ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 642
Na,
Augustino Chiwinga.
Aliyekua mgombea urais kupitia chama cha CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA ndugu Edward Lowassa, leo jumapili tarehe 15/1/2017,alikua mjini Bukoba Mkoani kagera.
Ametumia madhabahu matakatifu ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,kanisa ambalo pia alitumia madhabahu yake katika kampeni za urais mwaka 2015 kuomba walutheri wamchague yeye katika nafasi ya urais kwa kua yeye ni mlutheri na nchi haijawahi kua na Rais mlutheri tangu uhuru,ametangaza eti kwamba atagawa chakula wa wananchi wanaokabiliwa na "upungufu wa chakula."
Kwanza nasikitika kwa uongozi wa kanisa la KKKT kukubali madhabahu yake yaendelee kunajisiwa na ndugu Edward Lowassa, maana mtu huyu kwa dhambi na mabaya aliyowafanyia watanzania maskini na wanyonge wa nchi hii hafai kukaribishwa wala kusimama katika mimbari mitakatifu ya kanisa. Nina shaka na uadilifu wa viongozi wa kanisa la KKKT Bukoba.
Swali la kujiuliza ni wapi Lowassa na vibaraka wenzake wametoa mamlaka ya kutangaza uwepo wa uhaba wa chakula Tanzania ?
Kwa mujibu wa sheria, mwenye mamlaka ya kutangaza aina yeyote ya majanga au maafa Tanzania ni wakala wa taifa wa usimamizi wa maafa pekee.
Kwa hiyo kitendo cha Lowassa na vikundi vya watu hususani vibaraka wa CHADEMA kutangaza na kueneza habari za uongo kwamba kuna baa la njaa Tanzania inakwenda kinyume na kifungu cha 38(C) cha sheria namba 17 ya Sheria ya usimamizi wa maafa Tanzania ya mwaka 2015,ambacho kinasema
"Mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo na akijua kua sio kweli atakua ametenda kosa na atahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini au vyote kwa ka pamoja"
Kupitia nukuu hii ya sheria ni wazi kwamba ndugu Edward Lowassa ametenda kosa na naomba mamlaka husika zichukue hatua kali za kisheria juu yake na wenzake wote wanaosema uongo juu ya hali ya chakula nchini wafunguliwe mashtaka mara moja.
Pamoja na hayo uzalishaji wa mazao ya chakula hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016 ulikua ni tani 15,528,820 ukilinganisha na mahitaji yaliyokua 12,946,103, hivo kupelekea nchi kuzalisha ziada ya chakula tani 2,582,717.
Kwa maana hiyo ni kwamba taifa linajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 120 (120%)
Sasa sielewi hizi kelele za wapinzani kua njaa imeingia Tanzania zimetokea wapi na kwa misingi ipi, ikiwa wakulima walizalisha ziada ya chakula yaani tani 2,582,717, mpaka kufikia wakaingia tamaa ya kuuza mazao yao katika nchi za jirani mpaka pale serikali ilipoingilia kati .
Ni vema wanasiasa wakaacha kutia wananchi hofu za bure na kupandikiza chuki kwa maslahi yao ya kisiasa, kwani kwa kufanya hivo wanakua hawana tofauti na wahaini kama walivyo wahaini wa aina nyingine.
Huyu Edward Lowassa anayetangaza kugawa chakula tumuulize ni mwanananchi gani aliyemfuata kumuomba chakula, atuoneshe hata mmoja tu au atuoneshe kaburi la mwananchi yeyote aliyekufa kwa njaa.
Alikuyepo Bukoba na Mbunge Lwaktare ,mbunge amsaidie Lowasa kumuonesha mwanachi yeyote anayekabiliwa na "baa la njaa" kama atafanikiwa kumpata hata mmoja.
Kwanza hata ikitokea kweli liwepo ilo "baa la njaa" kama wanavyozusha (MUNGU EPUSHIA MBALI"
Wananchi hawawezi kupokea chakula chake kikichojaa damu jasho ,na dhulma zilizotokana na kuwaibia watanzania.
Ni heri kufa njaa kuliko kupokea chakula kilichotoka kwenye mikono yeye dhambi ya Edward Lowassa.
Huruma hii ya Lowassa ni ghilba na uzandiki tu wa kisiasa. Ingependeza kabla ya kuanza kujisifia kua atawapa watu chakula, kwanza angefanya yafuatayo;
1) Awarudishie wananchi pesa zote alizowaibia.
2) Arudishe mashamba na ranch zote alizopata kwa uporaji na rushwa.
3) Arudishe nyumba na viwanja vyote alivyovitwaa kipindi akiwa waziri wa ardhi nyumba na maendeleo mjini.
4) Arudishe pesa za Richmond.
5) Atueleze kiundani juu ya kifo cha mchungaji Christopher Mtikila.
6) Aweke wazi mali na kampuni anazomiliki na atueleze alizipataje.
7)Aweke wazi taarifa zake za ulipaji kodi.
Ni wazi kuwa CHADEMA na Lowassa wamekosa kabisa agenda ya kuuza chama chao, matokeo yake wanaokoteza okoteza vitu ambavyo havina msingi wowote wa hoja na kuvitumia kumshambulia Mh. Rais Dr. John P. Magufuli, na ni wazi kuwa wanamshambulia Rais yeye binafsi na sio chama cha mapinduzi
Hii inaonesha wazi kuwa wana mpango kabambe wa kumhujumu na kumchonganisha Mh.Rais na wananchi anaowaongoza, lakini kwa bahati mbaya ni kwamba wananchi bado wana imani na CCM na bado wana imani na mapenzi makubwa kabisa na Rais wao mpendwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli.
Mwisho nimalizie kwa kusema kwamba CHADEMA waache kutumia msamiati wa njaa kuwa agenda yao waache kutumia ghilba husda na uzushi kama kete yao ya kisiasa, kwani Tanzania haina njaa na wawaache watanzania wenye akili timamu wafanye kazi kwa maslahi mapana ya taifa lao.