Lowassa ataka mfumo wa elimu ufumuliwe

Lowassa ataka mfumo wa elimu ufumuliwe

Viongozi wa TZ ni wa ajabu sana!

(1)LOWASA-Alikuwa PM lkn HAKUTHUBUTU kuyasema mapungufu ya mfumo wetu wa elimu na KUYAPATIA UFUMBUZI alipokuwa madarakani!

(2)SUMAYE-Alikuwa PM na ndiye aliitumbukiza nchi kwenye rushwa ya uchaguzi alipoongoza Bunge litunge sheria ya TAKRIMA lkn sasa analia kuwa Mama Nagu alimuangusha kwa rushwa amesahau kuwa ni YY aliyeiasisi!

(3)Mzee Mangula nae juzi kasema atapambana na rushwa lkn KASAHAU kuwa ndiye yeye aliipamba kwa kutamka kuwa"mgombea kuwahudumia wapiga kura KABLA ya kupiga kupiga kura sio dhambi"lkn baadae akalalamika sana alipoangushwa kwa rushwa na Jah People kule Iringa!

INA MAANA VIONGOZI WETU WANAONA MATATIZO HADI WAKITOKA MADARAKANI?Lowassa na wenzake ni wa kupuuzwa na HAWANA JIPYA!

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za bongo, utagundua kuwa udhaifu wa shule za kata Lowasa alianza kuuzungunzia kabla hajaondoka madarakani. Alikuja na program za dharura kukabiliana na uhaba wa waalimu na vile vile kuhiimiza vyuo vikuu kupanua intake ya wanafunzi wa ualimu. Baada ya kuondoka madarakani akaja mtoto wa mkulima na power tiller, elimu ikasahaulika. Baada ya kusema hayo, nadhani ni muhimu kwa viongozi walio nje ya serikali kutoa michango yao ili serikali ya Kikwete izinduke usingizini maana wakisema wapinzani wanaambiwa ni wachochezi na wasioona "mafanikio" ya ccm.
 
Lowassa atasema jambo lolote analofikiri kichwani kwake kuwa litamsafisha, litamfanya akubalike katika mioyo ya wahanga wake. Lowassa we are all your victims. We surely deserve some respect - kuwa haya mawazo ni mazuri. Lakini sio mawazo yako!!!!!! Huyajui, huyaamini, unajisemea tuuu! Tunataka watu wanaosema mambo wanayoyajua,wanayoyaamini
 
Wachangiaji wengi humu JF ni wanafiki watupu tena wanapenda ushabiki usiokuwa na Tija!
Nianze kwa kusema mm sio mwanachama wa CCM! halafu niwaulize huu unafiki wenu! Tatizo ni nini? Kwani alichoongea EL ni uongo!? mara ngapi wadau wanalalamika? kwa hiyo yeye hana haki hiyo ya kuongelea matatizo yanayolalamikiwa kila kona? au mpaka waongee kina dr Slaa au Mh John Mnyika au Mbowe!? hapa huyu jamaa kaongea ukweli kuhusu matatizo pasipo kujali itakadi anatakiwa kuungwa mkono! Au nyie wanafiki mnapinga isiboreshwe tuendelee na mfumo huu wa sasa?
Kila kukicha mtu ana mawazo mapya inawezekana hakuwa nalo wazo hili kipindi kile lakini sasa hivi kutokana na mambo fulani kaona hili tatizo ikabidi aliseme! wangapi mnapanga jambo kesho yake mnabadilisha baada ya kupata mawazo mapya?

Huyu Mh EL mimi simlaumu kuanzisha shule za kata, nani aliyewaambia kuwa shule zikianzishwa zinakamilika siku hizo? acheni porojo kila mtu asimame kwenye nafasi yake katika kuboresha mapungufu na kuiuliza serikali pale ambapo inasua sua kutekeleza wajibu!
acheni unafiki pale penye ukweli tuongee ukweli acheni ushabiki wa kinafiki! hili la elimu ni kweli nalisupport na ni lazima tuipush serikali iwajibike! swala la ajira kwa vijana ni kweli lazima tuikumbushe serikali wajibu wake juu ya tatizo hili
 
Tume ya nini?
Mwenye sera za Elimu za CUF,NCCR na CHADEMA aweke humu tuzione au azione najua anapita humu au vibaraka wake wanapita watampelekea maana lile la Elimu BURE kasha lichukua.


Mkuu Kibanga,
NCCR-Mageuzi wameliongelea hili muda mrefu tu, tangia 2006.
1. Rejea kongamano la Elimu lilioitishwa mwaka huo na NCCR kwa ushirikiano na TANLET, jijini Dar es Salaam

2. Kutoka ilani ya NCCR-Mageuzi ya 2010, utaona humo suala la elimu bure hadi form IV linatajwa, kubadilishwa mitaala ya elimu kunatajwa
4.3.1 ELIMU NA MALEZI YA TAIFA
Uhai wa taifa lolote hutegemea sana misingi ya kielimu na kimaadili inayowaunganisha wananchi wake kuwa taifa moja lenye utamaduni mmoja. Ili kumjenga Mtanzania kiroho na kiakili, ili tuwe na mafanikio ya kiuchumi na kisiasa, na ili tuwe na taifa lenye utamaduni mmoja, hatuna budi kuwa na mfumo wa elimu na malezi ya taifa wenye maudhui na vionjo vya Kitanzania.


Lazima pia tuwe na mfumo wa elimu na malezi ya taifa utakaotupatia Mtanzania wa aina mpya mwenyewe taaluma ya kisasa ya kufanya kazi na kukabiliana na utandawazi wakati huo huo akiwa binadamu mwenye uadilifu, nidhamu, utaifa na moyo wa kujiamini na kuthubutu.
Elimu yetu lazima imjenge Mtanzania anayejiamini na mwenye kuweka mbele utaifa wake. Mtanzania wa aina hii atakuwa mshiriki mkamilifu na mshindani mzuri katika uchumi wa taifa na soko la dunia kwa ujumla.


Elimu hii isitujengee mlarushwa, goigoi, tapeli na msaliti wa maslahi ya Watanzania. Vijana wetu wamalizapo elimu ya msingi lazima wawe wamekamilika siyo tu katika elimu ya kinadharia bali pia kwa stadi za maisha ili waweze kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe na au kuajirika (watimizapo umri). Haya ni mageuzi makubwa ya kielimu yatakayoliondoa taifa kwenye misingi ya elimu iliyowekwa na utawala wa kikoloni kwa manufaa ya ukoloni, na kuliingiza taifa katika mfumo mpya wa elimu inayolenga kuzikomboa fikra ili kutufanya kuwa binadamu huru waliokamilika.


Ili kufanikisha mageuzi hayo, serikali itakayoongozwa na NCCR – Mageuzi itafanya mambo yafuatayo:


(a) Maudhui ya Elimu
1) Itabadili mitaala ya elimu kwa kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu ili kuipa ubora wa hali ya juu na maudhui na vionjo vya Kitanzania.


2) Itahakikisha kwamba mitaala yote nchini ni ile tu yenye manufaa na maana katika maisha halisi ya mtu mmoja mmoja.


3) Itaanzisha mpango kabambe wa elimu ya uraia na elimu ya maisha kwa jamii, mahali pa kazi na katika makazi ya watu.


(b) Mfumo wa Elimu


1) Itahakikisha mfumo wa elimu ya awali (chekechea) unaenea nchi nzima katika maeneo ya makazi, maeneo ya kazi na kwenye kila shule ya msingi ili kuwa na malezi makini kwa watoto na kuwapa fursa wanawake wazazi kushiriki katika shughuli za kila siku za uzalishaji mali.


2) Itaanzisha mfumo mpya wa elimu ya msingi yenye masomo ya stadi za maisha itakayoishia kidato cha nne ambayo itatolewa bure (bila malipo ya ada) kwa watoto wote wa Kitanzania.

3) Itaanzisha elimu ya sekondari itakayochukua miaka miwili ya kidato cha tano na sita kuandaa vijana kuingia vyuo vikuu. Elimu hii itatolewa kwa lugha ya Kiswahili sambamba na masomo ya lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa kuwa ya lazima.

4) Itaanzisha vyuo vya ufundi na mafunzo kwa vitendo kwa wali ambao hawakuchaguliwa kwenda kidato cha tano na sita ili kuwaandaa kwa ajira na pia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu vya ufundi na teknolojia.


5) Itapanua elimu ya vyuo vikuu kwa kuanzisha vyuo vikuu vipya visivyopungua vitatu katika miaka mitano ijayo ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa muda mrefu wa kuupatia kila mkoa angalau chuo kikuu kimoja.


6)Itapanua vyuo vikuu vilivyopo na kuboresha viwango vya taaluma, mazingira ya kusoma kwa wanafunzi na mazingira ya kazi kwa wahadhiri.


7)Itaboresha mishahara, marupurupu na pensheni za walimu wa shule za msingi, sekondari, wakufunzi wa vyuo na wahadhiri wa vyuo vikuu iwiane na gharama halisi za maisha na viwango vya taaluma zao.


8)Itaanzisha vyuo vipya vya waalimu kulingana na mahitaji ya waalimu wa fani mbalimbali za elimu, ufundi na tekinolojia.


9)Itapanua vyuo vya walimu vilivyopo na kuboresha elimu inayotolewa kulingana na mahitaji mapya ya mfumo mpya wa elimu utakaoanzishwa.


(c) Sera ya Elimu


1)Itabadili sera ya elimu ya taifa kwa kuipa maudhui, na upeo kulingana na mahitaji ya kimaadili na kimaendeleo ya taifa.


2)Itaweka asilimia 30 kuwa kiwango cha chini cha bajeti ya taifa kila mwaka kwa ajili ya elimu.


3)Itaanzisha utaratibu wa shule za bweni za wasichana ili kuwawezesha wasichana wengine kusoma pasipo kusumbuliwa na shughuli za nyumbani ambazo zimekuwa zikiathiri vibaya maendeleo yao ya kitaaluma.


4)Itaweka uwiano mzuri kati ya wanafunzi wa kiume na wa kike wanaojiunga na masomo vyuoni na kuzipa nafasi katika mitaala hoja za jinsia, uraia, haki za binadamu na utaifa.


5)Itaanzisha chuo cha taifa cha kufundisha viongozi kutoka sekta mbalimbali za jamii nchini ili kuipa nchi yetu mwelekeo maalum wa kudumu wa utamaduni wa kisiasa na demokrasia huru na maadili ya taifa.


6)Itaondoa kodi kwenye vifaa vya elimu na kuzipa ruzuku taasisi binafsi zinazoshiriki kutoa elimu rasmi ili kuziongezea uwezo wa kutoa huduma ya elimu kwa jamii inayofanana na ile ya taasisi za serikali.


7)Itahamasisha, itawezesha na kutoa vivutio na motisha kwa watafiti na wanasayansi na pia kutunza na kulinda uvumbuzi wao.



3. Rejea hoja ya Mbatia hivi karibuni Bungeni

HOJA BINAFSI BUNGENI KUHUSU UDHAIFU KATIKA SEKTA YA ELIMU NCHINI
James Francis Mbatia,
Oktoba, 2012
1. UTANGULIZI: MUKTADHA YA HOJA
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kwa kuwa tangu Taifa letu lipate uhuru wake mwaka 1961 (kwa Tanzania Bara) na mwaka 1964 (Mapinduzi ya Zanzibar) tulitambua umuhimu wa kufuta ujinga, kuelimisha wananchi ili tujiletee maendeleo, na hadi sasa kazi kubwa imefanyika katika kukuza elimu hapa nchini;Kwa kuwa katika Dira ya Taifa ya 2025 tunataja pamoja na mambo mengine kwamba, ifikapo mwaka 2025 tuwe tumejenga taifa la watu walioelimika kwa upeo wa juu; Kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, ambao una malengo manane ya millennia, lengo la pili likiwa ni elimu bora kwa wote; Na kwa kuwa ifikapo mwaka 2015 (takribani miaka mitatu toka sasa) itatubidi tujipime kwenye utekelezaji wa malengo hayo; Na kwa kuwa kwa muda mrefu kumekuwepo na viashiria vingi vinavyoonesha kwamba ubora wa elimu itolewayo nchini katika ngazi zote haulidhishi; Ipo haja ya kutathmini kwa undani hali ya elimu nchini na kuchukua hatua stahiki sasa.

2. OMBI NA UHALALI WA KUTOA HOJA HII
MheshimiwaSpika,Kwa mujibu wa Kanuni ya 56(1) ya Kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007, naomba kutoa hoja binafsi kuhusu Udhaifu ulioko katika sekta ya Elimu Nchini.Mheshimiwa Spika, Pamoja na kutambua kazi kubwa ambayo Serikali, kupitia wizara yenye dhamana ya Elimu imefanikiwa kuifanya; Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kwamba, hivi sasa taifa letu limo kwenye mgogoro mkubwa katika sekta ya Elimu. Mgogoro huu unajionesha katika sura zifuatayo: i. Kumomonyoka kwa maadili katika jamii ya Taifa letu; ii. Kuporomoka kwa Uadilifu miongoni mwa watumishi wa umma na kada nyinginezo; iii. Kuporomoka kwa Uwajibikaji; iv. Kuporomoka kwa kiwango cha utii wa Sheria na Kanuni mbalimbali; v. Kukithiri za ukiukwaji wa haki za Binadamu; vi. Kukua kwa utamaduni wa Ukupe; vii. Kutokuthamani Rasilmali, hususan rasilmali Muda; na viii. Kupungua kwa uzalendo miongoni mwa baadhi ya wananchi
Mheshimiwa Spika,
Sura tajwa hapo juu, ndizo chimbuko la matatizo yafuatayo:a. Kuporomoka kwa viwango vya huduma zitolewazo katika sekta mbalimbali;b. Kuporomoka kwa viwango na ubora wa bidhaa, majengo, na miundombinu;c. Kuporomoka kwa viwango vya uzalishaji wa bidhaa mashambani na viwandani;d. Uharibifu na uchafuzi wa mazingira;e. Udhaifu katika kukabiliana na majanga mbalimbali kama vile mafuriko, na matetemeko ya ardhi;f. Udhaifu katika kuzuia na kudhibiti ajali zinazoweza kuzuilika, kama vile: za vyombo vya usafiri, moto na milipuko ya silaha;g. Udhaifu katika kukabiliana na hatari za kiafya kwa binadamu na wanyama zitokanazo na uchimbaji wa migodini na usafirishaji au uhifadhi wa kemikali;h. Migomo ya Waalimu na Wanafunzi katika ngazi mbalimbali za mafunzo;i. Migomo ya wanataaluma mbalimbali; naj. Migomo ya wafanyakazi wa kada nyinginezok. Na katika namna ambayo ni mzunguko endelevu wa tatizo; Kuporomoka kwa viwango vya ubora wa elimu

3. UDHAIFU KATIKA MFUMO WA ELIMU
Mheshimiwa Spika,Hakika udhaifu ulioko katika sekta ya Elimu ndicho kirusi kilichoambukizwa katika sekta nyingine zote katika taifa letu, kwa sababu: A.Maendeleo yote ya taifa (kijamii, kiuchumi na kisiasa) ni tunda la mfumo wake wa Elimu. B. Uhai wa taifa lolote hutegemea wingi wa wananchi wake WALIOELIMIKA vyema.Kwa lugha nyingine, upo uhusiano sababishi kati ya elimu duni na ukengeufu katika jamii na hatimaye utendaji dhaifu katika uchumi na siasa za nchi. Uhusiano huu umethibitika kitaalamu.
Mheshimiwa Spika, Kwa ajili ya kuokoa muda, nitazungumzia sehemu ndogo tu ya udhaifu uliomo katika mfumo wetu rasmi wa Elimu. Hoja kwa kielelezo.Matokeo ya Utafiti niliofanya, kwa takribani miaka 17 sasa, yanaonesha ya kwamba udhaifu wa mfumo wetu rasmi wa elimu unatokana na mambo makuu matatu, ambayo hapa nchini imekuwa ni nadra kuyaangalia kwa undani tunapoendelea kutafuta ni kwa nini tumekwama katika masuala mbalimbali. Mambo hayo ni: I. Sera ya Elimu ya Taifa ya tangu mwaka 1995 na sera nyinginezo; II. Mitaala ya Elimu ya shule za Msingi na Sekondari; na III. Mihtasari ya Masomo na vitabu vitumikavyo katika shule za Msingi na Sekondari.

3.1TATIZO LA KISERA
Mheshimiwa Spika,Sera ya elimu ya taifa tunayoitumia sasa imekuwepo kwa muda mrefu sasa. Ukweli huo tu watosha kuonesha haja ya kuifanyia tathmini kubwa sera hiyo, ili licha ya kuangalia ni nini tumetekeleza na ni nini hatukutekeleza, tuifanye iendane na mahitaji yetu ya sasa. Ninatambua hatua zilizokwishachukuliwa na wizara husika, lakini kusudio la kuwa na sera mpya halijafanikiwa. Aidha, miongoni mwa mambo yaliyo bayana kwa sasa ni kwamba, masuala mengi ya kisera katika elimu, tunayoyafuata hapa nchini, yametokana na masharti na/au maelekezo tuliyopewa na vyombo vya kimataifa kama vile Benki ya Dunia, na Shirika la Fedha Duniani (IMF). Hata hivyo maelekezo ya vyombo hivi badala ya kutusaidia kuinua ubora wa elimu yametuletea matokeo yasiyokuwa mazuri na yanatuyumbisha. Matharani, miaka ya themanini vyombo hivi vilitutaka tupunguze matumizi ya raslimali za umma katika kugharimia huduma za jamii, ikiwemo elimu, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa uduni wa shule za umma nchini. Kana kwamba haitoshi vyombo hivi viliwahi kututaka tuelekeze zaidi raslimali katika elimu ya msingi, lakini miaka ya hivi karibuni vimebadili ushauri huo na kudai raslimali zaidi zielekezwe elimu ya juu. Ni kana kwamba tumegeuzwa kuwa sampuli ya kufanyiwa majaribio katika mahabara za kisera bila kujali athari mbaya za majaribio hayo. Kama taifa tunapaswa kutumia sera ambazo zimethibitika kitaalamu kwamba zinaleta matunda yanayotakiwa. Tusiendelee kuyumbishwa na vyombo ambavyo sera vinazozisimamia si za maslahi kwetu, kwa sababu tu sisi ni wahitaji wa misaada yao.

3.2(a) TATIZO LA MITAALA
Mheshimiwa Spika,Sanjari na matatizo hayo ya kisera, ni jambo la kusikitisha sana kwamba, hadi mwaka 2011, nchi yetu haikuwahi kuwa na mitaala rasmi ya kifaifa kwa ajili ya Elimu ya shule za msingi au sekondari. Ijapokuwa Wanasiasa, Wanaharakati na Wanataaluma wamekuwa wakiilalamikia wizara ya elimu kuwa na mitaala mibovu; lakini ukweli ni kwamba mitaala hiyo haikuwahi kuwepo. Hatujawahi kuwa na andiko mahususi la mtaala wa elimu kwa Taifa la Tanzania. Kwa mantiki hiyo, kwa miaka mingi tumekuwa na chombo ‘mfumo wa elimu' lakini kisicho na usukani. Taasisi ya Elimu imekuwa ikiajiri Wakuza Mitaala kwa zaidi ya miaka 15, bila ya kutoa mitaala yoyote katika namna ya andiko mahususi; KULIKONI?
Nitoe angalizo pia, kwamba nyaraka za wizara ya elimu zina ainisho la dhana ya mitaala ambalo kwa kiasi fulani ainisho hilo nalo linatoa mtazamo usiotuwezesha kutambua mitaala tunayotakiwa kuwa nayo kwa mapana yake ambayo taaluma ya ukuzaji mitaala inayatambua. Ukiangalia kwa mfano, rasimu ya pili ya sera mpya ya elimu inaeleza mtaala kama ifuatavyo;‘Mtaala wa Elimu ni jumla ya mambo ambayo mlengwa anatakiwa kuyapata katika mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa lengo la kufikia matarajio ya jamii na taifa.'
Ainisho hili lina ukweli kiasi, lakini lugha yake ni ya jumla jumla sana. Matharani, maneno yaliyotumika; 'mtaala … ni jumla ya mambo …' sio maelezo mahususi, maana hayaelezi ni mambo gani hasa hayo. Aidha, ainisho halitaji sababu hasa (purpose) ya utoaji elimu, halifafanui mchakato wa utoaji elimu hiyo (unafanyikaje na unafanyikia wapi), halielezi vigezo na mamna ya kupimwa kwa ufikiaji wa malengo ya elimu, na wala halitaji wazi wazi matokeo tarajiwa ya elimu italajiwayo. Laiti kama nyaraka zetu zingetaja kuwa mtaala ni jumla ya maarifa, maadili, ujuzi na uzoefu, ainisho hilo lingekuwa wazi zaidi. Tunapaswa kuzingatia pia kwamba mtaala ni mchakato (mchakato huo lazima tuuseme); mtaala ni jitihada ya kutokeza mazao fulani (mazao hayo lazima tuyataje, tusiishie kusema tu kwamba ni 'matarajio ya jamii na taifa…', bali matarajio mahususi ambayo ni stadi, uwezo, na mitazamo tunayotaka wanaofundishwa maarifa na ujuzi fulani wawe nayo), na mtaala ni praxis; sharti maarifa na ujuzi yaonekane katika vitendo na mienendo ya waliopata elimu.

Mheshimiwa Spika,Katika nchi nyingi duniani, wazazi au walezi wa kila mtoto aendaye shuleni wana haki ya kujua mtaala wa shule husika. Kwa kuzingatia haki hiyo vyombo vya elimu huwajibika kumpatia kila mzazi/mlezi nakala ya mtaala inayoonesha wazi sababu za mwanae kupatiwa elimu ya kiwango husika, elimu hiyo itapatikana katika mchakato gani, ni nini kinachotarajiwa kuwa badiliko la mtoto baada ya kupatiwa elimu hiyo, na badiliko hilo litapimwa namna gani. Utaratibu wa namna hiyo huwapatia wazazi na walezi ushiriki wa moja kwa moja katika utekelezaji wa mtaala. Hapa kwetu hayo hatufanyi, si tu kwa sababu hatujawa na uwezo huo bali hata mtaala wenyewe (kama nilivyokwisha eleza) hatukuwa nayo tangu uhuru (hadi mwaka huu ambako naambiwa kuna andiko ambalo hata hivyo bado halijatolewa kwa umma).

3.2 (b) TATIZO KATIKA MIHTASARI
MheshimiwaSpika, Kwa kuwa mitaala ndiyo inayoweka malengo ya elimu yanayoongoza utengenezaji wa Mihtasari wa masomo yote, licha ya kwamba mitaala hatuna, Mihtasari iliyopo (ambayo kwa maana hiyo inatokana na mazoea tu ya uwepo wa mfumo wa elimu) hivi sasa haina Malengo yanayoeleweka vyema, na imekosa viwango vya kitaaluma vinavyokubalika kitaalam. Mihtasari yote iliyopo, inaonesha kwamba, kama taifa tumeshindwa kutofautisha malengo na madhumuni ya Elimu ya Mtanzania. Aidha, mihtasari hiyo inaonesha kwamba tumeshindwa kutumia vyema lugha rasmi za kitaifa (Kiswahili na Kiingereza) katika kubainisha malengo hayo.Kwa mfano:A.Katika nyaraka za wizara (mihitasari) zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili, malengo ya Elimu yapo Kumi, wakati zilizoko katika Kiingereza malengo yapo Tisa. B. Katika malengo hayo, kuna sentensi moja ya kiingereza yenye kiunganishi "and" mara saba; na sentensi hiyo imekuwa ikitumiwa hivyo hivyo tangu mwaka 1995 ilipoandikwa katika Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo. C.Malengo ya Elimu ya Msingi, kwa lugha ya Kiswahili, yapo 18; wakati katika lugha ya Kiingereza yapo 10. Ni aina gani basi ya elimu tuliyonayo, kama malengo yake yamebainishwa kwa namna ya ubabaishaji kiasi hicho?

4.
UDHAIFU KATIKA VITABU VYA KIADA NA ZIADA
Mheshimiwa Spika,Licha ya matatizo ya kimkakati tuliyonayo katika nyaraka zinazoongoza elimu, kuna udhaifu mkubwa katika utendaji; kiuwezo na kimaadili.Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, kitengo kilichopo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kinachotoa ithibati kwa vitabu vya kiada na ziada – Educational Materials Approval Committee (EMAC), kimeshindwa kutekeleza wajibu wake kama inavyopaswa. Kitengo hiki kimesababisha mafuriko ya vitabu vinavyopotosha Elimu ya taifa letu.Kwa mfano, sio tu kwamba vitabu vingi vya somo la Hisabati vilivyopewa ithibati na EMAC vina makosa mengi ya Kitaaluma, lakini hata mfumo wa uandaaji wa vitabu hivyo una harufu ya Ufisadi.
MheshimiwaSpika, Nitatoa mfano.Mnamo mwaka 2009 kupitia mpango uitwao ‘Teaching and Learning Materials Program (TLMP), Taifa letu lilipata msaada wa dola za Kimarekani milioni 13, ambazo ni sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 20 na milioni 400, kutoka shirika la United States Agency for International Development (USAID), kwa ajili ya kuandika na kuchapisha vitabu, na kugharimia vifaa vya kufundishia masomo ya Hisabati, Fizikia, Kemia na Elimu-Viumbe kwa idadi isiyopungua milioni 2, laki 2 na elfu 50. Makosa lukuki yaliyo katika vitabu vilivyochapishwa kutokana na mradi huo yanatisha na kusikitisha; hasa ikizingatiwa kwamba Wizara ilipata uwezeshaji wa timu ya Watalamu kutoka South Carolina State University. Matharani, katika vitabu vya "Mathematics for Secondary Schools, Volume I, II, III, and IV", kama inavyoonekana kwenye utangulizi wake; Mwandishi Mkuu, ndiye huyo huyo Mhariri Mkuu, na pia ni Msomaji Mkuu. Kitaaluma na kimaadili, mtu haruhusiwi kuhariri au kupitia andiko lake mwenyewe. Utaratibu huu kengeufu ulitumika pia kwa wengine wote walioshiriki kuandika vitabu hivyo; walipewa nafasi ya kuhariri na kupitia kazi yao wenyewe. Dosari hii haikubaliki popote duniani.
MheshimiwaSpika,Harufu ya ufisadi inayofuka katika jambo hili, iko katika mambo matatu: I. Mgongano wa kimaslahi; Hapa ni pale watendaji wa EMAC waliposhiriki kuandika vitabu walivyovipatia ithibati; II. Utayarishwaji wa andiko (typesetting) kufanyika nchini Malaysia, na upigaji chapa kufanyika nchini Kenya. Kazi hizi zinaweza kufanyika hapa nchini, kwa maslahi ya taifa letu. III. Vitabu viliandikwa kwa idadi ya waandishi isiyowiana: Wamarekani 10, na Watanzania 4. Hata hivyo lugha iliyotumika katika "Volumes" zote 4 sio sahihi. Yaani, Kiingereza ni kibovu; jambo ambalo linalopotosha wanafunzi na kuwafanya wasielewe mada au maudhui yaliyokusudiwa.
Mheshimiwa Spika, Hii ni mifano michache tu inayothibitisha mgogoro mkubwa uliopo katika sekta yetu ya Elimu hapa nchini.

5.
HOJA
Mheshimiwa Spika,Kwa mujibu wa Kanuni ya 117(1) na (3) za kudumu za Bunge; ninaomba kutoa hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ya kuchuguza kina cha udhaifu huu wa kimfumo katika sekta ya Elimu hapa nchini. Aidha, ikiwezekana kamati hiyo ipendekeze hatua za kuchukuliwa ili taifa liondokane na udhaifu huo hatari.

6.
HITIMISHO
Mheshimiwa Spika,Nisisitize kwamba, Elimu iliyopangwa kwa sera bora na mitaala bora pekee, yenye mihitasari na vitabu vilivyotayarishwa kwa umakini mkubwa na uadilifu, ndiyo yenye uwezo wa kujenga Taifa la watu waadilifu, wazalendo, wachapakazi, watambuzi wa haki na wajibu wao katika jamii. Elimu ndio Mapigo ya Moyo ya Taifa letu. Mapigo ya Moyo yakienda kinyume na asilia yake, UHAI huweza KUPOTEA! Tunao wajibu wa kuokoa uhai huo.

MheshimiwaSpika,NAOMBA KUTOA HOJA.
 
Vipi mbona unasalimia Kama vile unataka kuomba kura ili uchaguliwe ? Anyway siwezi kuitikia maana sijui umri wako na wewe hujui wangu!

Baada ya hapo niseme sasa akina lowasa na ccm yao wamekaa madarakani muda mrefu na wamekuwa na muda Wa kutosha kujaribu kila aina ya mawazo Na sera zao , ziwe mpya au za ku copy na ku pasty ! Ni wazi kwamba ni vinganganizi na wameshoka !

Wawape basi nafasi na wengine wajaribu ili tuone mawazo na sera zao !

Akina lowasa wameishiwa na sera na wameshoka na mawazo Yao pia ! Sasa wapumzike na kuwaacha akina Dovutwa ( wapinzani ) wajaribu kusukuma gurudu la elimu !

Ni hayo tu kijana Wa shikamoo !
 
Lowasa ni mnafiki wa kutupwa. Nchi aifilisi yeye na mafisadi wenzake ambao kila leo wako njiani ama kubembea au kutibiwa majuu kwa gharama ya walipa kodi. Watoto wao wawasomesha majuu, nchi za majirani, au nchini kwenye shule zenye hadhi kwa kodi zetu. Leo hii analalamikia mfumo wa elimu aliouanzisha mwenyewe akijua hautamuadhiri yeye na mafisadi wenzie. Hii in maana kweli? Kwa sasa watanzania tumeshaumizwa ya kutosha na hii mifisadi. Kwa sasa afunge domo lake asubiri 2015 tumwonyeshe kwa vitendo kuwa tuna akili kuliko anavyofikiri. Yaani inashangaza hakusoma hata alama za nyakati pale Arumeru alipokuwa anavalia shati la kijani na kupiga makelele ya chura.
 
Mimeisikia kauri ya waziri mstaafu juu ya elimu yetu kuwa mahututi na ndoto zake namunga mkono miakwamia mheshimiwa huyu. Pamoja na yote yaliyopita na kashfa nyingi juu yake naoma kama huyi mzee sasa amefahamu wapi alijikwaa. Hakika kuinua maendeleo ya nchii hii ni kuinua elimu yetu na si elimu hii ya makundi pia hatuwezi kuinua elimu kama hatukuwajali walimu wanaofundisha. Hongera Lowasa umeona mbali kila binadamu hujifunza kwa makosa.
 
Ni mafanikio gani aliyoongoza?Ina maana 2008 alipokua anashughulika hakuona miaka 5 mbele?Huyu naye ni kiongozi?
 
Mimeisikia kauri ya waziri mstaafu juu ya elimu yetu kuwa mahututi na ndoto zake namunga mkono miakwamia mheshimiwa huyu. Pamoja na yote yaliyopita na kashfa nyingi juu yake naoma kama huyi mzee sasa amefahamu wapi alijikwaa. Hakika kuinua maendeleo ya nchii hii ni kuinua elimu yetu na si elimu hii ya makundi pia hatuwezi kuinua elimu kama hatukuwajali walimu wanaofundisha. Hongera Low,
walimu ni ngaz ya kufikia malengo yenuya kisiasa,mkipata mnchokitaka mnaanza kuwatukana mara mbayuwai na kutowajali.
 
Huyu White Hair Aache Mambo Ya Ajabu, Kwann Kipindi Hoja Binafsi Ya Mbatia Inawasilishwa Alikuwa Kimyaaaaaaa Hakumshauri Asha Ngedere Waichukulie Criaz Hyo Kitu? Anaota Urais Huyu Hakuna Kingine!
 
Huyu bwana naye anakera na siasa zake za woga; haya mambo ya kushuka kwa kiwango cha elimu na ukosefu wa ajira kwa vijana "time bomb" tumemsikia mara nyingi sana akiyarudia rudia, kinachoudhi haya mambo makubwa na ya maana kweli kweli kwa nini anapenda kuyazungumzia kwenye vikao visivyo na maamuzi!? Interviews; radio talk shows na kwenye fund raising zake lukuki makanisani?!

Kwa nini hatujawahi kumuona au kumsikia akiyasema na kuyatilia mkazo katika vikao muhimu vyenye maamuzi kama ndani ya Bunge au katika vikao vya kamati kuu na NEC vya CCM!!??

Mara ya mwisho Lowassa kuzungumza bungeni ni siku alipoitaka serikali kuwa kuchukua maamuzi magumu; akabezwa!takribani mwaka mmoja na nusu uliopita! kuanzia wakati huo EL ni Bubu akiwa Bungeni lakini huko makanisani na kwenye talk shows loo; utafikiri kawekewa flash disc!!

Wacha majungu EL; chukua maamuzi magumu zungumza ndani ya vikao vya kiutendaji
 
Back
Top Bottom