Lowassa anaishi kama rais nje ya Ikulu

Lowassa anaishi kama rais nje ya Ikulu

Katika mambo ambayo huwa yananifanya nimwone Lowasa ni genius ni ambavyo aliweza kuwageuza waliokuwa wakimtukana na kumkashifu kwa ufisadi na kuwafanya kuwa, watetezi na washabiki wake wa mahaba. Kwa hilo, Lowasa nakupigia saluti.
 
Tunashukuru Kwa TAARIFA Hiyo ILA NA SISI WENYE UCHUNGU WA NCHI HII TUNAISHUKURU SANA, MNO NA KUNAKOTUKUKA KWA SERIKALI KUPITIA MAMLAKA ZAKE HUSIKA KUMALIZA KUANDAA MASHITAKA YA MAFISADI WAKUBWA WA NCHI HII NA SASA MAHAKAMA YA MAFISADI INAMALIZIWA HUKU PIA WALE WAPELELEZI WA UINGEREZA WA SFO NA WAO WAKIWA TAYARI WAMESHAKAMILISHA KILA KITU KUHUSU SAKATA ZIMA LA RICHMOND NA MUDA SI MREFU TANZANIA TUTAHESHIMIANA NA WATU HAMTOAMINI MASIKIO NA MACHO YENU YA NINI KITAKACHOTOKEA. NI VIZURI SANA SASA HIVI AKIISHI KAMA RAIS KWANI SOON ATAISHI KAMA YULE WA IVORY COAST. Naomba Niishie Hapa Tafadhali.

Anaetakiwa kuishi kama Gbagbo wa Ivory coast ni yule wenu wa kisiwani genge lake
 
Sawa tumewasikia. Sasa simameni na mzungushe mikono yenu hewani kwa saa moja mpoze nafsi zenu.
 
EL amebadili siasa za Tanzania kwa 100%.JPM ni zao lake kwa 100%.Kipimo sahihi ni kuwa akiongea ujue chama na Serikali matumbo joto na akikaa kimya kwao ni utata mtupu.Tanzania inahitaji wanasiasa wa viwango vya Lowassa ambao wataifanya Serikali ifahamu kuwa kauli,nia na matendo yao yanafuatiliwa kwa ukaribu.
 
Hao ni vibaraka wa ufipa. wanamliwaza kisaikolojia baada ya kumtapeli mabilion yake na kumuaminisha kwamba anaweza kuiangusha CCM..
CCM ITAKUA MADARAKANI MIAKA 8000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000
ivi kumbe lowasa bado yupo
 
Hili gazeti la nipashe nimelishusha hadhi afadhari hata Tanzania daima
 
makamanda mnatupotezea muda kwa kuleta habari za mtu ambaye alikuwa mgombea urais tu. hiyo ilishapita. si mwenyekiti wa chama wala kiongozi wa namna gani. labda kama kashapewa cheo. tuacheni tupige kazi sasa. Yeye si amekinunua chama mwacheni akijenge mpeni nafasi. chama kilichovamiwa na mafisadi. balaa tupu
 
Kwa waliombali usome hapo chini, je kukutanana na makundi mbalimbali ndio kuishi kama rais nje ya ikulu? Basi hata Mzee Mengi tuseme hivyo?
Lowassa anavyoishi kama Rais nje ya Ikulu
NA MWANDISHI WETU
31st January 2016
B-pepe
Chapa

Edward Lowassa
Licha ya kutotangazwa mshindi wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana, aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amekuwa na ratiba zinazofanana kwa kiasi fulani na Rais John Magufuli, imefahamika.

Kwa mujibu wa matangazo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Lowassa aliyekuwa akichuana kwa karibu na Magufuli katika muda wote wa kampeni za miezi miwili zilizoanza Agosti 21, 2015, alishika nafasi ya pili baada ya kupata asilimia 39.97 ya kura zote halali zilizopigwa.

Magufuli aliibuka mshindi baada ya kupata asilimia 58.46 ya kura hizo na aliapishwa Novemba 5, 2015 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tangu wakati huo ameendelea kusimamia mabadiliko kadhaa katika serikali yake ya awamu ya tano.

Hata hivyo, Nipashe imebaini kuwa licha ya Lowassa kutotangazwa mshindi na kuingia Ikulu, mgombea huyo wa urais wa mwaka jana amekuwa na mwenendo wa matukio yanayofanana kwa kiasi kikubwa na ya kiongozi dola.

Lowassa alipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu akidai alipokwa ushindi na NEC kwavile takwimu zake zinaonyesha alipata asilimia 60 ya kura zote halali.

Katika uchunguzi wake huo uliohusisha baadhi tu ya matukio, Nipasahe imebaini kuwa Lowassa ameendelea kufanya hafla na matukio makubwa kama Rais licha ya kuwa kwake nje ya Ikulu.

“Bungeni kuna mawaziri kivuli… na sasa Lowassa ni kama Rais Kivuli kwa sababu baadhi ya matukio huhusika akiwa kama kiongozi mmoja mkubwa katika nchi,“ mmjoja wa wachambuzi aliiambia Nipashe kwa sharti la kutotajwa jina.

Kadhalika, katika uchunguzi wake, Nipashe imebaini kuwa baadhi ya matukio yanayomfanya Lowassa aishi kama rais nje ya ikulu ni kukutana kwake na wafanyabiashara, kualikwa kama mgeni rasmi na kukutana na Balozi wa Japan.

Pia amewafunda mameya na wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa), mwamvuli wa kisiasa ambao Chadema ni mwanachama wake, kwa kuwapa onyo kuwa wasipotimiza ndoto za wananchi watachukuliwa hatua. Mambo hayo, yamefanywa pia kwa nyakati tofauti na Rais John Magufuli.

ATETA NA MAALIM SEIF
Novemba 13, mwaka jana Lowassa alikutana na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad na kujadiliana naye juu ya mkwamo wa kisiasa wa Zanzibar miongoni mwa masuala mbalimbali.

Lowassa alifanya hivyo baada ya Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kumtembelea kwenye ofisi zake binafsi zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, Januari 24 Lowassa alikutana na Maalim Seif kwa mara nyingine tena mjini Dodoma na kujadili masuala ya Zanzibar, kabla wote kwa pamoja hawajakutana na wabunge wa Ukawa kutoka Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi.

Rais Magufuli aliwahi pia kukutana na Maalim Seif, Ikulu jijini Dar es Salaam na kujadiliana naye masuala kadhaa kuhusiana na hatma ya Zanzibar baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa visiwa hivyo. Kikao hicho cha Rais Magufuli na Malim Seif kilifanyika Desemba 21, mwaka jana.

AMTEMBELEA SUMAYE MUHIMBILI
Januari 11 , Rais Magufuli alifanya ziara ya kwenda kumjulia hali Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Siku mbili baadaye, yaani Januari 13, Lowassa alifanya hivyo pia, akienda kumtembelea Sumaye ambaye walikuwa naye bega kwa bega katika uchaguzi mkuu uliopita baada ya kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutua Chadema kama alivyofanya Lowassa.

APOKEWA KWA KISHINDO NA WAKAZI DAKAWA
Januari 24 Lowassa aliyekuwa njiani kuelekea Dodoma, alikutana kwa muda na wananchi waliomsimamisha barabarani katika eneo la Dakawa mkoani Morogoro.

Lowassa alizungumza kwa muda na wananchi hao na kushangiliwa kwa nguvu kabla ya kuendelea na safari yake.
Lowassa alifanya hivyo ikiwa ni siku mbili tu zimepita (Januari 21, 2016) tangu Rais Magufuli apokewe pia kwa kishindo na wakazi wa Arusha wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Mamia ya wananchi walijitokeza kumsikiliza Rais Magufuli aliyekuwa amevalia magwanda ya kijeshi.

AFUNDA MAMEYA UKAWA DAR
Januari 18, Lowassa alikutana na mameya wanaotoka Ukawa wa Manispaa za Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuzungumza nao masuala kadhaa kabla ya kuwaonya kuwa watatimuliwa iwapo hawatatimiza lengo la kuwatumikia wananchi kwa namna inayotarajiwa, ikiwamo kuinua mapato, kuboresha usafi, kukomesha ubadhirifu kwenye manispaa zao na pia kushughulikia kero ya foleni jijini humo.

Tukio linalofanana na hilo limefanywa mara kadhaa na Rais Magufuli, ikiwamo Novemba 7, mwaka jana wakati alipokutana na makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu ambao aliwapa maelekezo ya kazi huku akiwaonya kuwa atakayeshindwa kwenda na kasi katika kushughulikia kero za wananchi hataachwa.

AKUTANA NA BALOZI WA JAPAN
Januari 18, Lowassa alikutana na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati wa kusaini mikataba ya miradi mitatu yenye thamani ya Dola 204,300 kwa ajili kusaidia Shule ya Kingolwira, Morogoro, Shule ya Muyuni na Kituo cha Afya cha Lutheran kilichopo Arusha.

Rais Magufuli, kwa nafasi yake, ameshakutana pia na mabalozi kadhaa ikiwamo Novemba 30, mwaka jana wakati alipokutana na mabalozi wa China na Korea.

AKUTANA NA WAFANYABIASHARA
Januari 14, Lowassa alitembelewa ofisini kwake, Mikocheni na wafanyabiashara kadhaa wa Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuzungumzia nao masuala mbalimbali.

Tukio kama hilo limewahi pia kufanywa na Rais Magufuli Desemba 3, mwaka jana wakati wa mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara, alipokutana Ikulu na wafanyabiashara wakubwa na kubadilishana nao mawazo.

WASEMAVYO ZAIDI WACHAMBUZI SIASA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, akizungumza na Nipashe, alisema Lowassa ni mwanasiasa mahiri, aliyebobea na anayejua anachokifanya.
Alisema anajitajidi asisahaulike kwenye ramani ya siasa na nyoyo za Watanzania.

"Kwa sasa hana nafasi ndani ya Chadema zaidi ya kutambulika aliyekuwa mgombea urais ambayo siyo nafasi rasmi ilishaisha wakati wauchaguzi mkuu, haendi bungeni, haudhurii vikao vya madiwani labda aalikwe Monduli, atajulikanaje anachofanya ndiyo maana atafuta fursa na nafasi ili aendelee kuwepo ndani ya mioyo ya watanzania," alisema.

Aidha, aliishauri Chadema kuangalia namna ya kumpa wadhifa ndani ya chama hicho ili awe na shughuli za kila siku za kichama na kwamba kama ana nia ya kuimarisha upinzani nchini kwa kutumia nafasi hiyo, atafanya mambo mengi.

Alisema baada ya chama hicho kumpoteza aliyekuwa Katibu Mkuu, Dk. Willbriad Slaa, sasa wanahitaji mtu mwenye mbinu na mikakati kama Lowassa awepo ndani ya uongozi na kufanya shughuli za kila siku.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa, alisema Lowassa ni mwanasiasa wa upinzani na hivyo ana hiari ya kuendelea na shughuli za siasa za kuimarisha chama chake na nyinginezo, hivyo haoni kama kuna tatizo juu ya kile anachokifanya hasa kwa kutambua vilevile kuwa ni waziri mkuu mstaafu.

“Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Lowassa amekuwa kimya hajafanya chochote kikubwa ukilinganisha na wanasiasa wa nchi jirani kama Kenya (Raila Odinga).

Amekuwa akifanya mikutano ya hadhara na shughuli nyinginezo," alibainisha na kuongeza:
"Anachofanya Lowassa ni siasa za kawaida. Lazima akutane na wapiga kura na makundi mbalimbali ikiwa kuiwashukuru wapigakura.”

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema anachofanya Lowassa ni kwa sababu anatambua nafasi yake katika jamii kuwa ana wafuasi wake na wa Ukawa ambao wanamhitaji hivyo ni lazima akutane nao.

“Ni mapema sana kwa sababu mwezi Oktoba mwaka jana, uchaguzi umemalizika hadi sasa tupo kwenye kipindi cha mpito. Kulikuwa na nia ya Ukawa kushukuru wapigakura lakini wamewekewa vikwazo… siyo Rais kivuli,” alisema Baregu.

“Kila mtu ana haki ya kukutana na yeyote au kundi lolote alimradi hajavunja sheria wala kwenda kinyume cha Katiba.”
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Nyumbu mna visa sana, mnalikataa jina lenu la nyumbu?

Kuna jina na kuna uhalisia.

Mngoni akiitwa Ngonyani, hawi nyani.

CCMscrow ni NYUMBU kwa uhalisia. Hilo hamkwepi. Mna akili za NYUMBU KABISA. So meza hiyo kwanza.

Ukirudi nakupa zingine kuthibitisha uNYUMBU wako na wenzio CCMscrow.
 
Tunashukuru Kwa TAARIFA Hiyo ILA NA SISI WENYE UCHUNGU WA NCHI HII TUNAISHUKURU SANA, MNO NA KUNAKOTUKUKA KWA SERIKALI KUPITIA MAMLAKA ZAKE HUSIKA KUMALIZA KUANDAA MASHITAKA YA MAFISADI WAKUBWA WA NCHI HII NA SASA MAHAKAMA YA MAFISADI INAMALIZIWA HUKU PIA WALE WAPELELEZI WA UINGEREZA WA SFO NA WAO WAKIWA TAYARI WAMESHAKAMILISHA KILA KITU KUHUSU SAKATA ZIMA LA RICHMOND NA MUDA SI MREFU TANZANIA TUTAHESHIMIANA NA WATU HAMTOAMINI MASIKIO NA MACHO YENU YA NINI KITAKACHOTOKEA. NI VIZURI SANA SASA HIVI AKIISHI KAMA RAIS KWANI SOON ATAISHI KAMA YULE WA IVORY COAST. Naomba Niishie Hapa Tafadhali.
Wengi tunafahanu jinsi Lowassa na team yake, wanavyojitahidi usiku na mchana kuhakikisha wanamkwamisha mheshimiwa Dk JPM na serikali yake asifikie malengo yake.
Ndio maana pamoja na kutokuwa na wadhifa wowote ule kichama, Lowassa kwa makusudi Rasmi amepiga kambi mjini Dodoma kuhakikisha UKAWA wanamtumikia yeye Ili kulivuruga bunge.

Hofu yake Kubwa ni kivuli chake mwenyewe na hofu ya kutumbuliwa jipu, kwani itakuwa ndio shimo lake la mwisho
 
Kimsingi, Watanzania tunamtambua Lowassa kama Rais, ndio maana hata baada ya CCM kumwibia kura bado tuko naye bega kwa bega!
 
Kama, kama ndio neno la maana zaidi katika mjadala huu wote, mnapojadili likumbukeni sana neno hili
 
Back
Top Bottom