VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Hapa siropoki. Naandika facts. Nasema baada ya tafakuri ya kutosha. Nimefanya tafakuri,pamoja na kiburi mashuhuri cha kichama, na kugundua kwa kuona na kusikia kuwa Lowassa atashinda uchaguzi wa mwaka huu. Ninaposema hapa ninahuzuni kubwa kwa chama changu. Ninausema ukweli huu mchungu kwangu kama kada mzoefu na hata nisiyemkubali Lowassa. Lakini,wacha niseme. Atabezwa lakini ukweli u wazi.
Lowassa atashinda. Kwanza, ana wapigakura. Pili,ana walindakura. Tatu, ana mfumo wenye mvumo tangu 2010. Amejiandaa na kuandalika. Hakika,Lowassa ana ushawishi na ufuasi mkubwa ndani na nje ya CCM;ndani na nje ya upinzani ambapo ndipo alipo. Kilichobaki,kama njia ya kumkwamisha ni kumshtaki tu kwa makosa ya jinai. Kumshtaki kutadhihirisha 'uchafu' wake tunaousema na kuutegemea kichama. Amasivyo, Lowassa hazuiliki kwenye boksi la kura.
Lowassa sasa ni mpinzani. Anapingana na chama tawala. Naye ameruhusu kushtakiwa kama kuna ushahidi wa Richmond na kashfa nyinginezo ambapo alitajwatajwa. Kwakuwa amejiunga na akina Dr. Slaa, Mbowe, Lissu, Maalim Seif, Juma Duni Haji, na wengineo waliozoea kushtakiwa naye ashtakiwe kama kuna ushahidi. Lowassa hana tena ulinzi na kinga ya kichama kama zamani (kama uliwahi kuwepo). Nini kikwamishe tena ikiwa yeye ni mkosaji na ni mpinzani?
Wapo walio CCM ambao watapiga kura kwa Lowassa. Wapo humu kimaslahi tu. Wapo watakaompigia 'kura za huruma' asiposhtakiwa. Wapo wanaohama chama sasa,wakihama na wafuasi wao ima kiakili au kimwili. Chama kinatikisika.Chama kinapasuka ingawa,kisiasa, inatupasa kujikaza kiume. Akikusanya wa humu, wa mle na wale walio huru anashinda. Hatahivyo, mpambano wa Oktoba utakuwa wa karne!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam