Lowasa: Kuvuliwa Madaraka, Kujiuzulu na Kustaafu

Jaji joseph sinde warioba hakupewa term ya pili ya uwaziri mkuu na makamu wa rais wa jamhuri wa muungano bila jamii kuelezwa sababu za kutoteuliwa kwake tena kwa awamu ya pili, vivyo hivyo kawawa,msuya na salimu, john malecela yeye hakujiuzuru bali rais alivunja baraza la mawaziri na kumuondoa ktk kiti kile lakini wote hawa ndugu zangu wana jf ni wastaafu ktk kiti hicho. Hatujahoji hili ila tumemkomalia edward lowasa, huyu ni mtu makini aliyethubutu kujiuzuru na kuilinda heshima yake kichama na mamlaka aliyomo. Rais kikwete alikiri na kuridhia kujiuzuru kwake. Anastahili kuheshimiwa, kuenziwa na zaidi ni mstaafu mwenye rekodi ya kuwajibika kitu ambacho mzee wetu malecela alishindwa kukifanya 1994.

Anastahili kuheshimiwa waungwana.
 
Ninachokiona hapa ni matumizi tu ya lugha ambayo yamezoeleka na kuhalalishwa kana kwamba ni sahihi. Nionavyo, neno "mstaafu" halipaswi kutumika kwa jinsi linavyotumika sasa, na badala yake ingekuwa inatumika maneno yafuatayo. "Waziri mkuu wa zamani" (Former prime minister) au Rais wa zamani (Former President). Mbona waliowahi kuwa mawaziri na sasa sio mawaziri hatutumii maneno "Waziri mstaafu wa Elimu, au Kilimo, n.k?"

Mtu kama alikuwa na wadhifa wa Waziri Mkuu na baadaye yakafanyika mabadiliko akaondolewa kwenye wadhifa huo, au yeye mwenyewe akajiuzulu, hatuwezi kusema kwamba amestaafu uwaziri mkuu, na kwa maana hiyo si sahihi kumwita waziri mkuu mstaafu. Badala yake, ni sahihi kumwita aliyekuwa Waziri Mkuu, au Waziri Mkuu wa zamani (Former prime minister).

Au kwa mfano, siyo sahihi, kusema "Spika mstaafu" Pius Msekwa, bali tunatakiwa kusema "Aliyewahi kuwa spika au Spika wa zamani Pius Msekwa (former speaker).

Suala la mafao ya wanasisa wa hizo nyadhifa liko kisheria, bila kujali muda aliotumika kwenye hicho cheo, ili mradi tu awe ametumika kwenye wadhifa huo hata kama ni kwa saa moja, atastahili kupata hayo mafao kwa mujibu wa wadhifa aliokuwa nao.
 
Jaji joseph sinde warioba hakupewa term ya pili ya uwaziri mkuu na makamu wa rais wa jamhuri wa muungano bila jamii kuelezwa sababu za kutoteuliwa kwake tena kwa awamu ya pili, vivyo hivyo kawawa,msuya na salimu, john malecela yeye hakujiuzuru bali rais alivunja baraza la mawaziri na kumuondoa ktk kiti kile lakini wote hawa ndugu zangu wana jf ni wastaafu ktk kiti hicho. Hatujahoji hili ila tumemkomalia edward lowasa, huyu ni mtu makini aliyethubutu kujiuzuru na kuilinda heshima yake kichama na mamlaka aliyomo. Rais kikwete alikiri na kuridhia kujiuzuru kwake. Anastahili kuheshimiwa, kuenziwa na zaidi ni mstaafu mwenye rekodi ya kuwajibika kitu ambacho mzee wetu malecela alishindwa kukifanya 1994.
Anastahili kuheshimiwa waungwana.

Sina hakika kama unaelewa unayoyasema. Mtu kujiuzulu kwa kashifa nzito ya kuibia umma ni heshima?? WaTz kazi tunayo kweli kweli! Unawezaje, mtu mwenye akili timamu, unayeweza angalau kuchambua mambo ukatoa kauli kama hiyo?? Hiyo record ni zile chafu na haistahili kupigiwa mfano na mtu mweye akili na busara zake, labda kama naye ni mshirika kwenye huo uchafu!
 
Jaji joseph sinde warioba hakupewa term ya pili ya uwaziri mkuu na makamu wa rais wa jamhuri wa muungano bila jamii kuelezwa sababu za kutoteuliwa kwake tena kwa awamu ya pili, vivyo hivyo kawawa,msuya na salimu, john malecela yeye hakujiuzuru bali rais alivunja baraza la mawaziri na kumuondoa ktk kiti kile lakini wote hawa ndugu zangu wana jf ni wastaafu ktk kiti hicho. Hatujahoji hili ila tumemkomalia edward lowasa, huyu ni mtu makini aliyethubutu kujiuzuru na kuilinda heshima yake kichama na mamlaka aliyomo. Rais kikwete alikiri na kuridhia kujiuzuru kwake. Anastahili kuheshimiwa, kuenziwa na zaidi ni mstaafu mwenye rekodi ya kuwajibika kitu ambacho mzee wetu malecela alishindwa kukifanya 1994.

Anastahili kuheshimiwa waungwana.

(1) Chini ya Katiba yetu, waziri mkuu wetu ni mteule wa Rais. Imekuwa hivyo tangu cheo hiki kiliporudishwa nchini mwaka 1972 ingawa baadaye kiliongezwa kifungu kuwa mteule huyo akubaliwe na Bunge. Rais anaweza kumpa madaraka hayoi mtu yeyote kulingana na matakwa yake na vile vile anaweza kumpokonya mtu huyo wakati wowote kulingana na matakwa yake. Matakwa ya rais yanaweza kuwa hayana uhusiano kabisa na utendaji wa mtu huyo. Ndiyo maana kuna watu waliowahi kupokonywa cheo hicho halafu wakapewa tena: Msuya na Sokoine. Kwa hali hiyo, mabadiliko yote yaliyofanywa na rais na siyo hukumu kwa walionyanganywa madaraka yao kuwa wao ni wakosefu. Lowasa hakunyang'anywa madaraka yale na Rais, bali alijivua kusetiri aibu inayotokana na makosa aliyokuwa amefanya akiwa madarakani. Kesi yake ni kama ile Richard Nixon aliyekuwa rais wa marekani na kujiuzulu mwaka 1974 ili kuficha aibu ya kashfa za Watergate zilizokuwa zinamkabili. Tangu ajiuzulu mwaka 1974, pamoja na kuwa alisamehewa mara moja na rais aliyemfuatia, bado Rais Nixon hakupewa tena heshima ya urais hadi mwaka 2007 (miaka 33 tangu atoke madarakani na akiwa ameshakufa). Lowasa anatakiwa afuate njia ya Nixon.

(2) Hiyo rekodi ya utendaji na kuwajibika ya Lowasa kuwashinda waliomtangulia ni myth kubwa sana ambayo binafsi sikubaliani nayo. Mtu huyu alifanya maamuzi ya kijinga mengi tu ambayo hayakuwa hata na chembe ya busara. Ukiachilia mbali hilo la Richmond, jamaa aliahidi kutuletea mvua isiyokuwa ya sili kutokea Thailand (ujinga klweli huu), alitangazia umma kuwa ndege ya Uchumi inaruka lakini kama unavyofahamu uchumi wa Tanzania unashindana na wa Somalia, Chad, Malawi, East Timor na nchi za namna hiyo (ukurupukaji huo.) Alisema atajenga Hoteli ya kitalii kwenye mbuga za wanyama bila kuwasikiliza wanamzingira eti kwa vile Kenya nao wana hoteli ya namna hiyo (busara gani hizo). Kuna upuuzi mweingi sana alioufanya ambao mtu unaweza kuandika kitabu kikubwa tu.

Tukiachia hayo, kama angekuwa mstaarabu, basi asingesubiri tume ichunguze na kutumia mabilioni ya pesa za walipa kodi na kuja kuachia ngazi tu baada ya kugundua kuwa ameshazungukwa pande zote za dunia. Ningemheshimu tu kama angeamua kujiuzulu bila kulazimishwa. Bwana huyu alijiuzulu baada ya Mwakembe kumtaka afanye hivyo huku akiwa ameshikilia kifurushi cha ushahidi dhidi yake. Sioni kama kweli kitendo hicho ni cha kistaarabu kinachostahili kuheshimiwa.
 
Mimi nitatofautiana na wengi walionitangulia kwa sababu moja tu kubwa. EL pamoja na tuhuma nzito na lawama zinazomwandama ni kiongozi pekee nchini ambaye baada ya kukaa na kupima uzito wa tuhuma dhidi yake aliandika barua ya kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe. Pamoja na kujua angeweza kukataa na bosi wake asiwe na ubavu wa kumwajibisha, but like a good and brave soldier in a battlefield, he stopped the bullet meant for his commander.

EL hakufukuzwa, hakuvuliwa madaraka wala hakustaafishwa ila aliamua kukaa kando kwa hiari yake mwenyewe. Kitendo chake hicho peke yake kinamweka kwenye kundi la watu wenye msimamo ingawa halimwondoi kwenye swala la UFISADI. Hakuna anayejua kungetokea nini kama EL hangejiuzulu lakini kwa kufanya hivyo sioni ubaya wa kuitwa Waziri Mkuu Mstaafu. Tendo la Lowassa lisiwekwe mizani moja na la Mzee Mwinyi - La EL lilihitaji ujasiri na uwajibikaji wakati la Mwinyi lilihitaji uwajibikaji peke yake.
 
1. Maalim Seif, alilazimshwa kujiuzulu kwenye kikao cha CC yeye na wenzake flani waliwekwa ndani kwa muda kidogo, walipoachiwa hakuwahi kuitwa Waziri Kiongozi Mstaafu, wala kupewa mafao, Lakini katika kikao cha muafaka CCM wakamua kumrudishia mafao yake yote na heshima zake zote, sasa in the light ya yote yaliyoandikwa hapa kwenye hii thread, naomba kuuliza hii ishu ya Maalim Seif ina-fit vipi?

2. Kuhusu Lowassa, ninaamini kwamba aliondolewa na rais period!, na sio anybody else, rais alipowasili Dodoma, Waziri Mkuu akakosa uwanjani wa ndege mimi nilikuwa mtu wa kwanza kusema hapa kwamba he is done na hii ilikuwa hata kabla ya kuandika barua yake ya kujiuzulu, meaning kwamba Lowassa alijua mapema kwamba hana confidence ya rais tena, sasa alijuaje?

- Kwamba eti ni jasiri kwa kutoka bila kujitetea, labda kwa wasiofahamu, kwa sababu tunajua hela zilizotumika kujaribu kuwahonga wabunge wasikubali ripoti, tunajua njama zote zilizotumika kumghilibu Hosea, na kumpa ripoti ya kuchonga, huku Lowassa akiichukua original na kuificha, so much for a hero!, tunajua jinsi alivyojaribu kila njia kumshawishi Mwakyembe, kumpa ile ripoti original ili iwe kama ya Hosea, tumeyajuaje haya ya Hosea, mjumbe wake mmoja alipohojiwa na kamati ya bunge alisema ukweli wote na hata kuwafanya wabunge kumtaka Pinda, amuwajibishe Hosea!

Sasa after all this Lowassa is a hero? Only in Tanzania, ninaamini kwa nia njema kabisa kwamba Lowassa, anastahili kuitwa Waziri Mkuu Mstaafu kwa sababu the main thing ya mstaafu ni mafao, na ninaamini kwamba regardless ya sheria tulizonazo kuhusu mafao ya viongozi wetu wastaafu, ni walioko kwenye power ndio huamua nani apewe nini, siamini kabisa kwamba inafuatwa sheria, na siamini kwamba Lowassa anapewa mafao yote, zaidi tu ya walinzi ambao pia sio wengi kama wastaafu wengine!

Ahsante Wakuu!
 
Kuhusu Lowassa, ninaamini kwamba aliondolewa na rais period!, na sio anybody else, rais alipowasili Dodoma, Waziri Mkuu akakosa uwanjani wa ndege mimi nilikuwa mtu wa kwanza kusema hapa kwamba he is done na hii ilikuwa hata kabla ya kuandika barua yake ya kujiuzulu, meaning kwamba Lowassa alijua mapema kwamba hana confidence ya rais tena, sasa alijuaje?

Let's deal with the facts here, won't we?

Hatujui kama Lowassa aliondolewa na Rais.

Tunajua aliandika barua ya kujiuzulu.

Kuhusu u-hero wa kuachia madaraka mwenyewe, Lowassa amejiharibia mwenyewe kihistoria maana alisema anajiondoa kwa sababu "tatizo ni Uwaziri Mkuu." Alizira, kama anavyosema Mwanakijiji. Asingejitoa sababu ya "Uwaziri Mkuu," akasema "mimi sina makosa lakini naondoka kwa sababu ofisi yangu imeshachafuliwa" labda hapo tungempa credit kwa kuachia madaraka kwa kuheshimu ofisi.

Unwisdom ya Lowassa, ni kwamba, while in public ametangaza kuzira, officially sidhani kama kwenye barua kwa Rais alimwambia kwamba "naondoka kwa sababu hawa watu wana fitina na cheo cha Uwaziri Mkuu." Kwa hiyo, in the public eye, kajiharibia bure tu.

But then again, inawezekana kweli aliandika hivyo kwa Rais. Kuna mtu ameshawahi kuuliza Ikulu itoe nakala ya barua ya Lowassa ? Kwa crummy press ya Bongo sidhani. Hata tukio la kihistoria kama lile, hakuna hata kiumbe kimoja kati ya Waandishi wa Bongo aliyetaka kumuuuliza Rais kwamba aliambiwa nini kwenye barua ya Lowassa. Wanatudanganya "Rais amevunja baraza la Mawaziri." Amevunja vipi wakati limevunjika lenyewe automatically ?

Unless Kikwete alikataa ku sign barua ya Lowassa, akatengua baraza na Lowassa akiwemo, ili officially awe ameondolewa kwa kubadilishwa tu, kama vile Warioba au Msuya n.k. But, again, who knows in this country !

Kama unamaana hiyo, FMES, hapo inawekuwa sawa. Lakini sio kwa vigezo vya michongo ya Lowassa kukosa uwanja wa ndege basi Kikwete kamfukuza. Hiyo ni speculation ambayo hujui kama ni kweli.
 
1.
Let's deal with the facts here, won't we? Hatujui kama Lowassa aliondolewa na Rais. Tunajua aliandika barua ya kujiuzulu.

- Siasa haitengenezwi na facts peke yake, ndio maana huwa haina permanent truths, huwezi kusema ni a political fact kwamba rais wetu hakujua anything in advance kuhusu Membe na maneno ya OIC, sasa kuna facts ambazo zikionekana kwenye siasa huwa zinatabiri ukweli unaokuja katika siasa na hakuna sheria yoyote inayoweza kuvunjwa kwa mwananchi au wanaohusika kufanya huo utabiri na hakuna dhambi pia iwapo watadai credit kwa utabiri wao baada ya poliitical fact waliyoitabiri itatokea as of this case.

- Kabla ya kwenda Dodoma, tayari kulikuwa na speculations kwamba Mwakyembe, ana ripoti ambayo ina madudu mazito against marafiki wa rais, na kwamba rais mwenyewe in private ameruhusu Mwakyembe aipeleke bungeni kama ilivyo, sasa lets say ulikuwa ni uongo, rais alikwenda Dodoma kufanya nini wakati wa ripoti kutolewa bungeni?

- Kwa hiyo yes, tunaweza ku-discuss facts, lakini hakuna dhambi ku-discuss utabiri wa political facts yaani speculations za kuelekea kwenye, political facts zenyewe, unless kuna something else hapa hakijasemwa zaidi ya kujificha nyuma ya the so called "tujadili facts!"

2
. Kuhusu u-hero wa kuachia madaraka mwenyewe, Lowassa amejiharibia mwenyewe kihistoria maana alisema anajiondoa kwa sababu "tatizo ni Uwaziri Mkuu." Alizira, kama anavyosema Mwanakijiji. Asingejitoa sababu ya "Uwaziri Mkuu," akasema "mimi sina makosa lakini naondoka kwa sababu ofisi yangu imeshachafuliwa" labda hapo tungempa credit kwa kuachia madaraka kwa kuheshimu ofisi.

- Hapa tupo ukurasa mmoja.

3.
Unwisdom ya Lowassa, ni kwamba, while in public ametangaza kuzira, officially sidhani kama kwenye barua kwa Rais alimwambia kwamba "naondoka kwa sababu hawa watu wana fitina na cheo cha Uwaziri Mkuu." Kwa hiyo, in the public eye, kajiharibia bure tu.

- Again hapa tupo ukurasa mmoja.

4.
But then again, inawezekana kweli aliandika hivyo kwa Rais. Kuna mtu ameshawahi kuuliza Ikulu itoe nakala ya barua ya Lowassa ? Kwa crummy press ya Bongo sidhani. Hata tukio la kihistoria kama lile, hakuna hata kiumbe kimoja kati ya Waandishi wa Bongo aliyetaka kumuuuliza Rais kwamba aliambiwa nini kwenye barua ya Lowassa. Wanatudanganya "Rais amevunja baraza la Mawaziri." Amevunja vipi wakati limevunjika lenyewe automatically ?

- Wakati mbunge Masilingi, alipodai muongozo wakati wa kikao baada ya Lowassa kusema ameachia ngazi, Spika aliwakumbusha wabunge wote kua Lowassa bado ni Waziri Mkuu, mpaka Rais atakapotangaza kukubali barua yake ya kujiuzulu na akwakumbusha wabunge kwua rais amemfahamisha tayari yeye Spika, kuhusu kupokea barua ya kujiuzulu ya Lowassa.

- Tanzania tulishawahi kuwa na tabia za kutoa barua za viongozi wakuu kujiuzulu hadharani, I do not think so, sasa is it kwa sababu waandishi hawajawahi kuomba? I mean it is another million dollars question!

5.
Unless Kikwete alikataa ku sign barua ya Lowassa, akatengua baraza na Lowassa akiwemo, ili officially awe ameondolewa kwa kubadilishwa tu, kama vile Warioba au Msuya n.k. But, again, who knows in this country !
Kama unamaana hiyo, FMES, hapo inawekuwa sawa. Lakini sio kwa vigezo vya michongo ya Lowassa kukosa uwanja wa ndege basi Kikwete kamfukuza. Hiyo ni speculation ambayo hujui kama ni kweli.

- A sitting Rais wa Jamhuri anapokwenda mahali ambapo kuna a sitting Waziri Mkuu wake, kwa wale tunaofahamu vizuri ni excuse chache sana kama zipo kisheria za protocol zinaweza kukubalika, na katika hali ya mazingara haya ya kutolewa kwa ripoti bungeni inayomhusu Waziri Mkuu, alipokosa kuwepo uwanjani watabiri wengi wa siasa mimi nikiwa mmojawapo, tulitabiri kwamba ni dalili tosha kwamba mkuu yuko njiani kuondoka, and he did aliishia kuondoka kweli kama tulivyotabiri, sasa tatizo lako mkuu hapa liko wapi? Where?

Hayo mengine ya kutengua barua I have no clue umeyapata wapi? Kama the ishu ni kutoka kwa Lowassa, unataka kusema kwamba rais hakua anajua in advance kabla ya kwenda Dodoma? Na kwamba ilitokea tu kwa bahati mbaya au nzuri? Na hii ilitokea kwenye siasa za Tanzania?

Sometimes tukitumia hata common sense kidogo tu tunaweza kusaidia kutopoteza muda wa wananchi hapa JF.
 
Siasa haitengenezwi na facts peke yake, ndio maana huwa haina permanent truths, ... Kwa hiyo yes, tunaweza ku-discuss facts, lakini hakuna dhambi ku-discuss utabiri wa political facts yaani speculations za kuelekea kwenye, political facts zenyewe, unless kuna something else hapa hakijasemwa zaidi ya kujificha nyuma ya the so called "tujadili facts!"

Naomba urejee exchange moja uliyofanya na mchangiaji mwingine :

Mchangiaji:
Nadhani wakati wa Nyerere mstari kati ya chama na serikali ulikuwa…

FMES:
Sasa mkuu kweli unajenga hoja yote hii kwa kudhani tu?

Mchangiaji: Kutumia neno NADHANI ni kuruhusu mjadala! Niko tayari kusikiliza mawazo mbadala.

FMES: Nimekuuliza swali moja tu, kwamba kweli unaweza kujenga hoja kwa kutumia kudhani, umekuja na majibu mengi ambayo hayahusu swali langu kwako...
Kwa hiyo hata wewe hukubaliani na mpango wa kujenga hoja based on kudhani.

Kusema kwamba ilijulikana Lowassa angeondoka kwa sababu hakwenda airport siku ile ni speculations tu. Unasema nyinyi watabiri mliotea kwamba ataondoka, lakini huko ni kuchanganya issues. The issue is, mimi napinga unavyosema ni Kikwete ndio alimuondoa. Kutabiri hata Sheikh Yahaya naamini alitabiri, but that is not the issue here!

Unasema Rais alijua in advance ya kwenda Dodoma. Alijua nini, kilichomo kwenye ripoti, au kwamba Lowassa atajiuzulu? Kumbuka ile ripoti up to the minute Mwakyembe anamaliza kuisoma hakuna aliyejua - si Mwakyembe mwenyewe, si Rais, si Spika - hakuna aliyejua ni nini kitakuwa reaction ya Lowassa. Hata kama Kikwete alijua kilichomo kwenye ripoti kabla ya, bado hakuna aliyejua Lowassa ataamua kujiuzulu. That resignation was the first of its kind in our history. Hakuna aliyetegemea atajiuzulu.

Kuhusu kutolewa hadharani kwa barua ya kujiuzuku, swala hapa ni zito zaidi ya just "hatuna tabia" hiyo. Unajua mpaka leo hakuna Mtanzania, zaidi ya Kikwete na tarishi anaemfungulia barua, ambae anajua sababu rasmi aliyoitoa Lowassa ya kujiuzulu. Bungeni alichokisema – tatizo ni wivu wenu, chukueni cheo chenu – sidhani kama ndivyo alivyosema kwenye barua. Kwa hiyo, hili ni swala la kihistoria ambalo hakuna anaelijua. Kwenye rekodi rasmi za Bunge alisema essentially mimi nazira, kama alivyosema Mwankjj. Nasusa. That's what's known out in the public eye. But what is the official record ? Many will answer, "who knows,"? Lakini kwa Tanzania, the answer is, who wants to know ?

Halafu unaposema ni Kikwete ndio aliruhusu Ripoti ya Mwakyembe iende bungeni unakosea kwa sababu ile ilikuwa ni ripoti ya Bunge. Kikwete hakuwa na msemo pale. Kama wewe ni "mtabiri"wa mambo ya kisiasa then you should know this, FMES. Unaponishambulia "nitumie hata common sense kidogo", basi onyesha mfano, sio kuji expose kwamba vitu vya msingi kama hivi na wewe Mzee mzima vinakupita.
 
Naomba urejee exchange moja uliyofanya na mchangiaje mwingine :

Kwa hiyo hata wewe hukubaliani na mpango wa kujenga hoja based on kudhani.

The issue is, mimi napinga unavyosema ni Kikwete ndio alimuondoa. Kutabiri hata Sheikh Yahaya naamini alitabiri, but that is not the issue here!

Hata kama Kikwete alijua kilichomo kwenye ripoti kabla ya, bado hakuna aliyejua Lowassa ataamua kujiuzulu. That resignation was the first of its kind in our history. Hakuna aliyetegemea atajiuzulu.

Kuhusu kutolewa hadharani kwa barua ya kujiuzuku, swala hapa ni zito zaidi ya just "hatuna tabia" hiyo. Unajua mpaka leo hakuna Mtanzania, zaidi ya Kikwete na tarishi anaemfungulia barua, ambae anajua sababu rasmi aliyoitoa Lowassa ya kujiuzulu. Bungeni alichokisema – tatizo ni wivu wenu, chukueni cheo chenu – sidhani kama ndivyo alivyosema kwenye barua. Kwa hiyo, hili ni swala la kihistoria ambalo hakuna anaelijua. Kwenye rekodi rasmi za Bunge alisema essentially mimi nazira, kama alivyosema Mwankjj. Nasusa. That's what's known out in the public eye. But what is the official record ? Many will answer, "who knows,"? Lakini kwa Tanzania, the answer is, who wants to know ?

Lowasa alijua amesalitiwa, hakutegemea kuwa iko siku akiwa waziri mkuu atakuwa ktk kashfa ya moja kwa moja bila kulindwa. Aliushtukia mtandao wote na kuuona mtandao hauna maana as umeshindwa kumlinda, ndio maana alisusa.
 
1.
Re: Lowasa: Kuvuliwa Madaraka, Kujiuzulu na Kustaafu

Kwanza kabisa hicho juu ndio hasa kichwa cha hii mada.

2.
Naomba urejee exchange moja uliyofanya na mchangiaje mwingine :
Quote:Mchangiaji: Nadhani wakati wa Nyerere mstari kati ya chama na serikali ulikuwa…FMES: Sasa mkuu kweli unajenga hoja yote hii kwa kudhani tu?Mchangiaji: Kutumia neno NADHANI ni kuruhusu mjadala! Niko tayari kusikiliza mawazo mbadala.
FMES: Nimekuuliza swali moja tu, kwamba kweli unaweza kujenga hoja kwa kutumia kudhani, umekuja na majibu mengi ambayo hayahusu swali langu kwako, haya nimekubali naomba nikuachie mawazo yako!

Kwa hiyo hata wewe hukubaliani na mpango wa kujenga hoja based on kudhani.

- Great, nilipomuuliza mkuu kama anaweza kujenga hoja wka kutumia dhana ya kudhani, hakukubali, as opposed na mimi kwako nimesema nimejenga hoja based on kuamini, eti kuamini ni sawa na kudhani?

- Again nimekupa sababu zangu za kuamini, moja ikiwa Rais kufika uwanja wa ndege na waziri mkuu kutokuwepo uwanjani, pili speculations zilizokuwepo awali kwamba Mwakyembe ameruhusiwa na rais kwenda bungeni, na tatu kwamba after all this speculations ikawa Lowassa kuondoka, sasa yes nimejenga hoja based on kuamini na hoja imejitosheleza na results as of my predictions, based on kuamini, again hapa una tatizo wapi mkuu?

3.
Kusema kwamba ilijulikana Lowassa angeondoka kwa sababu hakwenda airport siku ile ni speculations tu. Unasema nyinyi watabiri mliotea kwamba ataondoka, lakini huko ni kuchanganya issues. The issue is, mimi napinga unavyosema ni Kikwete ndio alimuondoa. Kutabiri hata Sheikh Yahaya naamini alitabiri, but that is not the issue here!

- Waziri Mkuu hakwenda airport kumpokea rais, kwangu maana yake ni kwamba waziri mkuu alijua mapema kwamba rais hamuhitaji tena, kutokana na speculations zilizokuwa zimeenea kwamba rais amepelekewa ripoti na Mwakyembe, akaonywa kua kuna marafiki zake ndani na ripoti ina madudu, lakini akamruhusu aende nayo bungeni anyways, kitendo ambacho Lowassa alikijua tayari politically kikiwa na maana kwamba rais anakubaliana na yaliyomo, angekua hakubaliani nayo asingeiruhusu kufika bungeni, hivyo kumfanya waziri mkuu kijiaandaa kutoka kutokana na alama ya yeye kutokwenda uwanjani kumpokea rais.

- Pili rais hakua na ziara iliyokuwa imetayarishwa rasmi ya kwenda Dododoma wakati wa ripoti kutolewa, rais akaenda Dodoma na kupumzika Chamwino, kwangu ni alama ya nyakati kwamba alijua mapema yote yaliyofuatia ikiwa ni pamoja na kuondoka kwa Lowassa, na yeye kuvunja cabinet.

Hizi ni hoja zangu ndogo nilizojengea hoja kubwa ya kuamini kwangu kwamba rais ndiye aliyemuondoa Lowassa, I still stand behind my words, sasa again tatizo liko wapi hapa mkuu?

4.
Unasema Rais alijua in advance ya kwenda Dodoma. Alijua nini, kilichomo kwenye ripoti, au kwamba Lowassa atajiuzulu? Kumbuka ile ripoti up to the minute Mwakyembe anamaliza kuisoma hakuna aliyejua - si Mwakyembe mwenyewe, si Rais, si Spika - hakuna aliyejua ni nini kitakuwa reaction ya Lowassa. Hata kama Kikwete alijua kilichomo kwenye ripoti kabla ya, bado hakuna aliyejua Lowassa ataamua kujiuzulu. That resignation was the first of its kind in our history. Hakuna aliyetegemea atajiuzulu.

- Ni wewe ndiye hukujua, lakini mimi nilijua na ukienda huko nyuma utayakuta maandiko yangu yako wazi, nilisema ifuatavyo, behind the scene kabla ya kwenda Dodoma, Mwakyembe alipita kwa vigogo wote wa CCM, au kama nilivyosema "the brass" kuomba ushauri kutokana na yaliyokuwemo kwenye ile ripoti yanayowahusu marafiki wa rais, nikasema alipewa okay na wote ambao walimuarifu rais in advance kwamba wameipitisha na iko njiani kwenda kwake.

- Nikasema alipofika nayo kwa rais, rais alikataa hata kuiangalia akamuambia atangulie nayo Dodoma na yeye anakuja nyuma. Nikasema Lowassa alijaribu kwenda kwa rais kumuomba amsaidie at the last minute kabla ya kwenda Dodoma, rais akamuambia akasimame mbele ya taifa, yaani bungeni ajitetee yeye hawezi kumsaidia.

- Nikasema walipofika Dodoma, kilifanyika kikao cha wabunge wa CCM, ambapo yalifanyika mawili, moja kuchagua wajumbe watatu wa kwenda kwa rais Chamwino kumfikishia ujumbe wao on the ishu ya Lowassa, na pili Mkamba kujaribu kuwatisha wabunge kutokubali ripoti.

- Nikasema, Chamwino walienda Ameir, Makamba, na Malecela, wakatoa ujumbe wao, ambapo Mkamba na Ameir, walimtetea Lowassa, lakini ni Malecela ndiye aliyemuonya rais kwamba iwapo Lowassa asingetoka, basi wabunge wangemuwajibisha anyways, na rais akakubali hii hoja.
(Habari ambayo baadaye ilithibitishwa hata na magazeti yetu).

Kwa hiyo hapa mkuu, ni wewe tu ndiye ulikuwa hujui, lakini mimi nilikuwa ninajua, kama ambavyo nilikuwa ninajua kuwa atapewa yeye uwaziri mkuu rejea BCS nilipotabiri mapema.

5.
Kuhusu kutolewa hadharani kwa barua ya kujiuzuku, swala hapa ni zito zaidi ya just "hatuna tabia" hiyo. Unajua mpaka leo hakuna Mtanzania, zaidi ya Kikwete na tarishi anaemfungulia barua, ambae anajua sababu rasmi aliyoitoa Lowassa ya kujiuzulu. Bungeni alichokisema – tatizo ni wivu wenu, chukueni cheo chenu – sidhani kama ndivyo alivyosema kwenye barua. Kwa hiyo, hili ni swala la kihistoria ambalo hakuna anaelijua. Kwenye rekodi rasmi za Bunge alisema essentially mimi nazira, kama alivyosema Mwankjj. Nasusa. That's what's known out in the public eye. But what is the official record ? Many will answer, "who knows,"? Lakini kwa Tanzania, the answer is, who wants to know ?

- Hapa umeniacha nje, maana sina anything to do na hii point, ninajua for fact, kwamba Spika aliwaambia wabunge kwamba Lowassa, bado ni waziri mkuu, na kwamba rais amemtaarifu asubuhi kwamba amepokea barua ya kujiuzulu ya Lowassa, na kwamba mpaka atakapojibu Lowassa bado ni waziri mkuu, how do I know this ninazo tepu zote za ile procedure mwanzo mpaka mwisho, je barua iliandikwa nini I have no clue na wala sijajaribu at anytime ku-speculate on that ishu.

6.
Halafu unaposema ni Kikwete ndio aliruhusu Ripoti ya Mwakyembe iende bungeni unakosea kwa sababu ile ilikuwa ni ripoti ya Bunge. Kikwete hakuwa na msemo pale. Kama wewe ni "mtabiri"wa mambo ya kisiasa then you should know this, FMES.

- Mimi si mtabiri kama Sheikh Yahya, hapana mimi ninatabiri based on Ze -dataz at hand, yaani ambazo ninazo pamoja na speculations, kwenye siasa hii inakubaliika lakini kwenye mahakama huwezi fanya hivyo, yaani kutabiri ni lazima uwe na legal facts hapo ndipo wewe unaweza kua na hoja kuhusu mimi na utabiri, lakini sio kwenye siasa huku anybody anaruhusiwa kutabiri based on the facts anazozijua au Ze dataz, again hapa huna hoja mkuu!

Halafu kama utakumbuka huko nyuma kuna siku niliwahi kutabiri kwamba Lowassa hawezi kupewa umakamu wa CCM, kwa sababu mtoto wake alijenga nyumba ya shilingi millioni mia sita, ambayo muungwana alienda kuiona mwenyewe usiku mmoja kabla ya kwenda Dodoma, kwenye kikao hicho, na kweli Lowassa hakupewa, pamoja na juhudi zake zote za kukitaka hicho cheo.

7.
Unaponishambulia "nitumie hata common sense kidogo", basi onyesha mfano, sio kuji expose kwamba vitu vya msingi kama hivi na wewe Mzee mzima vinakupita.

- Kukuomba utumie japo commonsense kidogo, ni kukushambulia? Hapana unless kuna something I am missing hapa!

- Nionyeshe mfano on what? Haya ya mzee nimekuambia mara kwa mara mimi sio mzee, na ninaomba kukumbusha tena mimi sio mzee, kuna mahali umedai nina mika 55 nimekuambia hata 50 sijafika bado saana mkuu, can we put this ishu to the rest, mimi sio mzee na nisingependa kujua umri wako, please!

Ahsante Mkuu!
 
Unaenda kupiga tizi ? Tuambiane.

Hapana mkuu, nilikuwa napeleka watoto wangu kwenye kuogelea si unajua kila siku jioni, halafu unajua umuhimu wa waoto na michezo au?

Mimi Tiz huwa ninapiga saa tisa asubuhi, kabla ya kwenda kubaruani, maana wakuu wa afya wanashauri biashara asubuhi, sio jioni, au?

Thanx for asking, Bwa! ha! ha! ha! ha!
 
Sasa tum-address vipi? "Waziri Mkuu wa Zamani" au "Waziri Mkuu Mstaafu"

Tukumbuke kuwa Waziri Mkuu Mstaafu anabeba heshima ya Waziri Mkuu maisha yake yote, na hilo ndilo jambo ambalo silikubali kabisa kwa Lowasa; mtu huyu hana hata chembe moja ya heshima hiyo.
 
Hebu tuangalie scenario mbili:

1. EL anakataa kujiuzulu na wabunge wanapiga kura ya kutokuwa na imani naye, sasa kitu gani kinafuata. Je, Raisi anawajibika kumfukuza, kumstaafisha ama kumvua madaraka ?

2. El anakataa kujiuzulu na Raisi anavunja baraza la mawaziri na kuunda jipya waziri mkuu akiwa mwingine. Je, hapa EL amefukuzwa, amevuliwa madaraka ama amestaafishwa ?

Kati ya haya mawili je, ni wapi anastahili kuitwa waziri mkuu mstaafu ? Tunachojua kwa hakika ni kuwa Raisi alisikitika sana EL kujiuzulu.

Sasa kumpigia waziri mkuu kura ya kutokuwa na imani naye kunahitaji idadi ya wabunge wangapi na je , hiyo idadi ingepatikana ?

Je kama Raisi asingemchukulia hatua yoyote, bunge la CCM lingekuwa na ubavu wa kumwajibisha Raisi ? Je Raisi pia angepigiwa kura ya imani ?

Je wengine wote ambao kamati ya Mwakyembe ilitoa mapendekezo wachukuliwe hatua, ni hatua gani zimechukuliwa mpaka sasa tukimwacha EL, Karamagi na Msabaha walioamua kujiuzulu? Je si wengine bado wana madaraka yao k.m. Hosea, Mwanyika, Mgonja na wengineo ?

Namaliza kwa kusema alilofanya Lowasa lilikuwa tendo la kijasiri ingawa halimtoi kwenye genge la MAFISADI. Tume ya Mwakyembe kwa kutoa ripoti isiyokamilika kwa kile walichokiita kutunza heshima ya serikali kuliinyima hiyo tume credibility.

Nataka nieleweke kuwa sina ubia na EL wala simtetei kwa madhambi yake bali mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Nasubiri kwa hamu siku atakapofikishwa mahakamani na bila shaka akipatikana na hatia nitakuwa wa kwanza kudai avuliwe hata hilo jina.
 
Sasa tum-address vipi? "Waziri Mkuu wa Zamani" au "Waziri Mkuu Mstaafu"

Tukumbuke kuwa Waziri Mkuu Mstaafu anabeba heshima ya Waziri Mkuu masiha yake yote, na hilo ndilo jambo ambalo silikubali kabisa kwa Lowasa; mtu huyu hana hata chembe moja ya heshima hiyo.

Mkuu Kichuguu,

Heshima mbele sana, kwa kweli hiki ni kitendawili kikubwa sana, binafsi ninaomba siku chache tu, nifanyie utafiti wa kina wa hii ishu ya Lowassa, in the process nitawauliza wakulu wote waliohusika in one way or another, na nitakutumia majibu.

Ahsante Mkuu.
 
Back
Top Bottom