Lowasa: Kuvuliwa Madaraka, Kujiuzulu na Kustaafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowasa: Kuvuliwa Madaraka, Kujiuzulu na Kustaafu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Nov 12, 2008.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Nov 12, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Wanaforum,

  Sheria moja ya kazi huwa inaweka conditions za mtu kulipwa mafao baada ya kuacha kazi; sheria hii huwa inaelekeza kuwa mtu atalipwa mafao yake ya mwisho endapo tu mtu huyo ataacha kazi yake ile honorably: yaani ame amestaafu au kustaafishwa, siyo kufukuzwa na mwajiri wake au kwa kujiuzulu mwenyewe. Katika kuzuia waajiri wasiwe wanawafukuza waajiriwa wao makusudi ili kukwepa kuwalipa mafao, kuna vyombo mbalimbali vya kuwathibiti ikiwa ni pamoja na mahakama ya kazi.

  Sababu za mtu kuacha kazi honorably ni pamoja na umri au afya yake, muda aliokwisha fanya kazi kwa mwajiri yule, na kuisha kwa uhai wa kazi ile bila matakwa yake mwenyewe (kustaafishwa.) Sote tunajua wazi kabisa kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya kustaafishwa na kufukuzwa kazi.

  Sasa sababu ya kuandika hayo ni pale ninapoona kuwa Lowasa anakuwa addressed kama Waziri Mkuu Mstaafu ( ikiwa na maana kuwa ana haki ya kulipwa mafao yake ya kazi) huku inajulikana kuwa hakuachia madaraka yale honorably. Nionavyo mimi ni kuwa Lowasa ni Waziri Mkuu wa Zamani, yeye ni tofauti na wenzie kama Sumaye, Msuya, Malecela, Warioba, Salim, Sokoine, na Kawawa ambao ndio mawaziri wakuu waliostaafu. Lowasa anaweza kuwa grupu moja na Nyerere kwa vile Nyerere naye alijiuzulu Uwaziri Mkuu ingawa sababu zao za kujiuzulu ni diametrically opposite. Hatujawahi kumwita Nyerere kama waziri mkuu mstaafu kwa vile hakustaafu madaraka yale; ila katika kumbukumbu huwa tunasema kuwa alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza.

  Lowasa angeweza kuonekana kuwa ameachia madaraka hayo honorably, endapo angetengeneza mazingira yayanyoonyesha kuwa uhai wa madaraka yale umekwisha bila yeye mwenyewe kutaka, kwa mfano kama rais angevunja baraza lote la mawaziri na kuliunda upya huku nafasi ya waziri mkuu ikiwekwa mikononi mwa mtu mwingine bila kumhukumu Lowasa. Kwa vile Lowasa alijiuzulu kwa hiari yake mwenyewe na hivyo kuvuruga uhai wa madaraka yake yeye mwenyewe, basi mtu huyu si mstaafu na wala hastahili kulipwa mafao ya mwisho wa kazi. Tukiruhusu Lowasa apewe hadhi ya Waziri Mkuu mstaafu basi tutakuwa tunaweza mazingira mabaya sana ya kimaadili. Tutakuwa tumeruhusu watu watakaopewa madaraka haya kuyatumia vibaya halafu wakakimbilia kujiuzulu ili waendelee kupata marupurupu ya Uwaziri Mkuu. Hebu fikiria kuwa kama katika kipindi cha miaka mitano kila waziri mkuu atakuwa anajiuzulu baada ya miezi miwili na kuhesbabiwa kuwa ni waziri mkuu mstaafu; je, taifa litaishia kulea mawaziri wakuu wastaafu wangapi?


  Moderator

  Inawezekana topiki ya aina hii iliwahi kujadiliwa huko nyuma; samahani kwa kuirudia ila naomba uipe thread hii muda kidogo kabla hujaiunganisha na zinazofanana.
   
 2. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichuguu,

  inawezekana kuna wengine wanaona kujiuzulu kwa Lowassa kama ni uamuzi wake mwenyewe na hivyo kuuchukulia huo uamuzi kama kustaafu?!? Au wewe unaonaje?
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Nov 12, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Ni uamuzi alioutoa kutokana na kashfa zilizokuwa zinamkabili. Kwa vile alitangaza kujiuzulu, basi alijikosesha nafasi ya kuwa mmoja wa wastaafu, anabaki kuwa Waziri Mkuu wa Zamani. Angekuwa amefanya busara kama angemshawishi Rais avunje baraza la mawaziri na kuliunda upya bila yeye kuwemo; hapo uhai wa ajira yake ungekuwa imefikia kikomo bila matakwa yake na vile vile bila kufukuzwa, na angekuwa waziri Mkuu Mstaafu kwa kustaafishwa.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Lowassa hakujiuzulu (resign), wala hakustaafu (retire), na wala hakufukuzwa (fired); Alichofanya Lowassa ni kuzira (quit). Now, anachoweza kuitwa ni Quiter! He is a quiter that is someone who quit his job! Yes he did.

  We can decide to reward quiters if we want but quiters are what they are.
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Nov 12, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  quit kwa kiswahili ni nini kwa jinsi alivyofanya lowassa inabidi iwe na neno lake maalumu
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kichuguu

  huoni kuwa kuachwa katika baraza jipya la mawaziri kwa waziri mkuu ambaye kashfa ilikuwa inamuandama kama Lowassa ni sawa na rais kumfuta kazi na hivyo kutafsiriwa kama kafukuzwa kwa kashfa iliyokuwa inamuandama??
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kujiondoa!!!!!
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Nov 12, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,737
  Likes Received: 4,960
  Trophy Points: 280
  Kichuguu,

  ..you have raised vety interesting points.

  ..inawezekana Lowassa aliyaona haya unayoyasema hivyo akajihami kwa kujiuzulu.

  ..sijui kungetokea nini kama angeamua kupingana na findings za kamati ya Mwakyembe.

  ..wabunge walipaswa kujadili tuhuma zilizoelekezwa kwa Waziri Mkuu na ama kuzikubali au kuzikataa. uzembe huo wa Wabunge wetu ndiyo umesababisha huu utata na kutoa upenyo kwa Lowassa kupewa hadhi ya retired PM.
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Nov 12, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Ni kweli, lakini bado kiutaratibu hiyo ingechukuliwa kuwa ni reshuffle ya kawaida ifanywayo kwa matakwa ya rais mwenyewe ambapo ana uhuru wa kumpa madaraka hayo mtu mwingine yeyote yule. Ni kama ambavyo Nyerere alivyomwondoa Kawawa kutoka madaraka ya waziri Mkuu na kuyatoa kwa Sokoine; hiyo ilikuwa ni reshuffle ya kawaida kufuatia matakwa ya rais mwenyewe.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Nov 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kaangalieni maneno aliyotumia kulitaarifu Bunge mtajua kama alijiuzulu, kustaafu au kuondolewa... mtakuta kuwa aliamua "kuquit"!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Nov 12, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Good point, lakini hata hivyo kwa vile Lowasa alikataa madaraka ya waziri mkuu kwa sababu zisizotambulika kwa mstaafu, yeye siyo Waziri Mkuu Mstaafu eti; ni Waziri Mkuu wa Zamani.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Nov 12, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,737
  Likes Received: 4,960
  Trophy Points: 280
  Kichuguu,

  ..kama sijakosea Ballali alijaribu ku-resign lakini Raisi akakataa, na badala yake "akatengua" uteuzi wake.

  ..sijui ni kwa misingi ipi Raisi alikubali resignation ya Lowassa. pia haieleweki Lowassa alipoomba kwa Raisi kujiuzulu, aliomba kwa misingi na sababu zipi.

  ..kwa kweli ktk suala hili inabidi wananchi wamhoji Raisi wao.
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama ni hivyo basi angemuacha Lowassa mpaka issue ya Richmond ipoe na kuvunja baraza, lakini kitendo chochote cha kuvunja baraza wakati wa kashfa ya richmond inayomkabili PM ingekuwa ni sababu tosha ya EL kuonekana kaachwa kwa kashfa. Na kama angemuacha mpaka 2010 basi JK angekuwa kwenye kikaango saa hizi kuhusu hilo la PM,

  Kwa kifupi ni kwamba there is "Lakuna" Gap in our laws kuhusu how we can treat situation kama ya Lowassa kwa kuwa ni PM wakwanza kukutwa na situation hiyo katika historia ya TZ. Mjadala hapa ungekuwa tufanye nini ili wengine watakaokumbwa na situation kama ya EL siku zijazo wasifaidike na status ya "Waziri mkuu mstaafu"?
   
 14. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Okay,

  Hapa nimekuelewa mkuu.
   
 15. F

  Fataki Senior Member

  #15
  Nov 13, 2008
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naomba kusisitiza kuwa Lowassa alijiuzulu kwa kutumia maneno yafuatayo Bungeni: "nimeamua kumwandikia barua Mhe. Rais, niachie ngazi". Kuachia ngazi ni kujiuzulu! Hivyo basi, Lowassa hakustaafu, alijiuzulu. Ni makosa kumwita Waziri Mkuu mstaafu, yeye ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu au Waziri Mkuu wa zamani au simply "aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa". Kumwita Waziri Mkuu mstaafu ni kumpa heshima asiyostahili, heshima ya kwamba alimaliza muda wake wa miaka mitano pamoja na Rais aliyemteua.

  Limeulizwa swali: "kungetokea nini kama angeamua kupingana na findings za kamati ya Mwakyembe?" Jibu langu ni kuwa: Edward Lowassa angeishia kupigiwa vote of no confidence chini ya ibara ya 53A ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977. Nimeongea na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Mwakyembe na kugundua kuwa timu nzima (Mwakyembe, Manyanya, Selelii, Mnyaa na Mntangi) ilikuwa imejiandaa usiku kucha ikitegemea Lowassa kujibu mapigo na kukataa "kujipima". Lowassa mjanja bwana. Inasemekana kachero wake mkuu Peter Serukamba (Mbunge wa Kigoma), alikuwa anafuatilia mwenendo wa wana Kamati. Akagundua kuwa walikuwa na masanduku ya ushahidi nyeti, ushahidi ambao ulimgusa hata Serukamba mwenyewe ambaye anatajwatajwa kuwa ndiye aliyemshawishi mtoto wa Lowassa, Fred, kuibeba Richmond hadi kwa baba yake kwa ujira wa sh. 100,000,000 tu! Serukamba akamshauri Lowassa heri ajiuzulu kuliko kuumbuliwa. Ndipo Lowassa akatoa ile famous statememt ya kuzira: Nimeonewa sana, nimedhalilishwa sana, nime .......................
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Nov 13, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu, Lowassa hakujiuzulu, hakustaafu wala hakufukuzwa kazi; alizira.

  Ballali aliandika barua kwa Rais kumueleza kuwa ameamua kujiuzulu kwa sababu za kiafya na kushindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na hali hiyo. Kujiuzulu kwake hakukuwa effected hadi Rais akubali. Rais hakumkubalia na badala yake akatengua uteuzi wake.

  Lowassa hakufanya hivyo; wakati anasimama kuzungumza Bungeni na kutangaza kuwa amezira kazi alitumia maneno fulani; yatafuteni mtapata jibu lenu!
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kichuguu,

  Ukisoma sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa Wastaafu, ya 1993, bahati mbaya haitofautishi kabisa kati ya kustaafu, kujiuzuru, ku-quit, kuzira, kufukuzwa, kuachishwa, kususa, kuwa impeached, kuachia ngazi...

  THE POLITICAL SERVICE RETIREMENT BENEFITS ACT, 1999 No. 3
  Part I, Sect 4

  INTERPRETATION

  In this Act, ''former President'' means a person who has held the office of the President of the United Republic, but has ceased to hold that office and the expressions ''former Vice President, ''former Prime Minister'', ''former Minister'' and ''former Deputy Minister'' shall be construed accordingly.


  Hii sheria ya Wastaafu inatuambia vigezo viwili:
  1. "who held the office"
  2. "has ceased to hold that office."
  Hawasemi - na haijalishi - kiongozi ali "cease" vipi.

  Kwa maneno mengine, hata ukimkamata Waziri Mkuu, kwa mfano, anafanya subversion, halafu akafukuzwa kazi in disgrace, kwa mujibu wa sheria, huyu msaliti nae 1) alishika madaraka 2) akasimama kushika madaraka. Na huyu nae atapata heshima na mafao yake kama waliostaafu kwa kumaliza muda wao kwa heshima.

  Sasa hii sheria inaitwa ya wastaafu. Kwa hiyo wote ni wastaafu. Malue lue matupu.
   
 18. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kulinga na Katiba ya Tanzania, Ibara ya 57(2) hakuna kitu kinaitwa kuzira kama mwkjj alivyosema katika mambo yanayoweza kumfanya waziri mkuu aache nafasi yake. Lowasa impliedly alijiuzuru uwaziri mkuu. I will give him benefit of doubt kwamba alimwandikia barua rais na akakubali kujiuzuru kwake.

  Lowasa kwa kupitia wanasheria wake walish jua kwamba Bunge lingeweza kumpigia kula ya kutokuwa na imani naye na angeweza kupoteza "come back" kwenye siasa. So they played well.

  Sheria yetu ya mafao hiko kimya kuhusu ni nani anayeweza kufaidika nayo. Suala hilo ni subject to interpretation on the issue whether or not former PM means atawalioondoka kwa tuhuma za wizi etc.

  Shadow.
   
 19. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #19
  Nov 13, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Kwa hiyo ni muhimu tubadilishe Katiba ili kutenganisha viongozi waliomaliza vipindi vyao honourably na wale walioondolewa madarakani with disgrace. Kumwita Lowasa Waziri Mkuu Mstaafu na kumpa hadhi sawa na akina Sokoine, Kawawa, Salim, Msuya, Malecela, Waryoba na Sumaye ni kutukana na kupunguza hadhi za hao waliomtangulia.
   
 20. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #20
  Nov 13, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kumbuka hilo ni bunge la CCM lililopitisha hizo sheria za ajabu ajabu kwani wanajijua kwamba Code of Conduct kwao ni sufuri...Kama wangekuwa hawalindani huwezi kuweka sheria robo robo. Mfano hiyo definition ya Prime minister means ' former prime minister' kazi kweli kweli . CCM chonde chonde someni nyakati ...hata wakiibadili hiyo sheria, Lowasa kisha peta si unajua sheria does not act restrospectively teh teh teh.
   
Loading...