Wakuu, Salama.
Leo ndio nineamini kua UKAWA ndio habari ya mjini na hii imejidhihirisha leo.
Ninasema hivyo kwa sababu leo Magufuli ndio anaenda kuchukua fomu NEC lakini cha kushangaza magazeti yote ya leo Habari kuu ni Lowasa, Dr Slaa, Prof Lipumba = UKAWA.
Cha kushangaza zaidi Gazeti mahiri kwa kutoa habari za CCM (UHURU) limetoka na habari inayomhusu Prof. Lipumba (UKAWA) habari ya mgombea wao Magufuli imewekwa kwenye nafasi ambayo ingefaa zaidi kwa Mgombea wa Udiwani au Ubunge kua anaenda kuchukua Fomu.
Nitoe tu shukrani zangu kwa Wahariri wa Magazeti ya CCM & Co. kwa kitendo chao cha kuipa nguvu UKAWA kwani mnadhani mnavyoandika propaganda chafu juu ya UKAWA na Viongozi wake mkijua mnaidhoofisha imekula kwenu! Sana mnazidi kuiweka juu na kuifanya ieendelee kuwa midomoni na akilini mwa wananchi.
Tunashukuru sana kwa hilo.