gasto genaro
JF-Expert Member
- Oct 15, 2014
- 780
- 554
Swali zuri mkuu. Hawezi jibu. Alafu, cheki hii picha apa. Imepigwa na mtu wa kijijini huko Rombo Mkuu. Mazao yamekauka.. Watu wanasema hakuna njaaMnajua tatizo lipo lakini mpo bizy kupiga propaganda za kisiasa kuwa halipo. Mnadhani njaa au ugonjwa ni sawa na vyama vya siasa ambapo ukikataza mikutano basi inabidi watii la sivyo wanapigwa virungu na vitu vyenye ncha kali na wengine kupoteza maisha au kufungwa? Njaa au ugonjwa fulani kama vipo, vipo tu hata ukipiga mkwara, bila kuweka mikakati ya kuvikabili vinazidi kuenea na kuathiri watu wengi zaidi.
Sasa sitaki kujibu uchochei mwingi ulioandika hapo ila nataka kuuliza jambo moja tu.
KAMA KWELI NJAA HAKUNA, KAULI KUWA KUNA NJAA INAWEZAJE KUWATISHA WANANCHI? YAANI UMWAMBIE MTU MWENYE CHAKULA CHA KUTOSHA KABISA AU ALIYESHIBA NA MWENYE UHAKIKA WA KUSHIBA KWA MWAKA MZIMA ATI KUNA NJAA, GHAFLA NA YEYE AHISI KWELI NJAA IPO NA AINGIWE NA HOFU?
Tupige porojo huku mkiwa mnatafuta ufumbuzi. Hizo takwimu mnazoleta msije mkazikana na kuzikanusha baadaye. Mwisho wa siku tutaambiwa chakula kilichokuwepo kimeenda kwenye mashule na magereza tu.
After all, nina hakika misalaba mingi bado haijapata watu wa kuibeba, na kwa kuwa tulishaambiwa kila mtu abebe msalaba wake, hali itaendelea hivi hivi hadi misalaba yote imalizike kubebwa na wahusika.