Lowassa akiwa Rais... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa akiwa Rais...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JF2050, Dec 1, 2011.

 1. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jamaa kaja na style kali ya kumfagilia Lowassa, hii nimeitoa hapa:

  Lowassa; "Mungu Yupo Na Mimi Nitayashinda Majaribu" « Strictly Gospel


  Lowasa Edward Ngoyayi akiwa Rais wa Tanzania mambo 10 yafuatayo yatatokea:

  1. Mfumko wa Bei utashuka kutoka 17% ya sasa hadi 5% ndani ya miaka 5 ya mwanzo
  2. Thamani ya Shiilingi ya Tanzania itaimarika zaidi dhidi ya sarafu za nje hasa Dollar ya marekani na Yuro ya Ulaya.
  3. Shule za Sekondari zote za Kata alizoziasisi zitapata mabweni, Maabara, Vitabu, Walimu, Mdawati na Vifaa vyote muhimu ndani ya Miaka 2 ya mwanzo.
  4. Uchumi utakua kwa kasi kama ya ndege inayotaka kupaa angani kama enzi za Mkapa. Kumbukeni wakati ule wa Mkapa uchumi ulitaka kupaa ila baada ya Mhe. Kikwete kuingia Ikulu, ile ndege iliyotaka kupaa kama alivyosema Mkapa iliamua kuahirisha safari.
  5. Lowasa akiwa Rais wa Tanganyika na Zanzibar muungani wetu utaimarika zaidi. Natamani tuwe na Serikali Tatu. Kama serikali 3 haziwezekani basi Bora tuwe na Serikali MOJA yenye nguvu kiuchumi. Tuwe na Rais aliye na nguvu pande zote visiwani na Bara.
  6. Lowasa akiwa Rais wa nchi hii, Reli ya Kati toka DAR – KIGOMA/MZA itatengenezwa kwa kasi ya hali ya juu. Ndani ya miaka 3 ya mwanzo Reli itakuwa iko saaaafi sana.
  7. Lowasa akiwa Rais wa Nchii hii, uwajibikaji katika ofisi za umma, serikali na Binafsi utaongezeka kwa kasi. Sasa hivi Bara na visiwani uwajibikaji wa kazi umepungua sana. Watu wengi wanafanya dili za fedha tu bila kuchapa kazi. Lowasa si unamjua anavyowaka hapo hapo na kuwawajibisha wazembe bila kusubiri maamuzi ya vikao na taratibu na kanuni za kazi. Ukivurunda hapo ulipo anakuwasha vibao na kibarua kinaota miguu.
  8. Lowasa akiwa Rais, waislam na wakristo wataheshimiana na wataweza kufuata maadili ya dini zao. Rais akiwa Lowasa Makamu wake atakuwa Mwislam na Waziri Mkuu atakuwa Mwanamke mama Anna Tibaijuka (Professor).
  9. Lowasa akiwa Rais, ufisadi utaendelea lakini kazi mahala pa kazi zitaonekana na maendeleo yataonekana kwa haraka na uwajibikaji utaonekana kwa haraka. Kwa sasa ufisadi upo, uwajibikaji hakuna, kuwajibika au kuwajibishwa hakuna. Lowasa akiwa Rais watu siyo kwamba hawatafanya ufisadi wa mali za umma ila naamini nidhamu itakuwepo. Hata kama yeye anasemwa kuwa ni fisadi, lakini kazi zake kama waziri Mkuu tuliziona. Tatizo ni kwamba wengine ni mafisadi tuuuu ambao kazi yao ni kufukuzia dili za pesa kila kukicha, kazi za maendeleo hawafanyi. Kumbuka Mkapa alivyokuwa mchapa kazi. Kuchapa kazi hakumwondoi kuwa fisadi. Lakini watu hawatamsahau kamwe kwani aliweza kuushusha mfumko wa bei kutoka asilimia 40% mwaka 1995 hadi 5% mwaka 2005. Lowasa akiwa Waziri Mkuu Maamuzi magumu ya kuwajibisha wazembe aliyatekeleza na ndiyo maana na yeye aliamua kujiuzuru ilipotokea kashifa ya Richmond.
  10. Lowasa akiwa President wa URT wanafunzi wa elimu ya juu wote watapewa mikopo bila ubaguzi wala bila hata mmoja kubaki kwa visingizio vya bajeti ya serikali kuwa ndogo.

  Unakumbuka alivyoshawishi mabenki mwaka 2007 yafute vikwazo vya utoaji mikopo kwa wajasiliamali waliokuwa wanaomba mikopo ile ya mabilioni ya JK? Mabenki yalikuwa yamegoma yakitaka DHAMANA ZA MIKOPO hiyo iwe viwanja vya nyumba, Lowasa akakataa kwani kulikuwa na dhamana ya serikali.

  Lowasa akiwa Rais, atashawishi Mifuko ya Pensheni, LAPF, PSPF, NSSF, PPF, GEPF, ZSSF iweke utaratibu wa kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu kama alivyoishawishi yote kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma -UDOM. Kile chuo kimejengwa kwa fedha za kutoka Mifuko hiyo ya pensheni nchini na siyo wafadhili. Aidha, atashawishi mabenki yote ya biashara kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wanafunzi wote wanaokidhi vigezo vya kusoma elimu ya juu.

  Hayo ni baadhi tu ya yale yanayotarajiwa ikiwa Lowasa atagombea kuwa Rais na akashinda wapinzani wake wa kisiasa. Lowasa hata kama anatafsiriwa kuwa mchafu ni kwa sababu tu aliamua kujiuzuru. Hii haina maana kwamba wale ambao hawakujiuzulu walikuwa WATAKATIFU. Hivi kuna mtu wezaye kuwa Mtakatifu huku akiwa mwanasiasa?

  LOWASA EDWARD NGOYAYI, SONGA MBELE, MUNGU IBARIKI TANZANIA. HATA KAMA HUTAKUWA RAIS WA NCHI HII, WENGI TUTAKUKUMBUKA KWA MICHANGO YAKO YA MAENDELEO KWA NCHI HII NA WATU WAKE HASA MAKANISA/MISIKITI HATA KAMA UNGEKUWA FISADI WA VIPI?

  LOWASA EDWARD NGOYAYI WEWE NI POOA SANA. UNYENYEKEVU WAKO SIYO TU KWAMBA UTAKUKWEZA BALI PIA UTAKUOKOA MILELE.

  WATU WA KIGOMA TUNAKUKUMBUKA SANA ULIVYOSAFIRI KWA GARI TOKA BIHARAMULO-KIBONDO-KASULU, NGURUKA- UVINZA TABORA ILI KUANZA MCHAKATO WA KUTENGENEZA BARABARA YA LAMI TOKA KIGOMA HADI DODOMA. SONGA MBELE.
   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Anafaa kuliko wengine wanaotajwa kwenye chama hicho, hata hivyo nitampigia kura akiwa mgombea wa chama kingine, la sivyo hata akigombea na kifuu nitapigia kura kifuu.
   
 3. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,378
  Likes Received: 690
  Trophy Points: 280
  nashukuru mungu pia watanganyika hawanunuliwi sana na pesa watakula pesa zako na kesho watasimama kwenye ukweli! lakini swali zuri la kujiuliza! mbona mapema sana! lakini nililozuri zaidi nadhani ameongea na mungu akamwabia na kumuhakikishia kuwa hata kufa kabla hajawa rais.
  inauma jinsi fedha inavyopotosha matakwa sahihi ya uma!
  wakati niko form one head master wangu mmoja namkumbuka kwa jina moja bilalo alisema "kuhisi ni kosa na kuhisiwa ni kosa! kwanini uhisi na kwa nini uhisiwe wewe? kwangu mimi kuhisiwa ni kosa zaidi! hizi kelele za kutokuwa mwadilifu pamoja na kujituma vizuri katika kazi zake hazijaanzia kwenye nafasi ya uwaziri mkuu tu! ameanza mbali sana mtu huyu.
  binafsi nikiwa na uwelewa mdogo sana nilimkubali sana alipo kuwa waziri ofisi ya rais au waziri mkuu sikumbuki vizuri by zati time nilikuwa klaza sana. alijituma vizuri nakumbuka alitoa hata buku mbili kumsaidia mama mmoja aliyekuwa ametoka kujifungua baada ya kumkuta shamba na kelele kibao kuwa haikuwa haki!
  sasa leo kiko wapi? wangapi wamepoteza kazi kutokana na janga la umeme? wamefilisiwa mali zao kutokana na kushindwa kulipa madeni kwa kushindwa kuendesha biashara? ni mengi na sipendi kuwachosha! lakini tunahitaji kufikiri zaidi kabla ya kumwamini mtu huyu! hivi mfano rais akifa leo atahudhuria msiba wakati nafsi yake itakuwa inafikiria kuridhi nchi? binafsi nipo tayari kufa kwa kusema ninayo fikiria japo mimi si mwana siasa ila sintaacha kuwaelimisha watu wasiwe wapumbafu!
  tupaze zauti zetu kwani tunaotegemea watutete wengi watakuwa wamechoshwa na bahasha za vikao zisivyo rasmi na kalamu zao zitaandika habari za upande mmoja
  kidumu chama cha mapinduzi! zidumu fikra sahihi za mgombea urais wa sasa kupitia chama chetu! teheeeee kazi ipo.ningekuwa na gari ningetoa funguo lakini langu jembe la mkono lisilo na mpini nililobebwa na ujumbe usemao" kilimo ni uti wa mgongo"hivyo mimi ni wa kuteseka na umaskini wangu!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,775
  Trophy Points: 280
  Mzahamzaha huu mtakuta mtu yupo magogoni
   
 5. Kitaja

  Kitaja JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 2,656
  Likes Received: 700
  Trophy Points: 280
  Ndugu Chiwa umenena vema. nadhani mtoa mada anataka tuamini kuwa tz hakuna kama EL... hizo ni fikra potofu! fisadi mahali pake ni jela sio ikulu ati!...naomba ninukuu maneno ya Mh. Mwakyembe "hii nchi sio ya mabwege". aliyasema hayo wakati akijibu hoja za watetezi wa EL kuhusu Richmond.
   
 6. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Jamaa Karla hoja za msingi kabisa kwa ufupi hakuna Kama Lowassa
   
 7. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  thought the same
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  I'd prefer Lowasa for presidency than Membe, Makinda, Pinda, Kikwete, and many more CCM members...
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,775
  Trophy Points: 280
  Kaka uko karibu na mrija wa manywele nini?
   
 10. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hakuna haja ya chuki, vijembe na siasa za maji taka ndani ya chama kimoja. Nadhani ikiwa hivi itafaa sana. Uwepo mkakati wa pamoja. Mafahari wawili wawekwe katika zizi moja kisha muafaka ndio njia rahisi ya kupata maridhiano. LOWASA akiwa rais, basi SITTA awe waziri mkuu.

  SITTA akiwa rais, LOWASA nae awe waziri mkuu. Nadhani mambo yatakuwa bambam. Dalili zinaonyesha kuwa wazee hawa wameanza kuchukua jaramba taratibu kwa ajili ya kupokea kijiti. Kama ni kweli.

  Basi nawatakia mbio njema.
   
 11. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Alafu,,,
   
 12. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35

  yaani wewe ni masaburi kila kitu!!!kwa hiyo ccm watashinda huo uchaguzi?acha ujinga!huyo lowaasa wenu ni rais monduli tu!!!
   
 13. f

  firehim Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna rais Hapo. Ufisadi mtupu
   
 14. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #14
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  We kwa akili yako nyembamba kama sindano unadhani chama gani kitashinda? Fyatua akili zako hukooo! zirudishe kicwani.
   
 15. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  pamoja mkuu!!!!!!!!!
   
 16. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kuna watu yaani mpaka kero humu jf aaaaaaaaaaaaah, wasipoandika neno lowassa basi wanawashwa sana . Acheni kuuza utu wenu kwa pesa ambayo haiwezi kukusaidia katika maisha. Ningewaona watu wa maana sana kama mngeleta mikakati ya kuwatoa watu umaskini hapa jf.

  Awe lowasa au sita raisi hakuna cha maana watakachofanya. Rais wa Iran aliulizwa swali na mtangazaji kuwa anadhana aking'atulka madarakani irani haitakuwa na maendeleo? la hasha jibu lake nililipenda , fupi lisilo na maswali, kuwa maendeleo hayaletwi na raisi hata siku moja. Maendeleo yanaletwa na rasilimali mlizonazo, wataalamu, wasomi n.k vikitumiwa vizuri.

  Nchi yoyote duniani ambayo imeshindwa kujali hayo daima maendeleo sahau. Ndani ya CCM sijamwona yoyote anayoitetea nchi hii kuanzia wakulima, rasilimali hadi wataalamu wake. Wote wanawaza lini watapata nafasi waliibie taifa hili tu, hakuna cha zaidi. Waaulize kwa nini wanangangania kuingia ikulu kwa gharama yoyote ile, unadhani wana uchungu na taifa hili, la hasha ni matumbo yao yanawasumbua hamna la zaidi.

  Wamekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30 lakini hakuna jipya walilolileta zaidi ya kutuingiza katika umaskini usio na kikomo. Nawachukia sana watu wanaowatetea hawa nawafananisha na watu waliolala katika wafu.
   
 17. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #17
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yeeees...dats iz the point! Itazuia Mgawanyiko ndani ya CCM..,Na CCM itadumu milele na milele! Kama CCM Kinataka kishinde Uchaguzi 2015 Kirahisi Kiwaunganishe Mafahali Wawili yaani Sitta Na Lowassa! Hii Ndio Njia Pekee
   
 18. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35

  masaburi at work!!!!!!!!!!!kitashinda ccm kwa 92%,lowassa mgombea!!!!!!
   
 19. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #19
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ukitaka raha katika nafsi, we mkere mjinga tu ili usikie maneno yake.
   
 20. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  mungu azid kukubariki!!!!
   
Loading...