Lowassa ataka mfumo wa elimu ufumuliwe

Lowassa ataka mfumo wa elimu ufumuliwe

Matatizo ktk elimu ya Tanzania ni ya muda mreru sana. kama leo hii wanafunzi wengi wanakaa chini, hakuna vitabu vya kutosha, hakuna maabara, zana nyingine za kufunrishia kwa walimu hakuna. mishahara midogo kwa walimu na pia kuchelewa kulipwa madai yao mbalimbali nk Je hali hii haikuwepo kipindi Lowasa Waziri Mkuu? Hali ilikuwa hivihivi, je hakuiona? Kwa nini leo? au ndio anataka kujitengezea mazingira mazuri yq 2015 na aonekane mwema na mwenye uchungu na nchi hii? Je anadhani kwa mfano akirudi kuwa kiongozi wa nchi hii ndio atayaona tena haya? Me nasema, v2 alivyosema sio vibaya ila alipaswa kuyatekeleza alipokuwa kwenye nafasi ya kufanya hivyo, kwa hivi sasa itakuwa ni unafiki na kutafuta tu umaarufu ambao kwa sasa ni mgumu kwa vile watu tumeshamshtukia. Ajipange upya kivingine
 
Kiongozi yeyote ambaye amewahi kuiba hata shilingi moja ya UMMA, hatakiwi kufumbua mdomo wake kuwatetea wananchi. Haiwezekani unapokuwa gizani unauma, ukiwa kwenye mwanga unatetea. Huo ni unafiki
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huyu huyu Lowassa angekuwa bado serikalini angetetea kwa nguvu zake zote utendaji wa serikali. Ndiye aliyeanzisha shule za kata, ni lini amegundua kuwa kuna haja ya kuwa na waalimu bora kabla ya kuanzisha hizo shule? He is part of the problem, he cannot be part of the solution.
Alipoulizwa kuhusu walimu na vitendea kazi, Lowassa alisisitiza shule lazima zijengwe. Kukaa benchi kama kunamfanya mtu awe na akili basi kila kiongozi angekaa benchi kama mwaka na kurudi kazini.

Ujumbe wa Lowassa ni kuwa yeye ndiye alisimamia ujenzi wa shule za kata! kampeni
 
The guy is so desperate.Anaweza kusema ama kufanya chochote.Vitu alivyoshindwa kufanya akiwa PM anataka kutuambia Rais alikua akimzuia?Na vipi hapeleki hoja binafsi au mapendekezo bungeni?

-Hizi ghiliba na ulaghai wanaotaka kupandikiza ni lazima tukabiliane nazo.Kuanzia January tutazunguka vijijini kuwaeleza wananchi ukweli wakati huo huo tukiendelea kuunda mfumo na sera mbadala tutakazotumia baada ya 2015.......

Ndugu Ben naomba mkipita huko vijijini mchukue majina na namba za wanaopenda mabadiliko kwa ajili ya kuwasiliana nao mara kwa mara pindi mtakapokuwa mmeshapita kwa ajili ya kuhamasisha mabadiliko. huu ni wakati wa mabadiliko hatuwezi kukubali kuwa na mfumo wa waziri yule yule toka 1990 mpaka leo yeye ni kubadilisha wizara tu
 
Ndugu Ben naomba mkipita huko vijijini mchukue majina na namba za wanaopenda mabadiliko kwa ajili ya kuwasiliana nao mara kwa mara pindi mtakapokuwa mmeshapita kwa ajili ya kuhamasisha mabadiliko. huu ni wakati wa mabadiliko hatuwezi kukubali kuwa na mfumo wa waziri yule yule toka 1990 mpaka leo yeye ni kubadilisha wizara tu......

Noted Mkuu.
 
Ndugu Ben naomba mkipita huko vijijini mchukue majina na namba za wanaopenda mabadiliko kwa ajili ya kuwasiliana nao mara kwa mara pindi mtakapokuwa mmeshapita kwa ajili ya kuhamasisha mabadiliko. huu ni wakati wa mabadiliko hatuwezi kukubali kuwa na mfumo wa waziri yule yule toka 1990 mpaka leo yeye ni kubadilisha wizara tu........

Noted Mkuu!
 
Lowassa ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge inahusika na usalama & mambo ya nje. Ningetaka kujua, ni kwanini huyu mwenyekiti (Lowassa) haoengii kuhusu hali ya usalama wa raia na mali zao? Ni kwanini Lowassa hajaita waandishi wa habari, kama anavyofanya kwenye hii issue ya elimu, na kutoa maoni yake juu ya mauaji wa raia wasio na hatia?

Watanzania wanaoishi mipakanani wanavamiwa kila kukicha na watu wanaodhaniwa kutoka nchi jirani, maharamia wamezagaa kila kona, na wengine wamefia Dodoma, ni lini Lowassa ataongea? Silaha za moto ni nyingi mno huku mtaani na zinatumika kwenye ujambazi, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi anasemaje?

Lowassa ni ameshiriki sana kuanzisha shule za kata, na matokeo ya hizo shule yanaonekana sasa. Je, watanzania waendelee kuamini huyu mtu ana jipya la maana kwenye elimu?
 
Viongozi wa TZ ni wa ajabu sana!

(1)LOWASA-Alikuwa PM lkn HAKUTHUBUTU kuyasema mapungufu ya mfumo wetu wa elimu na KUYAPATIA UFUMBUZI alipokuwa madarakani!

(2)SUMAYE-Alikuwa PM na ndiye aliitumbukiza nchi kwenye rushwa ya uchaguzi alipoongoza Bunge litunge sheria ya TAKRIMA lkn sasa analia kuwa Mama Nagu alimuangusha kwa rushwa amesahau kuwa ni YY aliyeiasisi!

(3)Mzee Mangula nae juzi kasema atapambana na rushwa lkn KASAHAU kuwa ndiye yeye aliipamba kwa kutamka kuwa"mgombea kuwahudumia wapiga kura KABLA ya kupiga kupiga kura sio dhambi"lkn baadae akalalamika sana alipoangushwa kwa rushwa na Jah People kule Iringa!

INA MAANA VIONGOZI WETU WANAONA MATATIZO HADI WAKITOKA MADARAKANI?Lowassa na wenzake ni wa kupuuzwa na HAWANA JIPYA!........

Kwa kweli uliyoyasema yanahitaji kutiliwa maanani. Labda cha kuongezea hapa ni kwamba yawezekana wanapoexperience practical (real life) ya kitu ndipo wanaona madhara yake kwamba ni makubwa.

Pia yawezekana ndo wanakuwa na uelewa mzuri wa maswala hayo kwani binadamu hujifunza daima.
 
Ofcourse akae Pembeni.Kuna mdau kasema kuna vitu unaweza kuona ukiwa pembeni.Yes Namuunga mkono na ndiyo maana tunataka kumshauri na ikibidi kumshinikiza akae pembeni.Hatuko tayari taifa zima kugeuzwa Mradi wa RICHMOND

Ben Richmond unajua ya nani? yeye kama mtanzania kwenye katiba ibara ya 8 ana haki ya kuongea kuhusu nchi au kushauri hivyo siasa isipitilize wakati mwingine." KUNYATA ANYATE KINYONGA AKINYATA KICHECHE ANA VIZIA KUKU"
 
Simba Mangu ..... Hatuihatji kujua Richmond ni ya nani kwa sasa.. tutajua ni ya nani, wapi na nini tukisha badilisha uwezo wa kufikiri na kuja na mawazo mapya.. swali hilo la Richmond jibu lake ni lahisi sana ....ni kwamba Richmond ifanyika au ilikuwepo wakati yeye akiwa waziri mkuu na ndio maana akajiuzuru.. well done.. kwa Losawa kusema kwamba tunahitaji tume huru ya elimu maana yake ni kusema kwamba serikali yao ya CCM imepungukiwa mawazo ya kutoa suluhisho la tatizo la elimu Tanzania... Ni kwa nini kama mbuge asije na hoja ya tume huru au mswaada mpya bungeni a u anataka kutengenza ulaji mwingine wa tume huru.... serikali ina ma-expert kibao na sijui hao ma-ex[ert wa elimi ni hiviyo au nini.... kwa nini basi wasiwajaribu hata akina Rajani wa Twaweza... labda watasaidia... kama kweli serikali haina mawazo mapya yafaa sasa katiba mpya ije na kipengele cha ku-recall the whole governement for gross incompetence na kuifanya sio tu elimu bali hata secta nyngine kama afya, mazingira na uchumi kudorora... hii ni Dereliction of basic duties of the government kwa wananchi wa Tanzania maana hatukuwachagua waje kutuambia tunahitaji tume huru...

Kuna mambo yanahitaji tume huru na sio kama haya ya elimu.. Elimu inatakiwa mawazo mpya na kuwa na new policy framework Pia .. kuwapa waalimu motisha wa maana na kuajili competent people....

Akili zile zile zilizosababisha matatizo yaleyale mengi ya watanzania haziwezi kuyaondoa matatizo hayo.. tunahitaji akili mpya ili zije kutoa ufumbuzi wa matatizo yaliyosababishwa na akili za zamani...

Ndio maana tunaona wana-copy na ku-pasty sera za akina Dovutwa (Wapinzani) kwa sana bila ku-acknowledge source.. yaani ni kuibia mtindo mmoja halafu wanataka watanzania tukubali kwamba kuibia inaruhusiwa katika mtihani wa matatizo....wakati siku zote tumeambia shuleni primary kuibia hairuhusiwi na ukigunduliwa unafutiwa matokeo.. kwa nini tusiwafutie matokeo basi na tufanye mtihani mpya ili tu-pass
 
Anachosema Lowassa ni kuwa sera za chama chake kuhusu elimu zimeshindwa. It is as simple as that. Na anataka Watanzania wawaangalie wao tena kuona kama wanaweza kutengeneza walichobomoa.

Anachofanya ni kudivert attention ya big issues. Pamoja na kuwa ni kweli elimu yetu ina tatizo, ufisadi ni tatizo kubwa zaidi kuliko hilo, ufisadi unatakiwa kushughulikiwa kwanza. Will be good if he will be talking about that.
 
Tunakoelekea waTZ siyo kuzuri. Hivi kweli mtu aogope kutoa dukuduku lake moyoni au mawazo yake ya namna ya kuboresha jambo fulani eti kwa sababu tu jambo analoongelea alishindwa kulitekeleza wakati alipokuwa na fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi!!!??? Sidhani kama hiyo inaketa mantiki. In fact, kuna mambo ambayo ukiwa nje unayaona vizuri kuliko ukiwa ndani. Kwa hiyo, kwa kuwa nchi inahitaji mawazo ya watu katika kuijenga, lazima turuhusu kila mtu awe na uhuru wa kuchangia mawazo yake whether alikuwa au hajawahi kuwa kiongozi.

Lakini watu wanakuwa na doubt pale ambapo mtu anatoa maoni akiwa na ambitions huku akiacha kutolea maoni yale ya nayo mhusu zaidi kwa sasa..Tumeona mambo ya ulinzi wa raia wa nchi hii chini ya matukio mabalimbali ya ki-polisi...Hapo huyo mtu hatoi maoni anakaa kimya; then inapokuja kwenye maoni ya kinadharia ndiyo utaona anakuja na mambo lukuki tena akiwa ameshapata kuwa na nafasi ya kuyatenda lakini hakuyatenda...

Huwezi kusema utafanya ama tunapaswa kufanya hiki wakati wewe katika nafasi yako hufanyi kile unachotakiwa kufanya kwa wakati huo unapotoa maoni ya mambo mengine ambayo yako mbali zaidi. Mchagua jembe si mkulima so to speak!
 
Viongozi wa TZ ni wa ajabu sana!

(1)LOWASA-Alikuwa PM lkn HAKUTHUBUTU kuyasema mapungufu ya mfumo wetu wa elimu na KUYAPATIA UFUMBUZI alipokuwa madarakani!

(2)SUMAYE-Alikuwa PM na ndiye aliitumbukiza nchi kwenye rushwa ya uchaguzi alipoongoza Bunge litunge sheria ya TAKRIMA lkn sasa analia kuwa Mama Nagu alimuangusha kwa rushwa amesahau kuwa ni YY aliyeiasisi!

(3)Mzee Mangula nae juzi kasema atapambana na rushwa lkn KASAHAU kuwa ndiye yeye aliipamba kwa kutamka kuwa"mgombea kuwahudumia wapiga kura KABLA ya kupiga kupiga kura sio dhambi"lkn baadae akalalamika sana alipoangushwa kwa rushwa na Jah People kule Iringa!

INA MAANA VIONGOZI WETU WANAONA MATATIZO HADI WAKITOKA MADARAKANI?Lowassa na wenzake ni wa kupuuzwa na HAWANA JIPYA!

Ninachoipenda JF ni watu kuwa na reference pindi mambo yanapotokea ndivyosivyo kama yanayojiri sasa kumbe wale walalamikao ndio walioasisi
 
Anayosema EL ni strategy ya kutaka kurudi kwa nguvu wakati wananchi tunafahamu kwamba alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuhakikisha hayo yote yanatendeka pindi alipokuwa PM, anaposema sasa hivi ni kama janja ya nyani tu kwa kuwa anajua tumesahau
 
Tume ya nini?
Mwenye sera za Elimu za CUF,NCCR na CHADEMA aweke humu tuzione au azione najua anapita humu au vibaraka wake wanapita watampelekea maana lile la Elimu BURE kasha lichukua.
 
Anaota uras huyo, anajitafna tafna na kujing'ata meno tuone anahuruma nasisi. Mbona hakuizuia Richmond akaacha ijipenyeze bila

kuchukua hatua mpaka bunge likaingilia? Mwizi ni mwizi tu hata kama aseme yeye hahusiki lakini yeye si alikuwa kolongo la kupitia huo uchafu wa Richmond!!!!
 
Lowassa acha unafiki, amekuwa waziri miaka Ishirini mitatu ikiwa waziri mkuu, alifanya nini kwa wananchi asimame na aseme ili tujue nje ya hapo anataka simpathy vote. Atueleza kwanza yeye kama mtumshi wa umma aliwezaje kuapata Nyumba Mbili pale mahando, na zile za arusha mbezi beach, kampuni za Alpha brand school, cleaning and supper dealer wa Voda. Mr Lowassa we are not stupid as you think, and dont event try to tell us is your son we know the boy ............ AJisafishe kwa haya machache ndio aanze hii desparations zake kutafuta urais at any cost.
 
LEO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI:WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema kuna haja ya kutathmini upya mfumo wa elimu nchini, ili kuona kama bado unafaa au la.Alisema hatua hiyo inapaswa kufanywa sasa kabla mambo hayajaharibika zaidi na kwamba anaamini kuwa tangu mfumo uliopowekwe enzi za Mwalimu Nyerere, kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.

Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ofisini kwake jijini Dar es slaam.‘’Mimi nasema kuwa sasa wakati umefika kama taifa. kuunda tume ya elimu, ili kuangalia na kupitia mfumo wote wa elimu, kuangalia mitalaa yetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, kuangalia ubora wa elimu hiyo, vitabu gani vitumike, maslahi ya walimu, yaani kwa ujumla tuangalie upya kuhusu mfumo wa elimu yetu.’’alisisitiza Lowassa.Lowassa alipendekeza kuundwa kwa tume ya elimu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ili kwenda na wakati. “Tume hiyo iundwe kuchunguza, kutathmini na kuona, endapo mfumo wa elimu wa sasa unaendana na wakati,”Lowassa alisema nchi zote zilizoendelea duniani, zimekuwa zikifanya hivyo.“Marekani hivi sasa kuna mchakato wa kuangalia elimu inayotolewa kama inaendana na changamoto za karne ya 21,” alisema.Kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kwamba mitalaa ya elimu nchini, haimwandai mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha ya karne hii ikiwa ni pamoja na kujiajiri.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa sana katika sekta ya elimu, hususan awamu hii ya nne ambayo kwa mafanikio makubwa, imeweza kujenga shule za sekondari katika kata zote nchini.Katika mkutano wake mkuu wa nane hivi karibuni mjini Dodoma, CCM ilitoa mapendekezo kadhaa miongoni mwao likiwa la kuboresha elimu nchini.‘’Mimi nilipata bahati ya kuongoza juhudi hizo za Serikali kwa mafanikio makubwa kujenga shule hizo, lakini mafanikio hayo yamekuja na changamoto zake’’alisema.Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafanikio hayo ni ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo, uhaba wa walimu na vitendea kazi vikiwemo vitabu na masilahi kwa walimu.

Alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na wasomi waliobobea ambao wanaweza kazi hii ya kuangalia mitalaa inayotumika ili kuona kama inakidhi haja na matakwa ya karne ya sasa.My Take- Hivi Lowassa anapochukua muda mwingi kuongea haya na vyombo vya Habari ni sehemu sahihi?.

Lowassa ni Mbunge kama wabunge wengine kwa nini haya anayoyasema asingeyaongea Bungeni ambayo ni sehemu muafaka na Bajeti ya serikali ndiko inakopitia?

Mh Lowasa ameongea mambo ya kawaida sana ambayo hata hapa maskani huwa tunayaongea, halafu nastareheshwa na namna alivyoyatamka kana kwamba hajawahi kuwa MWONGOZAJI wa harakati za ukombozi wa Mtanzania.
Kwa kuongezea ni kuwa WAANDISHI KANJANJA, narudia, WAANDISHI KANJANJA wa hapa TANZANIA wanampamba sana huyu Mh Lowasa, laiti angekuwa ni keki basi ingekuwa na ngazi tano kama sio saba, lakini ikumbukwe kuwa hata kama keki itapambwa na kulembwa namna gani, mwisho wa siku lazima iliwe na vijiunga unga vyake vitaanguka sakafuni. Nashauri waandishi makini waachane na hawa viongozi zilipendwa, wafukue talanta ambazo yeye mwenyewe Lowasa anazitaja kuwa "Tanzania inao wasomi mahiri", hii inamaanisha Waandishi makini wawatafute hawa wasomi mahiri wanaosifiwa na Lowasa, kisha waandishi watuelimishe kuhusu umahiri wa wasomi hao, ili tuwafahamu na kisha tuwakabidhi nafasi za kisiasa na kiutendaji ili tuikwamue nchi yetu toka hapa ilipozamishwa KWA MAKUSUDI na ufisadi wa CCM ambao kwa kiasi kikubwa umewapofua macho MAKANJANJA kiasi kwamba fikra zao haziendi mbali na upeo wa shida ya tumbo almaarufu NJAA.
 
niliwahi kumsikia lowassa akiponda dhana nzima ya kilimo kwanza....sasa ameponda elimu
 
LEO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI:WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema kuna haja ya kutathmini upya mfumo wa elimu nchini, ili kuona kama bado unafaa au la.Alisema hatua hiyo inapaswa kufanywa sasa kabla mambo hayajaharibika zaidi na kwamba anaamini kuwa tangu mfumo uliopowekwe enzi za Mwalimu Nyerere, kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.

Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ofisini kwake jijini Dar es slaam.‘’Mimi nasema kuwa sasa wakati umefika kama taifa. kuunda tume ya elimu, ili kuangalia na kupitia mfumo wote wa elimu, kuangalia mitalaa yetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, kuangalia ubora wa elimu hiyo, vitabu gani vitumike, maslahi ya walimu, yaani kwa ujumla tuangalie upya kuhusu mfumo wa elimu yetu.’’alisisitiza Lowassa.Lowassa alipendekeza kuundwa kwa tume ya elimu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ili kwenda na wakati. “Tume hiyo iundwe kuchunguza, kutathmini na kuona, endapo mfumo wa elimu wa sasa unaendana na wakati,”Lowassa alisema nchi zote zilizoendelea duniani, zimekuwa zikifanya hivyo.“Marekani hivi sasa kuna mchakato wa kuangalia elimu inayotolewa kama inaendana na changamoto za karne ya 21,” alisema.Kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kwamba mitalaa ya elimu nchini, haimwandai mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha ya karne hii ikiwa ni pamoja na kujiajiri.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa sana katika sekta ya elimu, hususan awamu hii ya nne ambayo kwa mafanikio makubwa, imeweza kujenga shule za sekondari katika kata zote nchini.Katika mkutano wake mkuu wa nane hivi karibuni mjini Dodoma, CCM ilitoa mapendekezo kadhaa miongoni mwao likiwa la kuboresha elimu nchini.‘’Mimi nilipata bahati ya kuongoza juhudi hizo za Serikali kwa mafanikio makubwa kujenga shule hizo, lakini mafanikio hayo yamekuja na changamoto zake’’alisema.Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafanikio hayo ni ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo, uhaba wa walimu na vitendea kazi vikiwemo vitabu na masilahi kwa walimu.

Alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na wasomi waliobobea ambao wanaweza kazi hii ya kuangalia mitalaa inayotumika ili kuona kama inakidhi haja na matakwa ya karne ya sasa.My Take- Hivi Lowassa anapochukua muda mwingi kuongea haya na vyombo vya Habari ni sehemu sahihi?.

Lowassa ni Mbunge kama wabunge wengine kwa nini haya anayoyasema asingeyaongea Bungeni ambayo ni sehemu muafaka na Bajeti ya serikali ndiko inakopitia?

Jamani! jamani! Jamani!
Huyu edo inaelekea ni msahaulifu sana. Hakumbuki jinsi alivyokuwa anaipiga vita HakiElimu kwa kuikubusha serikali masuala haya ya ubovu wa elimu na misingi yake na akawashtaki kwa rais dhaifu JK! Leo anajitokeza kupiga debe yale ambayo aliwapinga Haki Elimu.

Fisadi edo alishindwa kuuona udhaifu huu akiwa madarakani lakini anauona akiwa nje maana yake ni kuwa hafai kuwa kiongozi kwa kuwa anapokuwa madarakani anakuwa kipofu na kukosa vission.
 
Back
Top Bottom