Naomba msome hii ArticleDAWASCO wamkataa Mkurugenzi wao...
2008-03-22 09:41:24
Na Mashaka Mgeta
Wafanyakazi wa Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wao, Bw. Alex Kaaya, wanayedai kuwa `aliwekwa` madarakani na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, aachie ngazi kwa kushindwa kuendeleza kampuni.
...``Alituahidi kutupatia viwanja kwa kila mfanyakazi, kufanya mikutano kila baada ya miezi mitatu, kutuletea maisha bora ili tumudu kuwasomesha watoto wetu, hajatekeleza hayo yote,`` alisema.
...``Hata hivyo, Bw. Nkakatisi, aliwataka wafanyakazi hao kufuata sheria, kanuni na taratibu, ili kupata suluhu ya kero zinazowakabili.
Bw. Nkakatisi, aliyekabidhiwa risala ya wafanyakazi hao, alisema hatua yoyote itakayokuwa kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizopo, itaashiria vurugu na hivyo kuwafanya wasifikie malengo yao...
SOURCE: Nipashe
imetoka kwa Nipashe 22/03/08
Source links: http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2008/05/10/114077.html`Mapokezi ya Chenge aibu`
2008-05-10 11:37:18
Na Pendo Fundisha,PST, Mbeya
Baadhi ya wakazi wa Mbeya na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, wamelaani mapokezi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge (CCM) na wanachama wake kwa madai kuwa yanakidhalilisha chama hicho na kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete.
Walisema hakuna sababu za msingi za kuwafanyia mapokezi makubwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanazorotesha juhudi za chama hicho na serikali katika vita yake dhidi ya ufisadi.
Mapokezi ya aina hiyo ni ya pili kufanyika baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake baada ya kuhusishwa katika kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond iliyodaiwa kupata zabuni kwa njia ya utata.
Baada ya kujiuzulu kwake Februari mwaka huu, Bw. Lowassa alifanyiwa mapokezi makubwa jimboni kwake Monduli, mkoani Arusha.
Bw. Chenge alijiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu mapema mwezi uliopita, baada ya kufichuliwa kwa habari kwamba anamiliki zaidi ya Sh. Bilioni 1.2 ambazo zimehifadhiwa katika akaunti moja nje ya nchi. Fedha hizo zinadhaniwa kuwa zilipatikana kifisadi katika \'dili\' la ununuzi wa rada ghali ambayo kimsingi Tanzania ilikuwa haiihitaji.
Baada ya kujiuzulu Bw. Chenge wiki hii alikwenda jimboni kwake na kupokelewa na msafara mkubwa wa magari na wapiga kura wake wakiwemo makada wa vyama.
Wakizungumza juzi jioni walipokuwa wakiangalia taarifa za habari katika televisheni mbalimbali zilizokuwa zikionyesha mapokezi hayo yaliyohudhuriwa na baadhi ya makada wa CCM wakiwa katika makundi, walidai huo ni udhalilishaji wa chama hicho na viongozi wake.
Wakiongea na PST baadhi ya viongozi hao walidai kuwa imekuwa ni kejeli kwa serikali pale viongozi wa ngazi za juu waliokumbwa na tuhuma za ufisadi na kujiuzulu na kukimbilia katika majimbo yao kujisafisha.
``Kwa kweli wananchi, hususan wanachama wa CCM mnapaswa sasa kugeuka na kuangalia ni nini kinachofanywa na viongozi wa ngazi za juu, na si tu kujipanga katika barabara na ofisi za chama kwa ajili ya mapokezi ya watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Mnajidhalilisha kwa kunufaisha mafisadi na nyinyi wananchi wenye maisha duni mkizidi kupandishiwa gharama za maisha,`` alisema kiongozi mmoja.
Walisema wananchi walikuwa wakisubiri kauli ya serikali kupitia kwa Rais Kikwete dhidi ya hatua za makusudi zinazochukuliwa dhidi yao, lakini kila kukicha wanawasikia watuhumiwa wakikimbilia majimboni kwao na vyama vyao vikiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi na kwenye mikutano ya hadhara.
Naye mwananchama wa CUF, mkazi wa kitongoji cha Majengo, Bw. Augustino Amani, alisema serikali ilipaswa kufumbua macho na kuwaeleza wananchi hatma inayochukuliwa dhidi ya watu wanaotuhumiwa na ufisadi.
Alisema kwa sasa serikali inapaswa kuwa wazi kwa wananchi na si kuwanyonya kwa kuwapandishia gharama za maisha kutokana na gharama za bidhaa hususan, mafuta, mazao ya chakula kama mahindi na kumfanya mwananchi mwenye kipato cha chini kushindwa kumudu kupanda kwa gharama hizo.
Ni moja ya viashiria kuwa watanzania bado hawaelewi kitu, wanahitaji kuelimishwa. Wanasiasa kambi ya upinzani wana kazi ya ziada. Yaani Bariadi wamenishangaza kweli as kwa kujua kuna UDP wengi basi mambo yangekuwa tofauti na wangeweza kumhoji vijisenti na angeshindwa kujieleza wangempiga chini kuwa sio mbunge wao;badala ya kuwawakilisha anawaaibisha. Kazi ipo 2010
Rev. Kishoka,
Ajabu kubwa wakiandamana Machinga serikali nzima inatishia kufanyiza lakini maandamano ya kuwafariji Mafisadi yanaungwa mkono na jeshi letu...
Ebu tujiulize hicho kibali cha kuandamana kumkaribisha fisadi kilitolewa na nani ikiwa Fisadi kwa maana ya matumizi ya neno hili ni Adui wa wananchi.
Fisadi = Mhujumu uchumi
Ngosha,
Si umesikia Katibu Mkuu akisema ni ruksa kuandamana?
Lakini kama nilivyosema awali kwenye ile thread ya divided perspective, what is wrong huko vijijini? au ni vitisho kutoka kwa viongozi na woga wa wananchi ulioambatana na "unyonge na Umasikini" ndio unafanya Wananchi waendelee kuunga mkono "watuhumuwa" wa Uhujumu uchumi?
tuuukubali ukweli, waliomshangilia chenge na lowasa walifanya hivyo kwa njaa zao, tunaambiwa kuwa yale magari yaliyoko kwenye msafara yanapewa mafuta toka kwenye akaunti ya vijisenti, kule bariadi kila mahali alipohutubia ngombe alichinjwa watu wakala bureee, ni mwanakijiji gani ataacha kujitokeza kupewa nyama ya bure, nyama anayokula mara moja kwa mwezi au sikukuu kama krismasi? mafisadi wamenunua nchi, wananufaika na umaskini waliowatengenezea wananchi, BADO SAFARI NI NNDEFU
may be hao wanavijiji hawajui thamani ya hizo pesa, wanadhani ni shilingi millioni moja ndio maana wanamwona bado anafaa, wananchi bado hawajaelimika na wataendelea kuwasifia tu, ooh mbunge wetu ana magari ya kiasi kadhaa, ana majumba mangapi.....bila kujiangalia wao wanahitaji kuwa na nini kimsingi
Huko vijijini ambako ndio asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi bado tuna matatizo makubwa sana ya kuwafahamisha hawa wenzetu kuhusiana na uharamia wa hali ya juu unaofanywa na mafisadi mbali mbali akiwamo fisadi Mkapa.
Na viongozi walio madarakani nao ni dhaifu mno labda kutokana na wao kuwa mafisadi au kuwaogopa mafisadi. Kikwete angekuwa kiongozi imara asingeruhusu Chenge kwenda kwenye jimbo lake kwa kishindo, hilo lisingetokea lakini tuna picha ya Rais pale Ikulu ambaye hana uwezo wa kufanya maamuzi yoyote kwa maslahi ya nchi.