Naungana na wewe, EL ni mvumilivu sana ila sina hakika na roho ya kusamehe na kutolipiza visasi.
Why Yellow T shirts?
Imedhihirika leo kwamba mh Edward Lowassa sio tu kwamba anapendwa bali pia ni tegemeo kubwa kwa watanzania wanyonge na wa hali ya chini.
Umati wa watu ambao haujawahi kuonekana pamoja na waendesha bodaboda wapatao elfu zaidi ya elfu ishiriki wamejumuika nae leo wakati alipokaribishwa kuwa mgeni rasmi wa chama chao.
endelea kusema hivyo,huko kenya napo walikua wanasema uhuru muuaji,mwizi wa ardhi etc..matokeo uliyaona.Huyu mtu alijiuzulu kwa ufisadi, habari ndiyo hiyo!
Hata apokelewe na kadamnasi ya watu, huo ni ukweli usiopingika.
Ni mchafu hasafishiki!!!
Ukitulia na kutafakari kwa kina, unaweza usiamini kama Lowasa leo hii anaweza akapigiwa debe namna hii.
mkuu hapo nakuunga mkono,huyu jamaa ni mvumilivu cijawahi ona popote!!
Lowassa ndiyo kiboko ya Chadema.
Hata mimi nashangaa.As if waliandaliwa
Ni kweli, kinondoni ilisimama zaidi ya saa mbili leo kumpisha lowassa, utafikiri ndio kafanyiwa inauguration
boda boda wa dar wamepewa shilingi ngapi na EL?Moshi alichangia Bilion moja, mwanza milioni 600. Dar nao wamefuata dau lau na si mapenzi wala kumpenda EL bali dau ndilo MKUKUTA /MKURABITA. Usicheze na ugumu wa maisha wa sasa.
Ametembeza pesa chafu tu hapo, wala huhitaji rocket science hapa kubaini nini kinaendelea. Na pesa hizi zimesambazwa pia kwa viongozi wa dini, wabunge, wajumbe wa NEC ya CCM, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, media, baadhi ya viongozi wa upinzani, etc