Lowassa ahoji maswali matatu kwa Magufuli

Lowassa ahoji maswali matatu kwa Magufuli

. Raia inabidi tuhoji ahadi tulizo ahidia na hii tutaisaidia sana serikali kutekeleza.

Kuhoji ni muhimu naungana na wewe. Tatizo ni hiyo benchmark.

Queen Esther
 
Hivi wewe hata habari yenyewe hujasoma unalalamika tukueleweje?!

Lowassa kama mpinzani,unafikiri kazi yake ni nini kama si kukosoa au kuhoji mwenendo wa serikali?

Wewe unadhani bado tuko enzi za chama kimoja?!

Salary Slip wewe ni Great Thinker wa muda mrefu hapa JF.

Sijapinga kuhoji. Nimeuliza Benchmark na hapo ndipo kwenye shida.

Queen Esther
 
Hayo maswali matatu uloandika kwenye kichwa cha habari yako wapi?

Mbona una mihemuko na Urais wa magufuli kwani una hisa pale?

Kasome Nipashe au soma hapo chinl

Lowassa ahoji maswali matatu kwa Magufuli.
NA WAANDISHI WETU
9th November 2015
B-pepe
Chapa

Edward Lowassa.
Aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),

Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.

Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.

?Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi,? alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.

Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.

?Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao,? alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo. Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.

Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.

Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.

CHANZO: NIPASHE
 
Mara nyingi kuna msemo unasemage behind every successful man there is woman behind and vice versa. Lkn behind any stupid man there is a woman behind. Na ndivyo ilivyo kwa hawa jamaa wanaooa toddlers badala ya mwanamke. Mawazo yao yanarudi kuwa ya kitoto. Haya magazeti ni ya mtu wa kilimanjaro - north. Usitegemee yampambe Magufuli. Bado wana maumivu wsli invest so much kumsafisha Lowassa na kumsaidia. Lkn Mungu si Athumani. Wameisoma namba. Magazeti haya hutumika sana kuwachafua watu hada wa kanda ya ziwa. Magufuli ndio rais atake asitake na wala hawezi kubadili matokeo ale malimau tu kama ana kichefuchefu na alee wajukuu kwa amani.
 
Umeeleweka kabsaa na ulichoongea ni kweli, Sasa ni wakati wa kujenga nchi na sio Majungu na Siasa kampeni zimekwisha jengni chama cheni na CCM Ijenge Nchi, Mlishasema hamumtambui sasa mmejuaje anayoyafanya kama hamumfatilii??? Tunachoshukuru sasa hivi UKAWA Wengi wameaanza kumkubali Magufuli....Kuwa Mwanasiasa haimaanishi hata jambo jema basi unakosoa kama kweli LOWASA Hakutaka Urais kwa ajili yake na group lake la wafanyabiashara kwa maslah yao basi sasa na akae kimya watu wajenge nchi.
 
Habari za asubuhi GT's

Leo katika kupitia magazeti asubuhi hii nimekutana na kichwa cha habari kikubwa chenye picha ya Rais wetu JPM na picha yenye ukubwa Kama hiyo ya Lowassa wakiwa wametazamana. Rais wetu JPM akiwa anatabasamu na Lowassa akiwa Kama mtu anayefoka.

Picha hizo na hicho kichwa cha habari zimechukua asilimia 90 ya ukurasa wa kwanza wa gazeti. Gazeti hili ni la Nipashe la Leo Tarehe 9/11/2015 (ISSN 0856.No 0578662).

Baada ya kutoa Utangulizi naomba kutoa hoja:-

1. Gazeti la Nipashe limeshindwa kuweka picha sahihi kwa heshima ya Rais wa awamu ya 5 na hilo ni kutokumtendea haki. Huwezi kuweka picha za ukubwa SAWASAWA na zaidi huyu Lowassa anaonekana Kama anatoa maneno makali kwa Rais wetu Dr. JPM

2. Gazeti la Nipashe linatakiwa kufahamu kipindi cha kampeni kimekwisha na Rais amepata kana. Huwezi kutoa umuhimu sawa kwa vitu visivyolingana.

3. Taarifa hii imepewa uzito mkubwa na ina Lengo fulani nyuma Yake ambayo wenye Hekima wamenielewa.

4. Sasa na kuja kwenye ujumbe wenyewe (contents)
- Naomba Mhe. Lowassa na watu wake wafahamu kuwa Rais wa awamu ya tano Dr. JPM anatimiza ilani ya CCM.

- Ni makosa ya kiufundi na ya kitaalamu kwa wasaidizi wa Lowassa kumshauri aje kwenye vyombo vya habari kukosoa utekelezaji wa ilani ya CCM kupitia Rais wake ambaye mpaka sasa Chadema hawajamtambua.

- Namna Yake (Lowassa) ya kutoa elimu bure aendelee kuiweka na siku akiwa Rais aitumie, kwanza ni vizuri CCM hawaku copy maana ingekuwa nongwa.

- Serikali ya CCM imeanza kutekeleza Yale iliyosema kwenye kampeni kupitia ilani ambayo kwa upande wa Chadema hatukuona mgombea hata mmoja wa Chadema akikabidhiwa. Sasa kiherehere cha nini?????

- Nashauri WAPAMBE wa Lowassa muachane na kukosoa ilani ya CCM kwani muda wa kampeni UMEISHA na sasa ni muda wa utekelezaji. "#HAPA KAZI TU#

- Nashauri Mhe. Lowassa uwe mvumilivu na uiache awamu ya 5 itekeleze majukumu yake. Mambo ya kutafuta waandishi wa habari ili uwe unafuta nyayo za Rais ni sehemu ya uhaini. Pia unasahau kuwa "Mamlaka na iheshimiwe na watu wote".

- Chochote unachokosoa kuanzia sasa kuhusu serikali ya awamu ya 5 uwe na reference ambayo ni Ilani ya CCM na sio maneno yako wakati upo kwenye majukwaa ya siasa. CCM haitekelezi maneno yako au matakwa yako.

- Kama kweli wewe ni mzalendo na unataka tujenge Tanzania yetu na unaona kuna hoja ya msingi; omba appointment kamuone Mhe. Rais.

- Achana kabisa na mambo ya kutafuta umaarufu kwenye magazeti na vyombo vya habari kujaribu ku water down juhudi za mheshimiwa Rais. Watanzania hatutaki malumbano sasa tunataka kuona kazi. (#Hapa ni Kazi Tu#)

Naomba kuwasilisha.

Queen Esther
Hivi unajielewa? Kukosolewa ni lazima...
 
Nakumbuka alisema atakaposhindwa ataenda kuchunga Ng'ombe sasa hivi anapaswa kukutana na wataalam wa mifugo na sio waandishi wa habari.
 
Yeye ni nani kumhoji Magufuli. Kwani ndio amekuwa msemaji mkuu wa kambi ya upinzani au ameshakuwa mk wa chadema. Kapumzike Monduli mwache Rais atimize ahadi zake kwa style yake na sio kws shinikizo lako
 
Maana ya nyomi kwenye mikutano ya kampeni ilikuwa fursa ya watanzania kusikiliza sera za wagombea.
Baada ya kusikiliza na kuchuja, ndipo wafanya maamuzi yao kwenye sanduku la kura.

watanzania si wajinga, wana uerevu wa kutosha kujua ahadi hewa na ahadi yenye uwezekano wa kutekelezwa.
Kwenye elimu, Lowassa aliahidi elimu bure toka chekechea hadi chuo kikuu mara moja. Magufuli yeye aliahidi elimu bure hadi kidato cha nne.

Baada ya kupima hoja hizo, wakampa Magufuli. Sasa kelele za Lowassa zinatoka wapi? Kwa mabilioni aliyonayo, akatoe elimu bure kule Monduli. Akawalipie hizo ada hadi Chuo Kikuu.

Amwache Magufuli afanye kazi yake kwa sasa.
 
Mungu akubariki Suip.

Queen Esther

Kasome Nipashe au soma hapo chinl

Lowassa ahoji maswali matatu kwa Magufuli.
NA WAANDISHI WETU
9th November 2015
B-pepe
Chapa

Edward Lowassa.
Aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),

Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.

Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.

?Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi,? alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.

Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.

?Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao,? alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo. Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.

Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.

Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.

CHANZO: NIPASHE
 
Hili linafundishwa chuo gani cha uandishi wa habari? Au limeelezwa na tume ya maadili ya uandishi wa habari?

1. Gazeti la Nipashe limeshindwa kuweka picha sahihi kwa heshima ya Rais wa awamu ya 5 na hilo ni kutokumtendea haki. Huwezi kuweka picha za ukubwa SAWASAWA na zaidi huyu Lowassa anaonekana Kama anatoa maneno makali kwa Rais wetu Dr. JPM
 
Kwanini hamuwezi kuongea bila kutaja kaskazini acheni ukanda mnajua fika kuna kawivu kwa sababu kaskazini ndipo wanapotoka wafanyabiashara wakubwa wasomi na watu wanaojielewa na kutambua haki zao juhudi zao binafsi ndio zimewafikisha watu wakaskazini hapo walipo kama umeamua kumponda lowasa na mengi au mbowe waponde wao binafsi sio kwa ukabila wao wala ukanda wao mbona wagogo na wanyaturu hamuwasemi au kwa sababu hawana madhara
 
Waswahili bwana...

Sasa unaulizwa swali uelezee utaratibu wewe unaanza habari za kufikiria nje ya boksi...

Fafanua hizo ethics za ukubwa wa picha ni sheria inayopaswa kufuatwa?

"THINK OUTSIDE THE BOX"

Queen Esther
 
- Achana kabisa na mambo ya kutafuta umaarufu kwenye magazeti na vyombo vya habari kujaribu ku water down juhudi za mheshimiwa Rais. Watanzania hatutaki malumbano sasa tunataka kuona kazi. (#Hapa ni Kazi Tu#)
Lowassa anatafuta umaarufu?
 
Atakosolewa tu, hata iwe vipi how come wote tuimbe wimbo mmoja, sarafu ina pande mbili. Ni lazima tujuzane ELIMU BURE ya style ipi?
 
Tatizo lenu CCM mnataka kutekenywatekenywa kama gazeti lenu la Uhuru linavyowatekenya na mnajichekesha. Magazeti kama Nipashe, Mwananchi na Mtanzania penye kusifu wanasifu penye kupiga wanapiga nyie mnataka musifiwe tu. Lowasa kwa sasa yuko kwenye kambi ys upinzani ni kaxi ya upinzani kukosoa mipango mibovu na isiyotekelezeka ya serikali wakati wowote. Hizo picha za Magufuli kazinunue ubandike chumbani mwako kabla hujalala uziabudu na kuzisifu.
 
Back
Top Bottom