Lowassa asisubiriwe anogewe na midundo, arejeshwe alipotoka!

Mimi nahitaji cheo kutoka CCM, mtanipa? Ha ha ha ha

Eeeeeh
Hakuna hajuaye

JPM anaowateua huko wengi wao hawana skills tosha anazotaka.. humu mpo wengi na mnayajua ya juu na chini.. hivyo itabidi tu aanze kuchukua wa humu naamini atanogewa na kuwafurahia..

Anzeni kujifungulia acxount LinkedIn pia mtu akiwasechi msomeke na huko

Mimi sipo kwa chama chochote..
Ni mdau tu wa humu.
 
Boss Petro E. Mselewa Nakumbuka toka mwanzo ukufurahi na kutaka Ufipa kumpokea Mamvi.

Siku kadhaa zilizopita, niliandika humu JF hivi:Rais wetu tumeshamjua, twende na midundo yake!. Waliokurupuka katika kuelewa walivyotaka wakaniponda sana. Lakini, niliyaona yaliyokuwa yakitaka kutokea na yameshatokea.Leo sishauri, ila naomba. Nilishashauri:Ushauri wa mwisho kwa CHADEMA: Mfukuzeni Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Itumieni nafasi ya kurudi kwenye mstari wenu!

Kimsingi, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ameamua kujitokeza hadharani na kucheza midundo ya Rais Dr. John Pombe Magufuli. He appreciated and congratulated the national and fruitful deeds of our President. In fact, our President likes to be appreciated. He was sincerely moved.

Katika kumsaidia Lowassa kusema na kutenda kwa uhuru na amani, CHADEMA 'imrejeshe' CCM ili akaungane na 'wenzake' wanaoyaona mema ya Rais Magufuli.Apewe uhuru wake haraka iwezekanavyo kwakuwa alipo si mahala sahihi. Aende akashauri, akasifu na kutoa suluhisho kwa mambo mbalimbali. Asisubiriwe anogewe na midundo akiwa CHADEMA!
 
Pole Mkuu asie Sikia la Mkuu huvunjika Guu

Sheikh Thabit Kombo alitushauri Tuweke Akiba ya Maneno

Zitto alitushauri tusiwaamini Wanasiasa

Jakaya akatushairi akili za kuambiwa changanya na zako

Ukizingatia misemo Hii Mitatu ukaifanyia kazi Siasa za Tanzania haziwezi kukuumiza kichwa

Siasa Duniani kote shida
 
Lowassa pekee hatoshi, Mbowe inabidi ajitathmini yeye kama mwenyekiti na katibu wake Mashinji. Haiwezekani eti chama kikuu cha upinzani kinapoteza wabunge na madiwani eti kwa kununuliwa na CCM, inamaana hata tukiwapa nchi mawaziri wao wanaweza kununuliwa. Inamaana wao hawana namna ya kupambana na hizo rushwa za CCM ?
Mnasusia uchaguzi, halafu baada ya hapo nini kinafuata ?
Toka jamaa alisema hajaribiwi mmeufyata kabisa, kutoa matamko na kurudi pangoni hakuonyeshi ukubwa wa tatizo mnalotaka kutuaminisha lipo kutoka utawala huu.
Kama uhuru na demokrasia ni muhimu ni lazima ipiganiwe, nyie ndio viongozi sasa tupeni hamasa ya kupigania huo Uhuru.

Kupambana na CCM ya sasa kunahitaji mtu mwenye uthubutu, labda Mbowe aliweza kupambana na awamu ya Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania, ila hii ya kazi tu ni mchezo mwingine kabisa !
Wananchi wapo nao sasa ccm kwa sifa zake za ufisadi na rushwa wanaona ndio sala si ndio maana nchi imefiriska kwa rushwa
 
Mara ya kwanza " huyu ni fisadi papa". Mara pili " huyu si fisadi na anafaa kuwa rais wetu, na kama kuna mtu ana ushahidi wa ufisadi wake aende mahakamani". Mara ya tatu "huyu bwana ni selfish sana". Mtu mwenye kutamka maneno ya namna hii kuwaamnisha wananchi wenzake ni lazima apate hukumu ya laana ya Mungu akiwa hapa hapa duniani.
 
Habarini wanajamvi wenzangu ? Poleni na majukum ya kulijenga taifa nianze kwa kukumbusha tu lile swali kililoachwa na katibu mkuu mahiri wa CHADEMA Dr Slaa je Lowassa ni asset ndani ya chama au liability?

Swali hili lilipuuzwa sana lkn lait wanachadema wangelitilia maanani leo sauti za bundi wa mpasuko zisingekuwepo CHADEMA Dr alijenga hoja mbali mbali zikiwemo ujio wa Lowassa chama kimeacha kujijenga kinamsifia mtu mmoja pia watu waliokipigania chama wametupwa wanathaminiwa waliohamia na upepo wa Lowassa pia ajenda ya chama ya kupambana na ufisadi ilikufa rasmi alipokuja mtu huyu?

Leo nawauliza wanaufipa kwa sauti ya Dr is Lowassa an asset or liability? Ifike wakati mwenyekiti wa chama na kamati kuu yote iliohusika wajiuzulu wapishe vijana watakaotengeneza chama bora chenye ajenda ya kusimamia leo CHADEMA baada ya mh Lowassa kumpongeza Rais kwa maendeleo anayofanya anaonekana hakifai chama ukweli utamuweka mtu huru.

Magufuli kafanya kazi iliotukuka mpongezeni na mnapoona anakosea mpeni ushauri nchi yetu sote tuijenge bila kugombea fito, bunge ni moja uchama kwenye bunge muufute.
 
He is neither an asset nor a liability. Ni mwanasiasa mbobevu ambaye hana permanent friend or enemy, but interests (nafikiri kwenda ikulu).

Kwenye game yoyote pamoja na siasa fanya mambo yafuatayo:

1. Don't take sides, put your personal interests first; and

2. Don't care what a brother does for a living, for as long as his interests does not conflict with yours.
 
Niliwahi kutoa ushauri huu kwa Lowassa

Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!
  1. Akijiuzulu ataeleweka tuu, kitendo cha kwenda ikulu bila taarifa ni kujiuzulu tosha, bado kutangaza tuu, na kurejea CCM.
  2. Lowassa baada ya kushindwa uchaguzi wa 2015, he is not an asset, he is a liability, hivyo hata akijiuzulu, no one will loose and no one will gain, just pain and regrets.
  3. Status yake kwa jamii itabaki high, well respected kwa sababu ameonyesha he can dare, a dare devil who can take the bull by its horn!. Chadema watamuheshimu, CCM watamuheshimu, na Watanzania, tutamuheshimu, he tried.
Paskali
 
In the beginning he was such a big asset ila kwa sasa ni liability amekuwa mbinafsi amesahau ilenyomi, amesahau waliomdekia barabara, amesahau pamoja alikuwa anatetemeka kama kuku mwenye kideri lakini watu walimkubali hivyohivyo. Naona ile albadir inawakuta wengi sana
 
Niliwahi kutoa ushauri huu kwa Lowassa

Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!
  1. Akijiuzulu ataeleweka tuu, kitendo cha kwenda ikulu bila taarifa ni kujiuzulu tosha, bado kutangaza tuu, na kurejea CCM.
  2. Lowassa baada ya kushindwa uchaguzi wa 2015, he is not an asset, he is a liability, hivyo hata akijiuzulu, no one will loose and no one will gain, just pain and regrets.
  3. Status yake kwa jamii itabaki high, well respected kwa sababu ameonyesha he can dare, a dare devil who can take the bull by its horn!. Chadema watamuheshimu, CCM watamuheshimu, na Watanzania, tutamuheshimu, he tried.
Paskali
Sasa hivi hataeleweka trust me
 
Siku kadhaa zilizopita, niliandika humu JF hivi:Rais wetu tumeshamjua, twende na midundo yake!. Waliokurupuka katika kuelewa walivyotaka wakaniponda sana. Lakini, niliyaona yaliyokuwa yakitaka kutokea na yameshatokea.Leo sishauri, ila naomba. Nilishashauri:Ushauri wa mwisho kwa CHADEMA: Mfukuzeni Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Itumieni nafasi ya kurudi kwenye mstari wenu!

Kimsingi, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ameamua kujitokeza hadharani na kucheza midundo ya Rais Dr. John Pombe Magufuli. He appreciated and congratulated the national and fruitful deeds of our President. In fact, our President likes to be appreciated. He was sincerely moved.

Katika kumsaidia Lowassa kusema na kutenda kwa uhuru na amani, CHADEMA 'imrejeshe' CCM ili akaungane na 'wenzake' wanaoyaona mema ya Rais Magufuli.Apewe uhuru wake haraka iwezekanavyo kwakuwa alipo si mahala sahihi. Aende akashauri, akasifu na kutoa suluhisho kwa mambo mbalimbali. Asisubiriwe anogewe na midundo akiwa CHADEMA!
Harejeshwi mtu hapa.Hasira na mihemko si ruhusa.Busara na hekma zaidi zinahitajika.
 
E bwana tena midungo yenyewe ni ile kutoka vijiji vya Nakapanya na nanguruwe kabisa nilikua sijui kama hawa jamaa moja ni mmasai na mwingine ngosha wanajua kucheza TODE!!!!!
 
Back
Top Bottom