Nyanya mbichi
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 3,716
- 2,220
Lowassa pekee hatoshi, Mbowe inabidi ajitathmini yeye kama mwenyekiti na katibu wake Mashinji. Haiwezekani eti chama kikuu cha upinzani kinapoteza wabunge na madiwani eti kwa kununuliwa na CCM, inamaana hata tukiwapa nchi mawaziri wao wanaweza kununuliwa. Inamaana wao hawana namna ya kupambana na hizo rushwa za CCM ?
Mnasusia uchaguzi, halafu baada ya hapo nini kinafuata ?
Toka jamaa alisema hajaribiwi mmeufyata kabisa, kutoa matamko na kurudi pangoni hakuonyeshi ukubwa wa tatizo mnalotaka kutuaminisha lipo kutoka utawala huu.
Kama uhuru na demokrasia ni muhimu ni lazima ipiganiwe, nyie ndio viongozi sasa tupeni hamasa ya kupigania huo Uhuru.
Kupambana na CCM ya sasa kunahitaji mtu mwenye uthubutu, labda Mbowe aliweza kupambana na awamu ya Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania, ila hii ya kazi tu ni mchezo mwingine kabisa !
Mkuu samahani wewe binafsi umepambanaje na CCM au wewe ni Mwanaccm?