Lowassa apata zaidi ya wadhamini Elfu hamsini jijini Mbeya

Lowassa apata zaidi ya wadhamini Elfu hamsini jijini Mbeya

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,078
Siku ya jana ilikuwa ni shangwe, Nderemo na Vifijo kwa wapenzi wa CCM wanaomuunga mkono Edward Lowassa katika mbio zake za Urais ndani ya CCM katika mkoa wa Mbeya baada ya kumpa mapokezi makubwa na zaidi ya wanaCCM ELFU HAMSINI kumdhamini kwa kutia saini fomu yake ya kuomba kugombea urais.

Hii ni rekodi mpya kabisa kwa Lowassa kupata wadhamini, ambako rekodi ya juu aliyoweka hapo kabla ilikuwa mkoani Kilimanjaro ambako alipata zaidi ya wadhamini Elfu 37.

Ikumbukwe kuwa Mbeya ni Ngome kuu ya Mark Mwandosya ambaye naye anaomba kugombea urais.

Source:ITV Habari.
 
hao mashabiki wengi walinunuliwa ili waonekane wanampa support.
vijana wangu wa boda boda jana wamenipa mauzo mapema sana. nilipowauliza leo vipi tena?
wakanambia leo kuna ulaji nje nje.! tumeshapewa chetu na mafuta juu
 
Wanaohitajika ni kama 90 tu. hao wengine ni mbwembwe za mafisadi
 
hao mashabiki wengi walinunuliwa ili waonekane wanampa support.
vijana wangu wa boda boda jana wamenipa mauzo mapema sana. nilipowauliza leo vipi tena?
wakanambia leo kuna ulaji nje nje.! tumeshapewa chetu na mafuta juu
Na huu ndo mchezo anaocheza Lowasa na mawakala wake. Wanadhani umaskini unaondoka kwa kuwapa vijana wa bodaboda vijisenti
 
Lengo ni kuwatisha wengine ili yeye aonekane kuwa anapendwa sana

Siyo kuwatisha tu,si kanuni inazuia mtu mmoja kudhamini zaidi ya mtu mmoja?kama ndivyo,anachofanya ni kutaka wengine wakose aonekane babu kubwa kumbe hovyo kabisa.mafisadi yana mbinu sana ya maigizo na ukichanganya na elimu yake ya filamu hapo lazima chama chake kiwe makini.mtu anayeungwa mkono na mafisadi wenzie mtakuwa salama akiingia ikulu?rostam awe waziri,karamagi,chenge,tibaijuka,bashe,serukamba,akumbukwe mtoto wa fisadi kingunge, etc.kazi ipo.
 
mlikuja na tuhuma ufisadi wananchi wameipotezea,ugonjwa Edo anapasua anga,ukanda imekosa mashiko,je mnalipi tena?
 
Pamoja na Lowassa kukusanya umati mkubwa wa watu alipoondoka,wapambe wake walibaki wakakabwa na wananchi waliokuwa wanadai wapewe chao,suala hilo lilikuwa linajadiliwa leo asubuhi na kituo cha Bomba fm.
 
mtalialia sana mwaka huu,Edo kawashika

Mbeya kaacha madeni mwambieni akalipe kwanza,safari hii wananchi hatutakubali kulizwa na Lowassa kwa mara nyingine tena.
 
Oh alitembeza ela balaaa elfu 40, 30, 20 zilitolewa balaaa madereva bodaboda ndo walifaidi sn
 
Back
Top Bottom