwa mafanikio makubwa, imeweza kujenga shule za sekondari katika kata zote nchini.

Katika mkutano wake mkuu wa nane hivi karibuni mjini Dodoma, CCM ilitoa mapendekezo kadhaa miongoni mwao likiwa la kuboresha elimu nchini.''Mimi nilipata bahati ya kuongoza juhudi hizo za Serikali kwa mafanikio makubwa kujenga shule hizo, lakini mafanikio hayo yamekuja na changamoto zake''alisema.

Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafanikio hayo ni ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo, uhaba wa walimu na vitendea kazi vikiwemo vitabu na masilahi kwa walimu. Alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na wasomi waliobobea ambao wanaweza kazi hii ya kuangalia mitalaa inayotumika ili kuona kama inakidhi haja na matakwa ya karne ya sasa.

My Take- Hivi Lowassa anapochukua muda mwingi kuongea haya na vyombo vya Habari ni sehemu sahihi?. Lowassa ni Mbunge kama wabunge wengine kwa nini haya anayoyasema asingeyaongea Bungeni ambayo ni sehemu muafaka na Bajeti ya serikali ndiko inakopitia?

.......
Ni kweli, mfumo wa elimu ufumuliwe, wananachi hawawezi hata kuandika kwa aya.
 
wanajf wenzangu!ni vema mtu ukawa maskini wa hela kuliko kuwa masikin wa kujenga hoja,uwezo wa kutambua unachangia nini na wapi na hasa dunia ya sasa,,well nirejee kwenye mada,mh lowasa kaeleza umhimu wa kupata tume huru ya elimu ambayo itatoa dira na mwanga nini kifanyike katika elimu yetu ili kuweza kumsaidia mtanzania kijana aweze kupata fursa ya ajira au kujiajiri mwenyewe,,nashangaa na kusikitika kuona great thinker wanakuwa watupu na weupe kuchangia kwenye hoja hii muhimu kwa mustakabali wa taifa letu.nilichokiona kwa mleta mada na wengine kama mzee mwanakijiji mnamshambulia lowasa kwa uccm wake na nafasi yake ya upm enzi hzo,na kusema kweli na nina hakika angekuwa bad
 
BMT;

Tanzania ya sasa ina watu wengi wenye elimu na uwezo. Ukiboronga kaa pembeni na waachie wenzako. Lowasa akae tu pembeni.
 
Tunakoelekea waTZ siyo kuzuri. Hivi kweli mtu aogope kutoa dukuduku lake moyoni au mawazo yake ya namna ya kuboresha jambo fulani eti kwa sababu tu jambo analoongelea alishindwa kulitekeleza wakati alipokuwa na fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi!!!??? Sidhani kama hiyo inaketa mantiki. In fact, kuna mambo ambayo ukiwa nje unayaona vizuri kuliko ukiwa ndani. Kwa hiyo, kwa kuwa nchi inahitaji mawazo ya watu katika kuijenga, lazima turuhusu kila mtu awe na uhuru wa kuchangia mawazo yake whether alikuwa au hajawahi kuwa kiongozi.
unajitahiiid kumpalilia mamvi,,,,lakini ndo hivo alichemka
 
Anachosema Lowassa ni kuwa sera za chama chake kuhusu elimu zimeshindwa. It is as simple as that. Na anataka Watanzania wawaangalie wao tena kuona kama wanaweza kutengeneza walichobomoa.

The guy is so desperate.Anaweza kusema ama kufanya chochote.Vitu alivyoshindwa kufanya akiwa PM anataka kutuambia Rais alikua akimzuia?Na vipi hapeleki hoja binafsi au mapendekezo bungeni?

-Hizi ghiliba na ulaghai wanaotaka kupandikiza ni lazima tukabiliane nazo.Kuanzia January tutazunguka vijijini kuwaeleza wananchi ukweli wakati huo huo tukiendelea kuunda mfumo na sera mbadala tutakazotumia baada ya 2015
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Anachosema Lowassa ni kuwa sera za chama chake kuhusu elimu zimeshindwa. It is as simple as that. Na anataka Watanzania wawaangalie wao tena kuona kama wanaweza kutengeneza walichobomoa.

The guy is so desperate.Anaweza kusema ama kufanya chochote.Vitu alivyoshindwa kufanya akiwa PM anataka kutuambia Rais alikua akimzuia?Na vipi hapeleki hoja binafsi au mapendekezo bungeni?

-Hizi ghiliba na ulaghai wanaotaka kupandikiza ni lazima tukabiliane nazo.Kuanzia January tutazunguka vijijini kuwaeleza wananchi ukweli wakati huo huo tukiendelea kuunda mfumo na sera mbadala tutakazotumia baada ya 2015 ingawa si lazima ifike huko vilevile
 
Blah blah blah blah
blah blah blah blah
blah blah blah blah !!!!!!!!!.com
 
BMT;

Tanzania ya sasa ina watu wengi wenye elimu na uwezo. Ukiboronga kaa pembeni na waachie wenzako. Lowasa akae tu pembeni.

Ofcourse akae Pembeni.Kuna mdau kasema kuna vitu unaweza kuona ukiwa pembeni.Yes Namuunga mkono na ndiyo maana tunataka kumshauri na ikibidi kumshinikiza akae pembeni.Hatuko tayari taifa zima kugeuzwa Mradi wa RICHMOND
 
Back
Top Bottom