Thread ya kipuuzi sana hii, Mods iondoeni
Wapuuzi ni wale waliouziana nyumba zetu za shirika la NHC kwa bei ya chee,
Wapuuuzi ni wale waliofilisi migodi ya nchi almasi na dhahabu,
Wapuuzi ni wale walioamua nchi kuwa na bajeti ya ombaomba,
Wapuuzi ni wale walioamua kuua viwanda vyetu vya ngozi,nguo na kamba,
Wapuuzi ni wale walioingia mkataba wa Richmond ulioliingiza Taifa kwenye hasara ya uchumi,
Wapuuzi ni wale waliokwiba fedha za wananchi na kugawana kwenye viroba,wengine wakiwa mahala patakatifu wanastukia zimeingia kwenye account na hawajui za nini?
Wapuuzi ni wale ambao,sauti za wapigakura wao juu ya katiba mpya,waliamua kuwakaba kooni na walipowatenza nguvu,wakaja na igizo la katiba inayopendekezwa,
Haohao,kesho wanakuja na safari ya matumaini ambayo walipokuwa na ari mpya,nguvu mpya,kasi mpya tayari walikuwa wameshindwa kwenye maisha bora kwa kila mtanzania,
Kisha wakathubutu,wakadai wameweza kutumia sanduku la mfuko wa Rushwa nchini na ikiwa watanzania watajichanganya mbele na kwa kuwa wameweza kuchota, basi safari ya matumaini watasonga mbele huku wakichukua chao mapema,
Kwani wamesema " hawaupendi umaskini"