Lowassa anapuliza huku na huku, CHADEMA na CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa anapuliza huku na huku, CHADEMA na CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwana wa mtu, Mar 1, 2011.

 1. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana JF,
  Kuna habari zinaendelea kunong'onwa chini kwa chini kwamba Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa lazima hivi sasa anatoa support kwa pande kuu mbili zinazopingana kisiasa CCM- ianyoongoza serikali rasmi na CHADEMA inayoongoza serikali nje ya ofisi.

  Taarifa zilizopo zinajikita katika hoja zifuatazo;
  1. Kwa kipindi kirefu Lowassa amejionesha, na anaendelea kujionesha kuwa bado ana nia ya dhati ya kuja kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais, na kwa kuwa kwa sasa inaadaiwa anapima upepo, ameanza kutoa support kote kuwili ili kuweza kujenga future yake-hata kama si kwa urais.
  2. Wanadai hivyo wanasema pia kuwa kwa kipindi kirefu haijanukuliwa au kusikika Lowassa akiwashambulia CHADEMA waziwazi, na hata kwa uficho, ukiachia mbali Chadema waliweka mgombea wa ubunge kwenye jimbo lae, lakini hajawahi kuwa-deal uongozi wa juu wa Chadema kuhusu hilo...
  3. Ukiachia mbali kuwa kwa sasa amekuwa akitoa matamko mengi yanayokinzana na misimamo ya CCM, ingawa yaweza kutazamwa kama uleule mkakati wake wa kurejea kwenye safu na kujipanga, lakini mengi ya matamko haya yanadaiwa kuwa kwa namna moja ama nyingine kwenda sambamba na misimamo ya CDM; mfano suala la katiba, tahadhari kuhusu Arusha kabla ya maandamano, jana kaibuka na suala la mishahara ya wafanyakazi..na mengine kama mnakumbuka..

  Ni kwasababu ya hizo hoja, inadaiwa kuwa kumekuwa na juhudi fulani anazifanya ama zimeshafanyika, za kutoa support kwa CDM katika shughuli zake, bila kusahau kuwa bado yuko kwenye chama chake CCM akiwa damu damu na huku akiungwa mkono na wengi sana kwenye vikao vikuu na ambao ndio tumaini lake hapo baadae.

  Maswali ni je, kama habari hizi ni za kweli, kuna athari gani kwa pande zote mbili,..na hasa CHADEMA ambako mtu kama huyu itakuwa ni maajabu kuwa na 'link'...tafadhali tujadiliane hili.
   
 2. S

  Salimia JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh!! Ngoja kwanza niingie kwa job nitarudi maana naona ishaanza kuwa tabu kama mambo yenyewe ni hivi.
   
 3. b

  banyimwa Senior Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hizo tetesi si za uongo hata kidogo. Huyu bwana anadaiwa pia kufadhili maadamano ya arusha na anafanya hivyo kupitia kwa kiongozi mwandamizi wa CDM. Ziko habari kwamba kwa sasa ndiye anayefadhili gazeti linaloonekana kuwa ndiyo mdomo wa CDM na mhariri mkuu wa gazeti hilo sasa ndiye kipaza sauti cha jamaa maana kila siku ya mungu yeye hakauiki humo kwa habari na makala za kumsifia. Ametamka wazi kwamba bora aisaide CDM kama hatapitishwa na vikao vya CCM kuliko kuunga mkono mgombea wa CCM atakayeshinda.

  Lakini tunamwambia wazi kwamba atanunua vikundi vya watu kadiri anavyopenda lakini hawezi kununua mapenzi ktuoka kwa wananchi milioni 45 ambao wanaumizwa na vitendo vyake na vya marafiki zake. Hana chake bwana!
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Everything is possible!mimi nilisikia anaisaidia CUF,NCCR na TLP huoni hajawahi kuvishutumu waziwazi au kwa kificho hivi vyama?
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  He! Jamaa hachoki tu?

  Kweli mkamia maji hayanywi!
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa upande wa Lowasa, naweza kusema ni mkakati mzuri hasa katika harakati zake za kuponya majeraha ya kutemeshwa uwaziri mkuu. Ni mchezo wa kisiasa, ni sehemu ya Propaganda, Propaganda siyo dhambi alimradi humshurutishi mtu.

  Kwa upande wa CCM, hii ni dalili mbaya kutokana na kuwa inajidhihirisha kuwa Lowasa amepoteza matumaini na Mwenendo wa chama chake, na kama raia yeyote basi anaitumia haki yake ya kimsingi kujijengea mustakabali mzuri iwapo mambo yatakuwa mabaya CCM. Ni wajibu wa CCM kuliona hilo na kulifanyia kazi ilhali bado mapema. Wasipuuze.

  Kwa upande wa CHADEMA, kama Lowasa ameamua kujipenyeza kwao, wasimfukuze, wamkaribishe hata kama anakuja kama mpelelezi. Wanachopaswa kufanya ni kujitengenezea namna watakayoweza kumtumia Lowasa indirectly ili ku-achieve malengo yao, ya muda mfupi na hata muda mrefu. Pia wakiwa na kitengo kizuri cha intelligence naamini kabisa yapo watakayoweza kujifunza kutoka kwa Lowasa, mradi wahakikishe hawampi nafasi ya kujipatia wafuasi wasio waaminifu. Ni juu ya CHADEMA na CCM kuwa makini namna ya kudeal naye. Agalau huo ni msimamo wangu kama kweli Lowasa anacheza mchezo huo...
   
 7. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usimshangae lowasa maana ni kada wa cccm,kwa nini usimshangae Dr slaa ambaye Arusha alihutubia mkutano wa hazara na kumsifu Lowasa kuwa waziri mkuu safi na ambaye alitolewa kafara na JK?
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Issue hapa siyo hiyo unayosema wewe. Huyu mtu ni sumu kubwa kwa watanzania, popote atakapohamia. Siyo mtaji wowote wa kisiasa kwa vile yeye ndiye chanzo cha matatizo yote haya ambayo yanatukabili na kujivua gamba lake ili awahadae watanzania kwamba yeye ni safi ndicho tunachokikataa. Yeye ndiye anayehusika na shida za watanzania ambao leo anajifanya kuwakimbilia na kuwatetea au kuwaonea huruma. Hii ni dalili mojawapo ya mnafiki.
   
 9. M

  Msharika JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Msishangae maze! uliza DR Augustino Lyatonga Mrema kuingia kwake Bungeni Pesa alipata wapi. Zilimwagwa toka IGunga na Monduli. Yeye ndiye walishirikiana na Rostam kumrudisha mrema Bungeni. Usishangae na mzee wa kiraracha Dr Akarudisha fadhili.
   
 10. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mtazamo wangu :

  1. Hizo ni sababu dhaifu sana ambazo zinaweza kutumika kumuhusisha na CDM, hata Sumaye anatoa maonyo na mitazamo tofauti na CCM.

  2. Kwa hadhi aliyonayo Lowasa ndani ya CCM,wengi wanamuunga mkono na viongozi wenzake wanamuogopa, hivyo hawawezi kumwambia asitoe maoni yake hadharani. Ni hatari kwa CCM kumuambia chochote maana wanaogopa mpasuko.

  3. Kama hizo tetesi za kuwasaidia CDM ni kweli basi CDM kinakabiliwa na hatari kubwa,heshima ya chama kwa jamii itaharibika. Lowasa ni mtuhumiwa mkuu wa ufisadi nchini, kama akiweza aweke mambo yake yote hadharani kwa wananchi, wananchi wenyewe wapime kama ni msafi au mchafu. Kama atagundulika kuwa ni msafi basi akaribishwe.
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  kama una akili timamu kuwa mwana ccm ni ngumu!huo ndio ukweli
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani Lowassa ana plan B. Anajua asipopata kupitia CCM na ikiwa CHADEMA watachukua dola kutakuwepo na vilio vya kutaka asulubiwe kwa ufisadi wake. Sasa hapa lazima viongozi wa Chadema wawe be careful kwa sababu huyu anaweza kuwa compromise ili asichukuliwe hatua zozote ikiwa kutakuwepo mabadiliko ya utawala. Nisingepokea msaada wake au urafiki wake.
   
 13. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kuna haya maneno niliyoya bold hapa chini:
  ni wakina nani wapo nyuma ya hizi bold nlizoweka..???:thinking::thinking::thinking:
   
 14. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ......huyu jamaa anaajenda zake nyuma ya pazia!!!!
   
 15. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  :A S 112:Lowasaaa????? Mhhhhhhh, hebu ngoja nikaoge kwanza, then nije nisome upya nahisi kama macho yangu yamenidanganya vile:hand::hand::hand:
   
 16. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sijui Nini..hoja hapo ni hiyo iliyoletwa..kama ilivyo kwa waandishi kama watoa taarifa wameomba kuhifadhiwa, unawahifadhi, ili pia wakati mwingine upate habari..kama hoja ingekuwa hao waliosema ingekuwa suala jingine(kwamba habari ni 'wao' na sio 'hiyo hoja')..na ndio maana pia hata wewe watumia jina 'Sijui Nini' badala ya.....
   
 17. e

  ebwana eh Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu lowasa namkubali sana kwa jinsio alivyo weza kutuletea jk na rostam ,akatulete anna makinda,alitupa makamba senior sasa na kwa style ya pekee anatuandalia serukamba na makamba junior kwa ajili ya 2015 na jinsi mitanzania ilivyo najuwa yatakuwa, kwa hilo naomba kumpongeza huyu lowasa
   
 18. b

  beahunja Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapimwe? Hapimwe Uhadilifu Wake? Hapimwe nn? Hivi kweli kuna mtu ana mashaka na Ripoti Dr. Harrison Mwakyembe? Mnataka nn ili muamini jamaa hafai. Hau tunataka kujaribu sumu kwa kuilamba. HILI JAMBO HALIJENGI HATA KIDOGO " TUSIDANGANYIKE NA UZUSHI" Tusimame imara kulinda rasirimali za nchi yetu. " TUSIYUMBISHWE" na kauli au upepo wa kisiasa ambao utanufaisha watu wasiostahili. " KWA VYOVYOTE VILE TUSIPOTE MUDA KUJADILI ILI JAMBO. Kwa manufaa ya nani?
   
 19. H

  Haika JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Watanzania wenye nia, nguvu, uadilifu na elimu ya kutosha, mtazamo chanya, wenye kupenda wanachi, kumuogopa Mungu watakapoisha, au kugoma kugombea urais, nitampa kura yangu Lowasa!!
   
 20. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Tuko pamoja Haika,wakiisha hao wote nami nitampa kura yangu,CHADEMA wasituangushe!!
   
Loading...