Lowassa akabidhiwa rasmi chama, kwafukuta

Kwa sasa ni wazi kuwa CHADEMA kuna jambo kubwa zaidi ya tunavyoona:

i) Jana Mkuu wa Chama cha CHADEMA na aliyekuwa mgombea urais kupitia kundi la UKAWA, E. Lowassa alionekana akiandamana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Znz, Salum Mwalim, katika ziara katika Jimbo la Monduli. Hili si jambo la kupuzwa kisiasa.

ii) Taarifa zilizopo ni kuwa Salum Mwalim ndo alikuwa chaguo la mkuu wa CHAMA kuwa Katibu Mkuu wa chama badala ya huyu aliyewekwa na Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe. Nafasi ya Salum Mwalim kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ili kuwa wazi hasa ukiangalia uzoefu na ukakamavu ambao aliuonyesha kipindi alipokaimu nafasi hiyo baada ya Dr. Slaa kujiengua na chama kwa sababu ya kumsimamisha Lowassa agombea nafasi ya urais na kuanza kumsafisha na kashfa zilizokuwa zinamwandama.

iii) Kitendo cha Lowassa kuanza kufanya kazi na Mwalim ambaye ni katibu mkuu ZNZ kumetafsiriwa kwa namna nyingine na wananzuoni wa siasa. Wapo wanaosema kweli Mbowe aliuza chama kwa Lowassa na kinyume na Katiba ya chama. Wengine wanasema ndani ya Chadema mambo yamekuwa magumu hivyo kila mtu anataka aonyeshee kuwa aliyemtaka ndo anaweza. Wengine wanasema haya ni maandalizi ya Lowassa kuongoza chama kikatiba katika uchaguzi wa ndani ujao. Haya tuache maana ni maono ya watu tu.

iv) Majuzi imeripotiwa kuwa kuna mgogoro mkubwa umekikumba chama hiki pendwa kwa sababu ya Mwenyekiti amefanya kififie haraka katika anga za siasa za sasa. Imejulikana kuwa wajumbe wa mkutano uliofanyika hivi karibuni, walitoa shutuma kali dhidi yake juu ya kushindwa kuongoza chama katika utawala huu wa rais Magufuli, ingawa haikuonyesha wazi nini ilikuwa chanzo. Nyuma pazia inaonyesha wengi wamechoshwa na maamuzi ya Mbowe yasiyoshirikishi pamoja na shinikizo lake la kumkaribisha Lowassa agombee urais bila kupima mbele nini kitatokea.

Kama haya yapo yanatoa taswira mbaya ya chama mbele ya ummaa wa Watanzania na nafasi ya chama katika siasa za usoni. Na ni dhahiri kuwa kwa sasa msadaa wa kifedha wa Lowassa ndani ya chama umepungua, hasa kumtambulisha Katibu Mkuu, wengi wanajiuliza juu ya ukimya wake.

Maana katika mkutano uliofanyika mkoani Mwanza baada ya kuteuliwa na chama ilikuwa kuzunguka nchi zima kumnadi na kuanza kufufua chama upya.
NINA IMANI NA CHADEMA
 
Lowasa ana uchungu sana na Kikwete na baadhi ya wana ccm hawezi kurudi nyuma isitoshe Lowasa hana njaa, kilichomrejesha nyuma mzee mwapachu ni njaa tu .
Na alikuwa bwiii Wakati anaruhudi... Walevi
 
Bora ubadili hiyo ID haikufai maana mwenye jina hilo /sifa hizo hafanani na mpenda uzushi kama unavyofanya hapa

Ofisi ya Katibu Mkuu ndio huratibu ziara zote.

Ben, anachokisema huyu bwana ni kuwa yeye anaamini kuwa mtazamo wako, mtazamo wa marando na mtazamo wa prof baregu juu ya Lowassa ni hasi. Anapata tabu kuamini watu kama ninyi mnawezaje kukaa na kufanyaa kazzi pamoja na mtu mliyetofautiana mitazamo kuihusu jamii? Aidha ungemjibu kuwa wewe huna mtazamo tofauti na Lowassa, mtazamo wenu umeunganishwa na itikadi ya chama. Au ungemjibu kuwa kwenye siasa kuna kukubaliana kutokubaliana huku watu wakiendelea kutoa hoja na hoja nguvu ya hoja hushinda. Sasa ndugu yangu ulivyo mu attack kupitia ID yake, lol,wanasiasa mnatakiwa muwe na 'ngozi' ngumu Ben
 
Lowasa ana uchungu sana na Kikwete na baadhi ya wana ccm hawezi kurudi nyuma isitoshe Lowasa hana njaa, kilichomrejesha nyuma mzee mwapachu ni njaa tu .
Unafikiri uchungu wake unasaidiaje taifa. Maana hata agepata urais angeanza kudili na watu binafsi na si matatizo ya wananchi.
 
hakuna Dili la kununua chama hizo propaganda zilitengenezwa na January Nape na Membe mkalishwa mkakariri pasipo kuchanganya cha kuambiwa na Akili zenu, wajanja wote wanajua kuwa hiyo story ulitengenezwa ili kuwadhoofisha ukawa ma Lowasa kwa ujumla.
Mbona husemi basi chadema walitengeneza kutuaminisha kuwa Lowassa ni Fisadi mkuu.
 
Sasa si wakati wa siasa,kama wanajenga chama waachwe wajenge chama chao na tunaofanya kazi tuachwe tufanye kazi tisubir wakati wa porojo ukifika 2020
Hatutaki chama chetu na upinzani ufe Tanzania, maana ikibaki hivi hatutafika 2020.
 
Umependa avatar au id maana vyote hivyo si mimi. Au umesha utwanga?
hata ukitumia avatar na id fake huwezi ficha personality yako. ndiyo niliyoipenda. unasemaje kuhusu kukaa chini na kuzungumza?
 
Mbona Faiza na genge lako hamueleweki? Kuna kipindi mlisema huyu katibu mashinji ni chaguo la EL mara hii mnasema EL chaguo lake ni Mwalimu. Kiweni na msimamo mnatuchanganya sisi wakosoaji weñu.
 
Harafu mikutano ya hadema sasa hiv mbona haina mafuriko kama ya mwaka jana? Nimeshangaa hata monduli kwao walijaa wanafunzi na wakubwa kidogo sasa mikoa mingine itakuwaje? Mi naona watu wako bize na magufuri ni afadhari muache mnapoteza muda.
 
Lowasa nje ya ccm amekuwa mwiba mkali kuliko alivyo kuwa ndani ya ccm, huko mlimzushia ufisadi na wizi, huku aliko msimtafutie tena jina chafu kama kanunua ni heri nilitegemea mgesema LOWASA KAIIBA CHADEMA NA WANA CHAMA WAKE.
 
Bora ubadili hiyo ID haikufai maana mwenye jina hilo /sifa hizo hafanani na mpenda uzushi kama unavyofanya hapa

Ofisi ya Katibu Mkuu ndio huratibu ziara zote.
Mkuu Ben, msamehe bure huyo. Tatizo maisha magumu sukari kilo moja imefika 7,000 na yeyeanalipwa buku 7.

Lazima wachanganyikiwe
 
Kwa sasa ni wazi kuwa CHADEMA kuna jambo kubwa zaidi ya tunavyoona:

i) Jana Mkuu wa Chama cha CHADEMA na aliyekuwa mgombea urais kupitia kundi la UKAWA, E. Lowassa alionekana akiandamana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Znz, Salum Mwalim, katika ziara katika Jimbo la Monduli. Hili si jambo la kupuzwa kisiasa.

ii) Taarifa zilizopo ni kuwa Salum Mwalim ndo alikuwa chaguo la mkuu wa CHAMA kuwa Katibu Mkuu wa chama badala ya huyu aliyewekwa na Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe. Nafasi ya Salum Mwalim kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ili kuwa wazi hasa ukiangalia uzoefu na ukakamavu ambao aliuonyesha kipindi alipokaimu nafasi hiyo baada ya Dr. Slaa kujiengua na chama kwa sababu ya kumsimamisha Lowassa agombea nafasi ya urais na kuanza kumsafisha na kashfa zilizokuwa zinamwandama.

iii) Kitendo cha Lowassa kuanza kufanya kazi na Mwalim ambaye ni katibu mkuu ZNZ kumetafsiriwa kwa namna nyingine na wananzuoni wa siasa. Wapo wanaosema kweli Mbowe aliuza chama kwa Lowassa na kinyume na Katiba ya chama. Wengine wanasema ndani ya Chadema mambo yamekuwa magumu hivyo kila mtu anataka aonyeshee kuwa aliyemtaka ndo anaweza. Wengine wanasema haya ni maandalizi ya Lowassa kuongoza chama kikatiba katika uchaguzi wa ndani ujao. Haya tuache maana ni maono ya watu tu.

iv) Majuzi imeripotiwa kuwa kuna mgogoro mkubwa umekikumba chama hiki pendwa kwa sababu ya Mwenyekiti amefanya kififie haraka katika anga za siasa za sasa. Imejulikana kuwa wajumbe wa mkutano uliofanyika hivi karibuni, walitoa shutuma kali dhidi yake juu ya kushindwa kuongoza chama katika utawala huu wa rais Magufuli, ingawa haikuonyesha wazi nini ilikuwa chanzo. Nyuma pazia inaonyesha wengi wamechoshwa na maamuzi ya Mbowe yasiyoshirikishi pamoja na shinikizo lake la kumkaribisha Lowassa agombee urais bila kupima mbele nini kitatokea.

Kama haya yapo yanatoa taswira mbaya ya chama mbele ya ummaa wa Watanzania na nafasi ya chama katika siasa za usoni. Na ni dhahiri kuwa kwa sasa msadaa wa kifedha wa Lowassa ndani ya chama umepungua, hasa kumtambulisha Katibu Mkuu, wengi wanajiuliza juu ya ukimya wake.

Maana katika mkutano uliofanyika mkoani Mwanza baada ya kuteuliwa na chama ilikuwa kuzunguka nchi zima kumnadi na kuanza kufufua chama upya.

Kama wewe ni mme, basi una tatizo kwenye hormones zako na kama ni mke bila shaka ni type ya Angelina wa Mrema
 
Harafu mikutano ya hadema sasa hiv mbona haina mafuriko kama ya mwaka jana? Nimeshangaa hata monduli kwao walijaa wanafunzi na wakubwa kidogo sasa mikoa mingine itakuwaje? Mi naona watu wako bize na magufuri ni afadhari muache mnapoteza muda.
Una TV kwako? Hujaona 'mto wa mbu' watu walivyozimia juzi kati?
 
Back
Top Bottom