Habari za asubuhi GT's
Leo katika kupitia magazeti asubuhi hii nimekutana na kichwa cha habari kikubwa chenye picha ya Rais wetu JPM na picha yenye ukubwa Kama hiyo ya Lowassa wakiwa wametazamana. Rais wetu JPM akiwa anatabasamu na Lowassa akiwa Kama mtu anayefoka.
Picha hizo na hicho kichwa cha habari zimechukua asilimia 90 ya ukurasa wa kwanza wa gazeti. Gazeti hili ni la Nipashe la Leo Tarehe 9/11/2015 (ISSN 0856.No 0578662).
Baada ya kutoa Utangulizi naomba kutoa hoja:-
1. Gazeti la Nipashe limeshindwa kuweka picha sahihi kwa heshima ya Rais wa awamu ya 5 na hilo ni kutokumtendea haki. Huwezi kuweka picha za ukubwa SAWASAWA na zaidi huyu Lowassa anaonekana Kama anatoa maneno makali kwa Rais wetu Dr. JPM
2. Gazeti la Nipashe linatakiwa kufahamu kipindi cha kampeni kimekwisha na Rais amepata kana. Huwezi kutoa umuhimu sawa kwa vitu visivyolingana.
3. Taarifa hii imepewa uzito mkubwa na ina Lengo fulani nyuma Yake ambayo wenye Hekima wamenielewa.
4. Sasa na kuja kwenye ujumbe wenyewe (contents)
- Naomba Mhe. Lowassa na watu wake wafahamu kuwa Rais wa awamu ya tano Dr. JPM anatimiza ilani ya CCM.
- Ni makosa ya kiufundi na ya kitaalamu kwa wasaidizi wa Lowassa kumshauri aje kwenye vyombo vya habari kukosoa utekelezaji wa ilani ya CCM kupitia Rais wake ambaye mpaka sasa Chadema hawajamtambua.
- Namna Yake (Lowassa) ya kutoa elimu bure aendelee kuiweka na siku akiwa Rais aitumie, kwanza ni vizuri CCM hawaku copy maana ingekuwa nongwa.
- Serikali ya CCM imeanza kutekeleza Yale iliyosema kwenye kampeni kupitia ilani ambayo kwa upande wa Chadema hatukuona mgombea hata mmoja wa Chadema akikabidhiwa. Sasa kiherehere cha nini?????
- Nashauri WAPAMBE wa Lowassa muachane na kukosoa ilani ya CCM kwani muda wa kampeni UMEISHA na sasa ni muda wa utekelezaji. "#HAPA KAZI TU#
- Nashauri Mhe. Lowassa uwe mvumilivu na uiache awamu ya 5 itekeleze majukumu yake. Mambo ya kutafuta waandishi wa habari ili uwe unafuta nyayo za Rais ni sehemu ya uhaini. Pia unasahau kuwa "Mamlaka na iheshimiwe na watu wote".
- Chochote unachokosoa kuanzia sasa kuhusu serikali ya awamu ya 5 uwe na reference ambayo ni Ilani ya CCM na sio maneno yako wakati upo kwenye majukwaa ya siasa. CCM haitekelezi maneno yako au matakwa yako.
- Kama kweli wewe ni mzalendo na unataka tujenge Tanzania yetu na unaona kuna hoja ya msingi; omba appointment kamuone Mhe. Rais.
- Achana kabisa na mambo ya kutafuta umaarufu kwenye magazeti na vyombo vya habari kujaribu ku water down juhudi za mheshimiwa Rais. Watanzania hatutaki malumbano sasa tunataka kuona kazi. (#Hapa ni Kazi Tu#)
Naomba kuwasilisha.
Queen Esther
============================================
Chanzo: Nipashe
http://s18.postimg.org/5fbk8t1rt/jfpost.jpg