Bubu Msemaovyo
Platinum Member
- May 9, 2007
- 4,189
- 3,552

Ndoto inatafsiriwa kuwa ni kitendo cha ubongo kurejesha tukio au matukio ambayo tayari yametokea kabla ya kuotwa upya. Aidha kuna ndoto ambazo ningependa kusema ni unabii na hizi huwakuta watu waliochaguliwa na Mungu kuwa Manabii.
Ndoto hizi za kawaida mara nyingi na ni kawaida kuotwa usiku na muotaji sharti awe amelala usingizi mnono.
Ndoto ya Edward N. Lowassa: Ameota siku isiyojulikana akiota kuwa ipo siku moja elimu ya Tanzania itakuwa ni ya haki na huru. Hii ina maanisha kuwa serikali ya chama chake cha CCM inaendesha mfumo wa elimu isiyo ya haki na siyo huru. Jambo hili ni kweli na hata mimi Bubu Msemaovyo bila kuota naona hilo. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo katika sera zake kina amini kuwa elimu ni haki ya kila Mtanzania na lazima itolewe bure kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu. Mh muotaji ndoto alisomeshwa na Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa mfumo huu wa elimu bure kuanzia alipokuwa moran hadi Laigwanani. Mh. Lowassa sidhani kama unaota mimi binafsi nina amini umesoma sera za Chadema na umeamini hilo. Kwa mateso ya kukandamizwa na CCM sisi wanyonge hatuna usingizi kwa hiyo hatuwezi kupata usingizi huo wa kutuwezesha KUOTA NDOTO.
Pia ninapata picha kuwa ulikuwa ukimuiga Mpigania haki wa Marekani Hayati Martin Luther King Jr, pale aliposema "I have a Dream" Mwanaharakati huyu siyo wa kuigizwa kamwe alichokiongea alikimaanisha na alijitoa nacho muhanga hadi wabaya wake wakamuua. Ili uweze kueleweka wewe Lowassa kosoa mfumo wa CCM hadharani na utueleze "You have a Dream" Tujue umekuwa ni mtu unayefanana na sisi tusioota ndoto bali tumezongwa na mkandamizo wa CCM.
Dreams are successions of images, ideas, emotions, and sensations that occur involuntarily in the mind during certain stages of sleep.
Tunakutakia usingizi mwema wenye kukuletea ndoto nyingi!!!