Lowassa amjibu Nape

Lowassa amjibu Nape

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
11,818
Reaction score
18,073
Lowasa amemshangaa Nape kwa kutoa matamko bila vikao vya chama! Amehoji kauli anazotoa zimetokana na kikao kipi cha Chama?

Lowassa amesema CCM anayoifahamu yeye mambo yote hujadiliwa na kuamuliwa na vikao vya chama!

Source: ITV habari kwa saa!
=======================

Siku moja baada katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Nape Nnauye kutoa kauli ya chama hicho kuhusu makundi yanayojitokeza kumshawishi waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kugombea urais, kuwa yanaweza kumkosesha sifa kiongozi huyo ya kuwania nafasi hiyo Mhe Lowassa amejibu kauli hiyo na kudai anashangazwa nayo huku akihoji imetokana na maamuzi ya kikao gani ndani ya CCM.

Mhe Lowassa anatoa kauli hiyo katika muendelezo wa kupokea makundi mbalimbali ya jamii kumshawishi kuwania nafasi urais ambapo safari hii waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zaidi ya 60 na wananchi wa kawaida wamefunga safari kutoka wilayani mbarali mkoa wa Mbeya mpaka mjini Dodoma kumshawishi agombee ambapo amesema kauli ya Nape Nnauye inamshangaza kwani chama cha mapinduzi kina utaratibu wake wa kujadili mambo kama hayo kupitia vikao mbalimbali.

Mhe Lowassa pia akawataka wanaoendelea kumnyooshea vidole kuhusu hatua ya wananchi wenye imani naye kujitokeza kumshawishi awanie nafasi hiyo wasubiri ufike wakati muafaka ili wana-CCM na wananchi waweze kutoa maamuzi yao huku akisisitiza watu hasa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemuhitaji.

Awali kundi hilo la vijana na bodaboda waliosafiri umbali wa kilometa zaidi ya 600 wakiongozwa na kamanda wa UV-CCM wilaya mbarali Ibrahim Ismaili wamesema lengo la safari yao hiyo ni kuungana na watanzania wengine kumtia moyo Mhe Lowassa ashawishike kuwania urais kwani wana imani kubwa naye huku wakidai pamoja na mambo mengine kama alivyoweza kujenga shule za kata nchi nzima pia ataweza kutegua bomu la tatizo la ajira hasa kwa vijana.
 
Lowasa amemshangaa Nape kwa kutoa matamko bila vikao vya chama! Amehoji kauli anazotoa zimetokana na kikao kipi cha Chama?

Lowasa amesema CCM anayoifahamu yeye mambo yote hujadiliwa na kuamuliwa na vikao vya chama!

Source: ITV habari kwa saa!
Nyerere alivyosema kuwa Lowasa mjinga hajakosea kabisa sasa ndiyo naanza kuelewa,

kwani Lowasa hajui kuwa nape ni msemaji wa chama,

Kwani kasema mangapi ambayo hayatokani na kikao au vikao.
 
Kauli ya Nape ni kauli ya Jk.

Lowassa jiandae kuenguliwa.Hivyo vikao unavyoongelea vikikaa kazi ni moja tu nayo ni kuhakikisha unapigwa chini.

Hata hivyo,hii ni laana ili tu CCM iangamie kupitia Lowassa na Kikwete.

Hata Mungu amewachoka na this time around lazima msambaratike kama sio kuhujumiana.

Ama kweli malipo ni hapa hapa duniani.

Mmetutendea uovu mwingi watanzania na sasa mungu kasema yatosha.

Mnara wa babeli unakaribi kuanguka.
 
Nyerere alivyosema kuwa Lowasa mjinga hajakosea kabisa sasa ndiyo naanza kuelewa,

kwani Lowasa hajui kuwa nape ni msemaji wa chama,

Kwani kasema mangapi ambayo hayatokani na kikao au vikao.

Alisema nini na wapi uliponukuu hayo maneno ya Nyerere?? kua EL ni mjinga??
Hata kama Nape msemaji wa chama.. lini walikaa KIKAO hivi karibuni mpaka kufikia Nape kumtamkia maneno EL
Acha ushabiki mandazi wivu unakusumbua si buree weee umetumwa!!
 
Mzee Mamvi anaweweseka hizo hela anazotoa posho angezitunza watoto wake waje wamsadie kwa kumuhudumia atakapokuwa nyuma ya nondo mapema november UKAWA itakapokuwa mjengoni.
 
Nyerere alivyosema kuwa Lowasa mjinga hajakosea kabisa sasa ndiyo naanza kuelewa,

kwani Lowasa hajui kuwa nape ni msemaji wa chama,

Kwani kasema mangapi ambayo hayatokani na kikao au vikao.

Acha mihemuko mkuu utaolewa,
Anatakiwa kueneza kile kilichoamuliwa kwenye kikao na si kuform kwa utashi wa division 4 yake!

Anayoyasema yamejadiliwa ktk kikao kipi? Lini?
 
Tatizo Nape kwenye hili swala pamoja na kuwa msemaji wa chama hayuko natural toka zamani..ndio maana ata kama anafanya kazi yake wengine wanadhani anafanya kwa sababu binafsi!

NB:Hili swala haliwezi kuwasaidia UKAWA kwenda ikulu na wala wasijidanganye ...Rais wa nchi hii hawezi kutoka nje ya CCM..
 
Lowasa amemshangaa Nape kwa kutoa matamko bila vikao vya chama! Amehoji kauli anazotoa zimetokana na kikao kipi cha Chama?

Lowasa amesema CCM anayoifahamu yeye mambo yote hujadiliwa na kuamuliwa na vikao vya chama!

Source: ITV habari kwa saa!

Vita vya panzi furaha ya kunguruuuu😀😀
 
Back
Top Bottom