Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Kwa sasa ni wazi kuwa CHADEMA kuna jambo kubwa zaidi ya tunavyoona:
i) Jana Mkuu wa Chama cha CHADEMA na aliyekuwa mgombea urais kupitia kundi la UKAWA, E. Lowassa alionekana akiandamana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Znz, Salum Mwalim, katika ziara katika Jimbo la Monduli. Hili si jambo la kupuzwa kisiasa.
ii) Taarifa zilizopo ni kuwa Salum Mwalim ndo alikuwa chaguo la mkuu wa CHAMA kuwa Katibu Mkuu wa chama badala ya huyu aliyewekwa na Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe. Nafasi ya Salum Mwalim kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ili kuwa wazi hasa ukiangalia uzoefu na ukakamavu ambao aliuonyesha kipindi alipokaimu nafasi hiyo baada ya Dr. Slaa kujiengua na chama kwa sababu ya kumsimamisha Lowassa agombea nafasi ya urais na kuanza kumsafisha na kashfa zilizokuwa zinamwandama.
iii) Kitendo cha Lowassa kuanza kufanya kazi na Mwalim ambaye ni katibu mkuu ZNZ kumetafsiriwa kwa namna nyingine na wananzuoni wa siasa. Wapo wanaosema kweli Mbowe aliuza chama kwa Lowassa na kinyume na Katiba ya chama. Wengine wanasema ndani ya Chadema mambo yamekuwa magumu hivyo kila mtu anataka aonyeshee kuwa aliyemtaka ndo anaweza. Wengine wanasema haya ni maandalizi ya Lowassa kuongoza chama kikatiba katika uchaguzi wa ndani ujao. Haya tuache maana ni maono ya watu tu.
iv) Majuzi imeripotiwa kuwa kuna mgogoro mkubwa umekikumba chama hiki pendwa kwa sababu ya Mwenyekiti amefanya kififie haraka katika anga za siasa za sasa. Imejulikana kuwa wajumbe wa mkutano uliofanyika hivi karibuni, walitoa shutuma kali dhidi yake juu ya kushindwa kuongoza chama katika utawala huu wa rais Magufuli, ingawa haikuonyesha wazi nini ilikuwa chanzo. Nyuma pazia inaonyesha wengi wamechoshwa na maamuzi ya Mbowe yasiyoshirikishi pamoja na shinikizo lake la kumkaribisha Lowassa agombee urais bila kupima mbele nini kitatokea.
Kama haya yapo yanatoa taswira mbaya ya chama mbele ya ummaa wa Watanzania na nafasi ya chama katika siasa za usoni. Na ni dhahiri kuwa kwa sasa msadaa wa kifedha wa Lowassa ndani ya chama umepungua, hasa kumtambulisha Katibu Mkuu, wengi wanajiuliza juu ya ukimya wake.
Maana katika mkutano uliofanyika mkoani Mwanza baada ya kuteuliwa na chama ilikuwa kuzunguka nchi zima kumnadi na kuanza kufufua chama upya.