Lowassa amtaka Zitto UKAWA

Lowassa amtaka Zitto UKAWA

Lowassa amtaka Zitto kujiunga UKAWA ili mpambano uwe kati yake na Magufuli.

Mazungumzo Makali yanaendelea namna gani ya kumjumuisha Zitto.

Chanzo: Magazeti ya Leo na Jana RAIA mwema


Lowasa anajua madhara ya kuingia upinzani. Kamwe hataondoka CCM hata kama hatakuwa active kisiasa ila atabaki ndani ya CCM. Swala la Zitto naamini hata Lowassa anafahamu kuwa Zitto ni sehemu ya CCM. Kwa vyovyote vile kina Nchimbi akiwa waziri wa mambo ya ndani atakuwa amemweleza Lowasa jinsi walivyomtumia Zitto kudhoofisha upinzani hivyo hata kama Lowasa angehamia upinzani (japo haitatokea) Zitto angekuwa sumu kali kwa sababu anajua fika jinsi ambavyo yuko upinzani kisanii na kikazi kwa ajira ya CCM na serikali yake.
 
Hukumbuki kauli ya mchungaji Msigwa kuwa Chadema ni kama kanisa la wokovu, halichagui, so kwanini zitto haruhusiwi kanisani (chadema)?

Nataka siasa ya msimamo ninayoweza kuiamini
 
msiwe wasemaje wa vyama ambavyo sio vyenu mtaumia nachoona magazeti wanauchokoza ukawa ili wapewe taarifa sahihi
 
Hukumbuki kauli ya mchungaji Msigwa kuwa Chadema ni kama kanisa la wokovu, halichagui, so kwanini zitto haruhusiwi kanisani (chadema)?

Kanisani akafanye nini wakati yeye ni mwislamu? Kanisa ni kwa wakristo tu.
 
Hakuna Ukweli wowote,,....CHADEMA hawana mpango wa kumchukua Lowasa

Pia ikumbukwe Act ni chama cha lowasa

Kati ya wewe na Mbowe aliyenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima akimkaribisha Lowasa CDM tumwamini nani?
 
Huu sasa utani, kabla hata hajakaribishwa rasmi tayari keshaanza kuongoza Chama kwa maagizo. Akiingia si ndiyo ataanza na kufukuza wanachama, ili abaki na aliohama nao.

Magazeti yanaandikwa na binadamu kama sisi, lkn kuna wakati waandishi huwa wajinga zaidi ya binadamu yeyote!
 
Ila kama ukawa wako tayari kumpokea Luwasa wanashindwaje kumpokea ZZK iwapo kama wote lengo ni moja? C unafiki huo?


Kwani lengo la zito ni kuitoa CCM madarakani?

Watu wengine hata kama hamuelewi je na picha hamuoni?

Jiulize why zito anakomaa na kuvunja vyama vya Upinzani?

Tangu chama chake kianze hakijawahi kuwa tishio kwa CCM na wala hakuna hata mwana CCM mmoja aliyejiunga nacho
 
Kati ya wewe na Mbowe aliyenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima akimkaribisha Lowasa CDM tumwamini nani?

Mbowe hakumtaja Lowasa kuwa anamkaribisha CHADEMA

Mbowe alisema watu wote wanakaribishwa...It was not specifice to Lowasa

Sasa ulitaka Mbowe aseme watu hawakaribishwi CHADEMA.

By the way Lowasa hana nia ya kuja UKAWA....Hizo ni porojo za social media
 
Mbowe hakumtaja Lowasa kuwa anamkaribisha CHADEMA

Mbowe alisema watu wote wanakaribishwa...It was not specifice to Lowasa

Sasa ulitaka Mbowe aseme watu hawakaribishwi CHADEMA.

By the way Lowasa hana nia ya kuja UKAWA....Hizo ni porojo za social media

DSC09866.jpg
 
Nimeisoma mahali na kuona ana point za msingi kumtaka Zitto kama kweli yeye Ngoyai anataka kwenda UKAWA, point yake ya msingi ni kuondoa dhana ya ukaskazini, anaona kama yeye akiwa Rais, halafu waziri Mkuu awe Mbowe au Slaa wote ni kaskazini akaona abadili mwelekeo.....ngoja tusikie wanavyozidi kujadiliana.
 
Kama Lowassa anataka kupewa fursa ya kugombea asiwape wenzake masharti otherwise arudi CCM tuone maana Zitto ni tapeli aubaingie ACT agombee lkn co kubebwa alafu unakuwa na masharti ya kijinga.

Chadema wakimrudisha Zitto kwenye kambi yao na withdraw support yangu kwao

Wewe baada uwithdraw kwa kukaribishwa kundini mtu aliyeujumu uchumi wa taifa hili yeye na genge lake. Wewe unakasirishwa na ZZK ambaye impact yake ndogo kwenye kuhujumu uchumi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom