Lowassa ahutubia Baraza Kuu la CHADEMA

Lowassa ahutubia Baraza Kuu la CHADEMA

View attachment 273359

Hatimaye Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema/UKAWA ndugu Edward Lowassa ahutubia baraza Kuu la Chadema
Katika hotuba yake Lowassa amesisitiza kuwepo na mshikamano na maelewano ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu,huku akiwahakikishia wajumbe kuwa ushindi ni "lazima" maana mbinu na njia za "adui" zinajulikana

nimekaa kimya muda nikidhani lowassa atafanya lakini naona kimya, kwanini lowassa havai gwanda za chadema??? kwaninii
 
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.

Nakusihi usituletee ujinga kwenye Imani yetu. Mtume Paulo halingani na Lowassa hata punje.

Paulo alikiri wazi kuwa aliwaua wafuasi wa Kristo kwa ujinga wake, Lowassa anabisha kuhusika na ufisadi ingawa maisha yake yanaakisi hilo.

Paulo aliongoka akiwa njiani kutekeleza unyama, lakini Lowassa kahamia CHADEMA ili apate nafasi ya kutekeleza unyama.

Paulo hakuokoka na kuchukua seniority ya mitume aliowakuta, bali Lowassa amegeuka mfalme ndani ya CHADEMA saa kadhaa tu tangu ajiunge.

Paulo hakununua wokovu wake tofauti na huyu mwanachama mpya aliyetoa mlungula apokelewe
 
Kwanini havai gwanda lakini!

nyamaza jana niliweka swala ili sawa. Kuwa kama kamati maalumu tiyari nguo za viongozi wetu zipo zinaandaliwa tiyari kuvaliwa wakati tunaenda kumnadi rais wetu lowassa, viongoz wetu wote warefu so zoezi la ushonaji linaenda polepole. Tulizen bol
 
Yaani JK haipa timu pinzani penati dakika ya 89 mechi ya fainali..mpigaji hataki ufundi wala mbwembwe yeye ni kupiga dochi tu mpaka nyavu zichanike
 
Siyo tu kuwa havai magwanda lakini hata zile sare za fulana na kofia za Chadema nazo 'hazigusi' mwili wake.

Inawezekana kimwili yupo Chadema lakini kiroho bado yupo Sisiemu.

Acheni unafiki Nyerere aliwahi vaa za ccm?
 
View attachment 273359

Hatimaye Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema/UKAWA ndugu Edward Lowassa ahutubia baraza Kuu la Chadema
Katika hotuba yake Lowassa amesisitiza kuwepo na mshikamano na maelewano ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu,huku akiwahakikishia wajumbe kuwa ushindi ni "lazima" maana mbinu na njia za "adui" zinajulikana

Furaha waliokuwa nayo watanzania siku ya uhuru itafunikwa na furaha watakayokuwa nayo watanzania siku UKAWA watakapowaondoa CCM madarakani.
 
Hana mbinu hata moja anayo ijua.
Arumeru kasababisha ccm imeshindwa.
Yeye mwenyewe kashindwa juzi juzi dodoma mpaka kaamua kuisusa ccm.
Leo hii kazipata wapi hizo mbinu?
Nyie mfuateni muwe kama nyumbu dume likitangulia na kundi lote linafuata hata kama mamba wamechachamaa.
Na nyie huko kaskazini ndio muko jirani sana na makundi ya nyumbu tabia zenu zinafanana.
Lakini mujue hapo munapo vuuka kuna mamba msilifute mutaisha.
 
Mzee Chizi na Makongoro Mahanga ndio magwiji wa kuiba kura na ndio hivyo washatoka. Saizi kabaki mmoja tu Masaburi
 
Tatizo ccm watatumia rasilimali zetu.na pesa zetu kuwagawa cdm,Vipi kuhusu wizi wa kura?jipangeni sawa sawa,Umoja ni ngu
 
Back
Top Bottom