Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Hakuna jipya kabisa sasa anauliza swali juu ya Dowans anasema hana majibu,du kazi ipo nyie Magamba
 
"I think this is enough for your stomach"... kwi kwi kwi kwi kwi.... eti kamaliza? sa si angeandika kwenye karatasi tu akawasambazia waandishi, yaani kaitisha waandishi mpaka huko alikokuwa kwa hicho alichoongea? Huyu jamaa kaishiwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
"I think this is enough for your stomach" watu matumbo yalikuwa yanaunguruma ndiyo maana kamanisha hivyo, cha maana alichoongea ni hicho cha vijana na ajira, ni bomu haswa
 
Wakati wa maswali ila naona hawa radio five wamerudi studio kunani . Hope mkuu invisible anataendelea kutuupdate . Hamna cha kujivua gamba wala nini, sijui kama huyu jamaa atajisafisha mhhhhhhhhhh

Mimi sijaelewa kajisafishaje hapo!
 
Akiwa rais low-hasa nina kila sababu ya kujipigilia ile pollonium ya mwakyembe!
 
Jamani sijaelewa kabisa promo yote ile aje kusema hayo tu haiingii akili hata kidogo labda anaendelea kupima upepo kabla hajaropoka.
 
anajitahidi kujisafisha lakini wapi . Nimeamini siasa ni mchezo wa mabavu zaidi ya rugby
hamna cha kujivua gamba wala nini

Kama kujisafisha kwenyewe ndiko huku basi ametufanya vipofu na wajinga wasiojua maana ya kuwa safi. Afadhali angekaa kimya kwani hakuna jipya aliloongea zaidi ya kundeleza tabia za kimabavu za kutojibu maswali nyeti ambayo majibu yake ndo wengi wetu tuliyatarajia. Huo urais akatafute kwa mazezeta ila kwetu ambao bado tunahitaji majibu kuhusu kashfa zinazomhusu apati kitu.
 
anaweza akawa anadhani kuwa Watz wa mwaka juzi ndio wa leo lakini kama kweli ndiyo hayo aliyoyasema, ndio 'law of diminishing return' inafanya kazi.
Sijui atakwenda kesho/jumamosi kuattend 50th Anniversary ya UDSM!!?
Huyo bwana hana jipya, naona hakuna kitu cha maana alichoongea, ni mambo yale yale ya kulalamika kwa kuchonganishwa na rais!. Anawapotezea watu muda wao kwa hizo pumba zake. Anataka watanzania wamuonee huruma kwa madhambi yake. Ni bora aseme tu kwamba anaanza kampeni za urais 2015.
Nilisema kuwa hana lolote la maana
 
"I think this is enough for your stomach" Hapo jamaa alikuwa anawashtua washkaji kuwa hakuna 'bahasha za kaki' kwi kwi kwi
 
Jamani sijaelewa kabisa promo yote ile aje kusema hayo tu haiingii akili hata kidogo labda anaendelea kupima upepo kabla hajaropoka.
Nadhani kuna kitu kazuiliwa. Alikuwa kishakaa ili aanze kuongea mapema, akaondoka ghafla. Yawezekana alipigiwa simu na kupewa maelekezo tofauti? Matarajio ya wengi yalikuwa aongelee masuala mengi, Richmond/Dowans, hali ya usalama a nchi, afya yake (baada ya kudaiwa kuwa alikuwa nje kwa matibabu) n.k

Alichofanya kimenishangaza, not expected at all
 
Tatizo Magamba wengi walikaa mkao wa Kushangilia Mtu Kujivua Gamba! Dah la Chenge liko Kiunoni ila la Huyu jamaa ndiyo kwaaaanza hata halina Habari kwamba linatakiwa Kuvuliwa LoL! Ngoja Malale Sugu aje hapa na Upupu wake
 
Kweli huyu jamaa ana roho ngumu aisee
Ndio hayo alioongea?

Alisema atatoa yaliyoko moyoni mbona sijayaona kwani yote aliyosema kila mtu anayajua na hakuna jipya. Hivi anafikiri urais unapatikana kirahisi hivi? Kama anataka kujua jinsi mind set za waTZ kuanzia mijini hadi vijijini zilivyobadilika asubiri 2015. Kama hajajiandaa kama walivyoshauriwa na Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba basi asubiri kupata stroke 2015
 
"I think this is enough for your stomach" Hapo jamaa alikuwa anawashtua washkaji kuwa hakuna 'bahasha za kaki' kwi kwi kwi. AU ni msg kwa JK kuwa sasa ni zamu ya wengine ushakula inatosha???
 
Back
Top Bottom