Lowassa aache uchonganishi, hakuna njaa nchini

Lowassa aache uchonganishi, hakuna njaa nchini

Kwahiyo ukipata tatizo unaanza kwanza kulitatua au unaanza kwanza kuangalia chanzo alafu ndio unalitibu....aaah mfano kuna kipindupindu hapo Chato na watu wanakula je utaanza kuwatibu na kuwaokoa au utaanza na kutafuta chanzo za huo ugomjwa. ..Nilisema tumsifie kada mwenzetu
Tanzania HAINA JANGA LA NJAA WANASIASA WACHACHE WANATAKA KUHARIBU NCHI YETU,,,tujiulize NI MAMLAKA GANI IMEWAPA HAO WANAOTANGAZA JANGA LA NJAA UWEZO WA KUTANGAZA TATIZO HILO???
 
Sasa kama aliwadhurumu wananchi kama unavyosema.kwanini wananchi wasipokee chakula kilichotokana na mali zao!?
 
Wachungaji, Baadhi ya Ma-DC, Masheikh, Magazeti na TV zote hizo huajziona/hujaviona umemuona Lowasa tu?? Una lako jambo, by the way, Njaa ni kama Mimba, haifichiki.
 
watu wanashindwa kuelewa kua lowasa in mwananchi kama wengine. anaposema ana njaa in kwenye kaya yake. so sioni cha kumlaumu. sasa Mimi nikisema kuna njaa unaniitaje mchonganishi?. kwani unanilisha.
na nikifanya juhudi kuwaunganisha wenye njaa kama Mimi kuna kosa gani?
 
Na,
Augustino Chiwinga.

Aliyekua mgombea urais kupitia chama cha CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA ndugu Edward Lowassa, leo jumapili tarehe 15/1/2017,alikua mjini Bukoba Mkoani kagera.

Ametumia madhabahu matakatifu ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,kanisa ambalo pia alitumia madhabahu yake katika kampeni za urais mwaka 2015 kuomba walutheri wamchague yeye katika nafasi ya urais kwa kua yeye ni mlutheri na nchi haijawahi kua na Rais mlutheri tangu uhuru,ametangaza eti kwamba atagawa chakula wa wananchi wanaokabiliwa na "upungufu wa chakula."

Kwanza nasikitika kwa uongozi wa kanisa la KKKT kukubali madhabahu yake yaendelee kunajisiwa na ndugu Edward Lowassa, maana mtu huyu kwa dhambi na mabaya aliyowafanyia watanzania maskini na wanyonge wa nchi hii hafai kukaribishwa wala kusimama katika mimbari mitakatifu ya kanisa. Nina shaka na uadilifu wa viongozi wa kanisa la KKKT Bukoba.

Swali la kujiuliza ni wapi Lowassa na vibaraka wenzake wametoa mamlaka ya kutangaza uwepo wa uhaba wa chakula Tanzania ?
Kwa mujibu wa sheria, mwenye mamlaka ya kutangaza aina yeyote ya majanga au maafa Tanzania ni wakala wa taifa wa usimamizi wa maafa pekee.

Kwa hiyo kitendo cha Lowassa na vikundi vya watu hususani vibaraka wa CHADEMA kutangaza na kueneza habari za uongo kwamba kuna baa la njaa Tanzania inakwenda kinyume na kifungu cha 38(C) cha sheria namba 17 ya Sheria ya usimamizi wa maafa Tanzania ya mwaka 2015,ambacho kinasema

"Mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo na akijua kua sio kweli atakua ametenda kosa na atahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini au vyote kwa ka pamoja"

Kupitia nukuu hii ya sheria ni wazi kwamba ndugu Edward Lowassa ametenda kosa na naomba mamlaka husika zichukue hatua kali za kisheria juu yake na wenzake wote wanaosema uongo juu ya hali ya chakula nchini wafunguliwe mashtaka mara moja.

Pamoja na hayo uzalishaji wa mazao ya chakula hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016 ulikua ni tani 15,528,820 ukilinganisha na mahitaji yaliyokua 12,946,103, hivo kupelekea nchi kuzalisha ziada ya chakula tani 2,582,717.
Kwa maana hiyo ni kwamba taifa linajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 120 (120%)

Sasa sielewi hizi kelele za wapinzani kua njaa imeingia Tanzania zimetokea wapi na kwa misingi ipi, ikiwa wakulima walizalisha ziada ya chakula yaani tani 2,582,717, mpaka kufikia wakaingia tamaa ya kuuza mazao yao katika nchi za jirani mpaka pale serikali ilipoingilia kati .

Ni vema wanasiasa wakaacha kutia wananchi hofu za bure na kupandikiza chuki kwa maslahi yao ya kisiasa, kwani kwa kufanya hivo wanakua hawana tofauti na wahaini kama walivyo wahaini wa aina nyingine.

Huyu Edward Lowassa anayetangaza kugawa chakula tumuulize ni mwanananchi gani aliyemfuata kumuomba chakula, atuoneshe hata mmoja tu au atuoneshe kaburi la mwananchi yeyote aliyekufa kwa njaa.

Alikuyepo Bukoba na Mbunge Lwaktare ,mbunge amsaidie Lowasa kumuonesha mwanachi yeyote anayekabiliwa na "baa la njaa" kama atafanikiwa kumpata hata mmoja.
Kwanza hata ikitokea kweli liwepo ilo "baa la njaa" kama wanavyozusha (MUNGU EPUSHIA MBALI"

Wananchi hawawezi kupokea chakula chake kikichojaa damu jasho ,na dhulma zilizotokana na kuwaibia watanzania.
Ni heri kufa njaa kuliko kupokea chakula kilichotoka kwenye mikono yeye dhambi ya Edward Lowassa.

Huruma hii ya Lowassa ni ghilba na uzandiki tu wa kisiasa. Ingependeza kabla ya kuanza kujisifia kua atawapa watu chakula, kwanza angefanya yafuatayo;
1) Awarudishie wananchi pesa zote alizowaibia.
2) Arudishe mashamba na ranch zote alizopata kwa uporaji na rushwa.
3) Arudishe nyumba na viwanja vyote alivyovitwaa kipindi akiwa waziri wa ardhi nyumba na maendeleo mjini.

4) Arudishe pesa za Richmond.
5) Atueleze kiundani juu ya kifo cha mchungaji Christopher Mtikila.
6) Aweke wazi mali na kampuni anazomiliki na atueleze alizipataje.
7)Aweke wazi taarifa zake za ulipaji kodi.

Ni wazi kuwa CHADEMA na Lowassa wamekosa kabisa agenda ya kuuza chama chao, matokeo yake wanaokoteza okoteza vitu ambavyo havina msingi wowote wa hoja na kuvitumia kumshambulia Mh. Rais Dr. John P. Magufuli, na ni wazi kuwa wanamshambulia Rais yeye binafsi na sio chama cha mapinduzi

Hii inaonesha wazi kuwa wana mpango kabambe wa kumhujumu na kumchonganisha Mh.Rais na wananchi anaowaongoza, lakini kwa bahati mbaya ni kwamba wananchi bado wana imani na CCM na bado wana imani na mapenzi makubwa kabisa na Rais wao mpendwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli.

Mwisho nimalizie kwa kusema kwamba CHADEMA waache kutumia msamiati wa njaa kuwa agenda yao waache kutumia ghilba husda na uzushi kama kete yao ya kisiasa, kwani Tanzania haina njaa na wawaache watanzania wenye akili timamu wafanye kazi kwa maslahi mapana ya taifa lao.

Augustino Chiwinga.
Maelezo yako meengi lkn nimeambulia patupu sijui kiswahili hukusoma?
 
Nashangaa wenye njaa wanalia njaa! Lakini wanaoshiba kwa kuwakamua wenye njaa wanapinga hakuna njaa.
 
Ukiamka tumbo linakuuma kaa karibu na choo na sio kukimbilia simu na kuwasha data ni lazima uishie kuandika mboji ya binadam nyambafu! Hivi kama njaa hakuna mnahangaikia nini? Kwann wàtato wa loumoumba mkitoka msalani hata hamjasafisha vizur hayo maeneo ya opposite of mauthi mnakimbilia kupinga kwamba hakuna njaa? Hivi mnapajua shinyanga na Simiyu au ninyi ni wa pwani hamjatembea tz main land? Na kwa taarifa yenu mtaisoma maana kila mkulu akifanya ziara hasa kwenye majanga mjipange kutetea alichosema na mkishindwa mtaishia kutuambia alikuwa anatania! Na nimjuavyo lowassa kuhusu njaa na mnavyokuja kwa kubwata kama mpo kwenye foleni ya vyoo vya stand ya ubungo hakika atawanyoosha tena yeye akitumia maneno mawili huko kwenu mtaandika kurasa za kutosha na hiki ndo kipimo kwamba ssm mlifikiria au mlifikirishwa kumteua huyu kugombea uprezdaa na kwa jinsi alivyombishi mtatepeta maana mtatetea mwisho atawakana!. Najua kuna siku mtamtetea kuwa alikuwa anachekesha hakuwa siriaz halafu yy atakuja kukanusha na kusema nilimaanisha hapo ndo mtajuta.
 
Mkubwa hivi njaa inawezekana kuwepo leo Tanzania wakati uku kahama Mchele kilo moja ni 1,200 mpaka 1,500. nijuavyo mimi ni kuwa ni kweli kubna ukame ambao unaweza pelekea msimu wa mwaka huu kukawepo na njaa lakini kwa sasa hakuna njaa na sehemu iliyopo njaa ni kawaida ya wakulima kuuza chakula chote na kuanza kusema kuna njaa
Mfano ni meatu na kishapu miaka yate wao ni watu wa kusaidiwa tu hiyo huwezi kusema kwa sababu ya watu wa Meatu na kishapu leo hawana chakula ukasema kuna njaa njoo kahama au nenda Rukwa, Mbeya ndio useme Tanzania kuna njaa
Nahisi shibe ndivyo inakufanya useme ujinga kama huu IPO siku na wewe utakuwa kama sisi tu
 
Ukawa acheni siasa za maji taka tena mshindwe na mlegee,uchochezi wa namna hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa lakini Mungu yuko upande wetu mtashindwa tu.AKIMALIZA 10 TUNAMUONGEZEA.
 
Nani mwenye mamlaka ya kutangaza hali yoyote ya hatari katika nchi? Mfano wa wazi kabisa ni pale tulivyovamiwa na Nduli Idd Amin Dadaa,Hayati Baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere akiwa amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Tanzania aliutangazia umma tena ktk mkutano maalumu na vyombo vya habari juu ya uvamizi wa nchi yao kutoka kwa Idd Amin Dadaa.
Mfano wa pili na hata baada ya kutokea kifo cha baba yetu au baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere ni Rais wa wakati huo ndugu Benjamin William Mkapa akautangazia umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari juu ya msiba huo.
Nachotaka kusema kila nchi inautaratibu wake wa kutangaza majanga ya kitaifa naweza kusema labda majanga makuu yanayotokea au yanayotishia kutokea ktk nchi,kwahiyo Watanzania tuwe makini kwa hilo kwani wahenga walisema 'Miluzi mingi ilimpoteza Mbwa muelekeo' kwahiyo Watanzania kama kunatishio lolote la njaa Rais wetu ni mtu wa watu na nimpenda watu na Rais wetu yupo ndani ya jamii hii hii ya Watanzania, kama kunatishio lolote ktk nchi atautangazia umma juu ya tishio hilo kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa Taifa hili teule.
Samahani hivi lilipotokea tetemeko mkuu ndiye aliyekuwa wa kwanza kutangaza? Acheni unafiki na kupakana mafuta. Hivi kwa nini waafrika ni wagumu sana kukubali wanapokosea?
 
Njaa IPO mkoa gani jamani!!???? Mbona mi sioni jambo hiliii
 
Mkubwa hivi njaa inawezekana kuwepo leo Tanzania wakati uku kahama Mchele kilo moja ni 1,200 mpaka 1,500. nijuavyo mimi ni kuwa ni kweli kubna ukame ambao unaweza pelekea msimu wa mwaka huu kukawepo na njaa lakini kwa sasa hakuna njaa na sehemu iliyopo njaa ni kawaida ya wakulima kuuza chakula chote na kuanza kusema kuna njaa
Mfano ni meatu na kishapu miaka yate wao ni watu wa kusaidiwa tu hiyo huwezi kusema kwa sababu ya watu wa Meatu na kishapu leo hawana chakula ukasema kuna njaa njoo kahama au nenda Rukwa, Mbeya ndio useme Tanzania kuna njaa


Kwa hivyo wewe mfano ukivunjika mguu basi sio mwili wote unaumwa kwa sababu uliovunjika.ni mguu tu?
 
Ni kawaida kwa wanasiasa kutumia mateso ya watu kujitafutia umaarufu. Lowassa ndio awape watu wenye njaa chakula? Kama nani sasa yeye? Upuuzi.
 
Kwa Lowasa na Chama cha Chadema kutoa msaada wa chakula, wakati Rais amesema hatatoa chakula kwa waadhirika wa tetemeko na wananchi kwa ujumla. Mimi ninaona hii ni dharau na kumvunjia heshima. Lowasa hawezi kuwa mkarimu kuliko Rais.
 
Kwa Lowasa na Chama cha Chadema kutoa msaada wa chakula, wakati Rais amesema hatatoa chakula kwa waadhirika wa tetemeko na wananchi kwa ujumla. Mimi ninaona hii ni dharau na kumvunjia heshima. Lowasa hawezi kuwa mkarimu kuliko Rais.
Huo ni mtazamo wako. Hata masikini anaweza kuwa na wema zaidi ya tajiri.
 
Back
Top Bottom