Lowassa akabidhiwa rasmi chama, kwafukuta

Lowassa akabidhiwa rasmi chama, kwafukuta

Hawana ujanja inabidi wakubali matokeo.

Kila nikimfikiria mtu kama Baregu, Mabere Marando, Ben Saanane uwa najiuliza awa watu wamewezaje kuwa comfortable kufanya kazi chini ya Lowassa? Nabaki kukubali wanasiasa wote baba yao mmoja ni watu wa maslahi binafsi ya matumbo yao. Ni mara elfu tuendelee kuongozwa ni hili zimwi litujualo lililomkabidhi chama mwanamapinduzi Magu.
Kile chama ni cha kitapeli.
 
Kwa sasa ni wazi kuwa CHADEMA kuna jambo kubwa zaidi ya tunavyoona:

i) Jana Mkuu wa Chama cha CHADEMA na aliyekuwa mgombea urais kupitia kundi la UKAWA, E. Lowassa alionekana akiandamana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Znz, Salum Mwalim, katika ziara katika Jimbo la Monduli. Hili si jambo la kupuzwa kisiasa.

ii) Taarifa zilizopo ni kuwa Salum Mwalim ndo alikuwa chaguo la mkuu wa CHAMA kuwa Katibu Mkuu wa chama badala ya huyu aliyewekwa na Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe. Nafasi ya Salum Mwalim kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ili kuwa wazi hasa ukiangalia uzoefu na ukakamavu ambao aliuonyesha kipindi alipokaimu nafasi hiyo baada ya Dr. Slaa kujiengua na chama kwa sababu ya kumsimamisha Lowassa agombea nafasi ya urais na kuanza kumsafisha na kashfa zilizokuwa zinamwandama.

iii) Kitendo cha Lowassa kuanza kufanya kazi na Mwalim ambaye ni katibu mkuu ZNZ kumetafsiriwa kwa namna nyingine na wananzuoni wa siasa. Wapo wanaosema kweli Mbowe aliuza chama kwa Lowassa na kinyume na Katiba ya chama. Wengine wanasema ndani ya Chadema mambo yamekuwa magumu hivyo kila mtu anataka aonyeshee kuwa aliyemtaka ndo anaweza. Wengine wanasema haya ni maandalizi ya Lowassa kuongoza chama kikatiba katika uchaguzi wa ndani ujao. Haya tuache maana ni maono ya watu tu.

iv) Majuzi imeripotiwa kuwa kuna mgogoro mkubwa umekikumba chama hiki pendwa kwa sababu ya Mwenyekiti amefanya kififie haraka katika anga za siasa za sasa. Imejulikana kuwa wajumbe wa mkutano uliofanyika hivi karibuni, walitoa shutuma kali dhidi yake juu ya kushindwa kuongoza chama katika utawala huu wa rais Magufuli, ingawa haikuonyesha wazi nini ilikuwa chanzo. Nyuma pazia inaonyesha wengi wamechoshwa na maamuzi ya Mbowe yasiyoshirikishi pamoja na shinikizo lake la kumkaribisha Lowassa agombee urais bila kupima mbele nini kitatokea.

Kama haya yapo yanatoa taswira mbaya ya chama mbele ya ummaa wa Watanzania na nafasi ya chama katika siasa za usoni. Na ni dhahiri kuwa kwa sasa msadaa wa kifedha wa Lowassa ndani ya chama umepungua, hasa kumtambulisha Katibu Mkuu, wengi wanajiuliza juu ya ukimya wake.

Maana katika mkutano uliofanyika mkoani Mwanza baada ya kuteuliwa na chama ilikuwa kuzunguka nchi zima kumnadi na kuanza kufufua chama upya.
Nini kinakufanya uamini kwamba ndani ya ccm hali shwari?

Lini Magufuli atakabidhiwa Chama cha Mapinduzi?

Baada ya kunyimwa visafeti vya fedha za walipa kodi na hazina mna mpango gani? Mlizoea vya kunyonga, lini mtaanza kuchinja?

Mlijengewa ukumbi mpya dodoma na HSC, ambae ametikisa nchi kwa kulitia hasara taifa (ukwepaji kodi), lakini anaendelea kupeta. Kwanini msianze Kukodisha ukumbi wenu kwa ajili ya shughuli za harusi na kitchen party kuongeza kipato?

Katibu Mkuu tuliyomzoea na mbwembwe yupo wapi, likizo?

Katibu mkuu mpya ambae Mheshimiwa anamtaka atapita dhidi ya Ulega et al?

CCM ya Bulembo na Makamba ipo wapi? Kwanini mwingine uwaziri amekalia kuti, shwari humo ndani?

Mwenyekiti kumtaja taja Lowassa kamati kuu (CCM) kwamba bado ni tishio maana yake nini?

Visasi dhidi ya wale wana ccm ambae mheshimiwa alisema usiku ukawa mchana CCM, mnavilipiza lini? Kiungulia kimeisha?

Cc Lizaboni, MsemajiUkweli
 
Hawana ujanja inabidi wakubali matokeo.

Kila nikimfikiria mtu kama Baregu, Mabere Marando, Ben Saanane uwa najiuliza awa watu wamewezaje kuwa comfortable kufanya kazi chini ya Lowassa? Nabaki kukubali wanasiasa wote baba yao mmoja ni watu wa maslahi binafsi ya matumbo yao. Ni mara elfu tuendelee kuongozwa ni hili zimwi litujualo lililomkabidhi chama mwanamapinduzi Magu.

Mkuu waliosema siasa ni mchezo mchafu hawakukosea?
Kila siku wanatuambia mambo tunayoyajua. wanaahidi mambo ambayo hata hayawezekani pindi chaguzi zikifika ilimradi wapate kula zetu. Wakishapata tu, hawatujui tena. Hukumbuki huyu huyu Lowasa kipindi cha awamu ya nne akiwa waziri mkuu aliwahikuulizwa swali kwenye mkutano kuwa "Mbona Maisha bora kwa kila Mtanzania mliyotuahidi hatuyaoni"? Jibu alilopewa Mwananchi huwezi amini. Kwa hiyo kuwaamini wanasiasa utaumia bure.. unaweza ukapata depression bure
 
Lumumba mmezidi kutia kinyaa,mmekuwa kama mashoga vidole juu na umbea umbea tu!
 
Dr slaa aliondoka na nyoyo za wanachadema original, zimebaki chadema maslah,kifuatacho ni aibu na fedheha ndio kitakacho wakumba
Aliondoka na mioyo yenu lumumba, mfuateni mkamlipie madeni na bili nyingine.
 
Post inapaswa kutafakariwa kwa umakini mkubwa. Pamoja ya kwamba kipendacho roho ni dawa.
 
Sijatoa taarifa ya CCM humu. Ila unaweza eleza umma hicho unachosema.

Kwa sehemu ndogo tu, hakuna kisasi kwa yoyote. Ambaye hakuwa nasi si sehemu yetu.
Nini kinakufanya uamini kwamba ndani ya ccm hali shwari?

Lini Magufuli atakabidhiwa Chama cha Mapinduzi?

Baada ya kunyimwa visafeti vya fedha za walipa kodi na hazina mna mpango gani? Mlizoea vya kunyonga, lini mtaanza kuchinja?

Mlijengewa ukumbi mpya dodoma na HSC, ambae ametikisa nchi kwa kulitia hasara taifa (ukwepaji kodi), lakini anaendelea kupeta. Kwanini msianze Kukodisha ukumbi wenu kwa ajili ya shughuli za harusi na kitchen party kuongeza kipato?

Katibu Mkuu tuliyomzoea na mbwembwe yupo wapi, likizo?

Katibu mkuu mpya ambae Mheshimiwa anamtaka atapita dhidi ya Ulega et al?

CCM ya Bulembo na Makamba ipo wapi? Kwanini mwingine uwaziri amekalia kuti, shwari humo ndani?

Mwenyekiti kumtaja taja Lowassa kamati kuu (CCM) kwamba bado ni tishio maana yake nini?

Visasi dhidi ya wale wana ccm ambae mheshimiwa alisema usiku ukawa mchana CCM, mnavilipiza lini? Kiungulia kimeisha?

Cc Lizaboni, MsemajiUkweli
 
Ulitaka wapime naman gani ili wajue yapi yangetokea mbele zaidi ya katiba ya Wanahci iliyochakachuliwa na zimwi la taifa ccm?

Angeligombwa uraishi Salum Mwalimu, au Slaa, angetangazwa kuwa mshindi kinyume na ilivyotokea mwaka 2010 na juzi kwa Lowasa? Nii lengo la kuchakachaua katiba ya wananch na kusimika utawala kwa nguvu ya dola? Naomb auwe serious.

Wewe ulitaka Lowasa afanye kazi na CHADEMA wote? Mbona hii kazi unfanya imekaa kinyoka zaidi?
Hivi we unaamini kuwa Lowassa alishinda urais?? Mbona wabunge hata 40 hakufanikisha!
 
Hivi we unaamini kuwa Lowassa alishinda urais?? Mbona wabunge hata 40 hakufanikisha!

Tatizo ni kwamba hamna upeo na uelewa wa mambo. Hii ni moja ya pungufu kubwa la Lumumba na utararibu wake to unleash vijana kwenye mitandao ya kijamii kwa ujira bila ya kuwaandaa. Mbona ni kawaida kwa chama cha siasa 'kushinda urais' lakini kikakosa majority ya viti vya ubunge? Fanya utafiti, ukiweza uliza humo humo Lumumba.

Tangia uhuru wa Tanganyika, ingawa uchaguzi wa Rais na Wabunge umekuwa ukifanyika katika kipindi kimoja, uchaguzi wa wabunge na Rais una dynamics tofauti kabisa. Hizi huwa ni chaguzi mbili tofauti. Fanya utafiti, ikiwezekana uliza humo humo Lumumba.
 
Back
Top Bottom